Bado Hujasema
Member
- Dec 1, 2024
- 15
- 20
Nimesoma taarifa hii nachelea kusema kuwa Kenneth Simbaya amalizane na hao waratibu. Hii ni aibu na fedheha kwa Taasisi kubwa nchini.
---
Sisi Waratibu wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania, tuliokuwa/ tulioajiriwa kupitia Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) chini ya mpango unaofadhiliwa na Swedish International Development Cooperation Agency (SIDA), tunatoa taarifa hii kwa umma kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za ajira unaoendelea kutukabili.
Mnamo tarehe 02 Disemba 2025, waratibu tulipokea notisi za kusitishiwa mikataba ya ajira kupitia barua pepe binafsi ya afisa wa UTPC badala ya mfumo rasmi wa taasisi. Notisi hizo zilionyesha kusitishwa kwa ajira kuanzia tarehe 31 Disemba 2025. Utaratibu huu uliibua mashaka makubwa juu ya uhalali wa kisheria wa mchakato huo, ikiwa ni pamoja na kutokuzingatia misingi ya haki ya kusikilizwa na kupata stahiki za ajira.
Mbali na kusitishiwa mikataba ya kazi kiholela, waratibu hatujalipwa mishahara kuanzia mwezi Septemba 2025 licha ya kuendelea kutekeleza majukumu yetu kikamilifu. Kitendo hiki ni ukiukwaji wa wazi wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366, ambayo inamtaka mwajiri kuhakikisha malipo ya mishahara yanafanyika kwa wakati na kwa mujibu wa makubaliano ya ajira.
Aidha, michango ya Hifadhi ya Jamii (NSSF kwa Tanzania Bara na ZSSF kwa Visiwani) kwa baadhi ya waratibu haijawasilishwa kwa vipindi tofauti visivyopungua miezi saba, licha ya kufanya ufuatiliaji mara kwa mara, hali inayohatarisha haki za msingi za hifadhi ya jamii na ustawi wa wafanyakazi na kukiuka Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, kifungu cha 12 na 13, pamoja na Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar, ambavyo vinamtaka mwajiri kusajili wafanyakazi, kukata michango yao na kuiwasilisha kwenye mfuko husika kwa wakati. Kushindwa. kufanya hivyo kunaweza kusababisha adhabu za kisheria ikiwemo kutozwa riba, faini, na hatua nyingine za kisheria dhidi ya mwajiri kwa mujibu wa sheria hizo.
Piła, waratibu hatujalipwa stahiki zetu za mwisho wa ajira wala hatujakabidhiwa Vyeti vya Utumishi (Certificates of Service), kinyume na matakwa ya sheria. Tunasisitiza vyeti hivyo vitolewe na UTPC wenyewe na si vinginevyo ili ziweze kutusaidia tunapoenda kudai haki zetu kwenye taasisi nyingine ambazo zinamtambua UTPC kama mwajiri wetu.
Jambo la kushangaza, tumefuatilia na kubaini kuwa kuna baadhi ya waratibu, makato ya Kodi ya Mapato ya Ajira (PAYE) yaliwasilishwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hadi kufikia mwezi Novemba 2025, wakati ambapo mishahara halisi haikulipwa kwa wafanyakazi hao. Kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332, hususan vifungu vya 7 na 81, kodi ya PAYE inapaswa kukatwa na kuwasilishwa pale ambapo mapato ya ajira yamelipwa kwa mfanyakazi. Hivyo, uwasilishaji wa PAYE bila kuwepo kwa malipo halisi ya mshahara unaweza kuashiria utoaji wa taarifa zisizo sahihi za mapato na ukiukwaji wa sheria za kodi, jambo linalopaswa kuchunguzwa na mamlaka husika.
Aidha mwajiri wetu amekua akikata 3% ya mshahara kwa kila mmoja wetu kama makato Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) fedha ambayo hatuna uhakika kama ilikuwa ikiwasilishwa kwenye mfuko huo kwani hakuna mratibu hata mmoja kati yetu aliyewahi kupata matitabu au kuwa na kadi ya bima ya afya kupitia ajira hii.
Madai Yetu:
1. Kulipwa mara moja mishahara yote iliyocheleweshwa.
2. Kuwasilishwa kwa michango yote ya NSSF pamoja na uthibitisho wake.
3. Kulipwa kwa stahiki zote za mwisho wa ajira.
4. Kulipwa fidia kwa kuvunjiwa mikataba kinyume cha sheria.
5. Kutolewa mara moja kwa Vyeti vya Utumishi.
6. Kurejeshewa makato ya NHIF kwa kipindi chote cha ajira.
Tunaziomba mamlaka husika, hususan NHIF, NSSF/ZSSF, WCF, TRA, CMA na TAKUKURU, kufanya uchunguzi wa kina juu ya suala hili ili kujiridhisha na kuhakikisha haki za wafanyakazi zinalindwa kwa mujibu wa sheria za nchi kwa kuwachukulia hatua wote watakaobainika kukiuka. sheria hizi.
Sambamba na hilo, Umoja wa Waratibu kwa kushirikiana na jopo la wanasheria wetu m wadau. wengine wapenda haki tunaendelea kuandaa hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja na kufungua shauri katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na kuwasilisha malalamiko katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili kufanyika uchunguzi wa kina kuhusu mwenendo mzima wa suala hili.
Kabla ya kufikia hatua hii, tulichukua juhudi za ndani kutafuta suluhu ya amani, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha madai rasmi kwa UTPC na kutoa notisi ya mwisho ya kisheria ambayo iliyomalizika tarehe 13 Machi 2026. Hata hivyo, hakukuwa na utekelezaji wowote wa matakwa yetu wala majibu ya kuridhisha yaliyotolewa na UTPC.
Tuliwasiliana na mfadhili (SIDA) ili kutaka kujua utatuzi wa jambo hili alitujibu kwa maandishi na kuthibitisha kuwa mwezi Mei alituma SEK 2,300,000 sawa na zaidi ya Tsh 630,000,000 mwezi Desemba, 2025 alituma kiasi cha SEK 500,00 sawa na zaidi ya Tsh. 135,000,000 kwenda kwa UTPC kwaajili ya uendeshaji wa shughuli za kiofisi ikiwa ni pamoja na mishahara ya watumishi. Kwa mwaka 2025 mfadhili ametoa zaidi ya Tsh. 735,000,000 kama ufadhili kwa UTPC.
Tunatoa tahadhari kwa taasisi mashirika mengine yanayofanya kazi na UTPC kwa kufadhili miradi mbalimbali inayoendelea, kuwa makini na kufuatilia kwa ukaribu matumizi sahihi ya fedha na mienendo ya miradi inayotekelezwa chini yao.
Kwa kumalizia tunasisitiza kuwa lengo letu ni kulinda haki za kisheria za waratibu, kuhimiza uwajibikaji, na kuhakikisha uwazi katika taasisi zinazohudumia sekta ya habari nchini. Tunaamini na kusisitiza kuwa "Haki za wafanyakazi ndani ya taasisi za sekta ya habari zinapaswa kuwa mfano wa kuigwa" uhuru wa vyombo vya habari tunaoudai kila siku unaanza na sisi wenyewe kabla ya wadau wengine.
Umoja wa Waratibu wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania
Machi 23, 2026
---
TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU UKIUKWAJI WA HAKI ZA AJIRA, KUTOLIPWA MISHAHARA, BIMA YA AFYA, MICHANGO YA NSSF/ZSSF NA MASUALA YA KODI KWA WARATIBU

MWISHO
Imetolewa na: