Mwananchi wa chini
JF-Expert Member
- Jul 23, 2013
- 227
- 599
Anaandika Dk Yahya Msangi (Phd) West Afrika
Kwa kweli Tanzania hakuna vyama vya kuweza kuitoa CCM!
Hebu fikiria: Sasa hivi kuanzia BBC, DW, SPACE mjadala ni nani yuko sahihi kuhusu kuachiliwa Mbowe (mtuhumiwa wa ugaidi).
Mosi: katika utawala wa sheria na wa kidemokrasia ni mahakama pekee ndio chombo kinachoweza kuamua nani anayo au nani hana hatia kwa kosa alilotuhumiwa nalo. Chombo au mtu mwingine yeyote hawezi kudai mshitakiwa anayo au hana hatia.
Inashangaza vyama vya upinzani ambavyo ndivyo vinavyodai demokrasia na utawala bora ndivyo sasa vinatoa hukumu dhidi ya mshitakiwa. Ndivyo vinadai kesi ni ya kubumba na mashtaka ya kuchongwa! Wanasahau miezi michache tu iliyopita walidai mahakama imetenda haki dhidi ya Sabaya.
Na vinasahau Sasa vinajitahidi kumfikisha Paulo Makonda mahakamani kwa madai kuwa sheria ifuate mkondo!
Sijui akitokea mtu akadai mashitaka dhidi ya Sabaya na Makonda ni ya kubumba na mashahidi ni wa kuchonga watakubali? Hivi hawaoni dunia inawadharau kutokana na ukigeugeu (double standard) aina hii?
Na hivi BBC na DW hawajui kanuni hii ya utawala wa sheria? Hivi UK na German inawezekana watu au chombo kisicho mahakama kutoa hukumu? Ni kujishusha sana kujikita kujadili huu upuuzi. Tofauti kati ya BBC na DW na 'radio mbao' ni ipi kama hili ni suala zito kwao? Matumaini yangu - kwa kuwa sasa Zuhura uko Ikulu utawashauri wenzio vyema.
Pili: hii vita ni kichekesho cha mwaka. Nakifananisha na msiba. Pametokea msiba halafu akaja jirani akaanza kulia kuzidi ndugu wa marehemu! Ndugu wa marehemu wanaona wivu kuzidiwa wakaamua kumuonya jirani anyamaze. Jirani kakataa kunyamaza! Anadai yéyé na marehemu ni ndugu! Ni kaka yake na eti ndugu wenyewe hawana uchungu kama yéyé!
Hivi hizi pande mbili hakuna hâta mmoja mwenye chembe ya busara? Ni faida gani wanapata kubishana nani ndugu wa marehemu zaidi ya mwingine? Hivi busara tu ya kawaida si kuambiana "kila mmoja afanye linalowezekana kufanikisha mazishi"? Mnabishana hadi live kwenye tv, redio na mitandao eti "mimi ndio nina mpango mzuri zaidi wa mazishi"?
So what? Hebu kueni! Utoto mpaka lini?
Kweli mfanye upuuzi wa kiwango hiki halafu mtegenee wana kijiji wawape uongozi?
Tatu: hivi hamuoni mnagombea kilo ya hewa (a fight over 1 kilogram of air)? Aliyeombwa asamehe kasamehe?
Mnavyokashifiana mtu atadhani aliyeombwa na Zitto kasamehe au alitaka kusamehe akazuiwa na kina Mnyika! Ni sawa watoto kugombana kwa pipi ambayo hâta haijanunuliwa! Kila Moja linalia "yanguuuu, yanguuuu!"
Nne: Kumbukeni mahakama ileile mliyoisifu kwa kumkuta Sabaya na hatia ndiyo mahakama hiyo hiyo inayosikiliza shtaka dhidi ya Mbowe. Mnachotakiwa ni kusubiri itoe hukumu. Mkifurahi sawa mkichukia mkate rufaa. Ndio utawala wa sheria mnaoudai miaka yote.