Julai 12, 2023, Balozi mstaafu wa Tanzania Nchini Sweden, Dkt. Wilbroad Slaa akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari alitoa kauli inayotuhumu waandishi wa habari kwa kufanya upotoshaji wa matamshi yake kwenye sakata la uwekezaji wa Bandari.
Baada ya kauli hii, wadau mbalimbali walianza kutoa maoni yao ambapo jioni ya siku hiyo ilianza kusambaa barua inayodaiwa kutolewa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) ikionesha masikitiko na kulaani kauli za Dkt. Slaa.
Barua hiyo ilienda mbali zaidi kwa kumtaka Dkt. Slaa kumba radhi kwa matamshi yake.
Baada ya kauli hii, wadau mbalimbali walianza kutoa maoni yao ambapo jioni ya siku hiyo ilianza kusambaa barua inayodaiwa kutolewa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) ikionesha masikitiko na kulaani kauli za Dkt. Slaa.
Barua hiyo ilienda mbali zaidi kwa kumtaka Dkt. Slaa kumba radhi kwa matamshi yake.
- Tunachokijua
- Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) ni Asasi ya Kiraia iliyoanzishwa mwaka 1996 na kusajiliwa rasmi mnano mwaka 1977.
Ni mwamvuli wa pamoja wa klabu za waandishi wa Habari Tanzania ambayo kwa sasa ina jumla ya klabu 28 za wanachama.
Miongoni mwa malengo ya UTPC ni Kujenga uwezo wa waandishi wa habari binafsi, ambao ni wanachama wa klabu za waandishi wa habari kupitia mafunzo, utafiti, ziara za mafunzo na mikutano pamoja na Kukuza na kudumisha kanuni za maadili kwa watendaji wa vyombo vya habari katika kukuza uandishi wa maadili.
Mjadala wa Dkt. Slaa kuhusu waandishi wa habari
Julai 12, 2023, Balozi Mstaafu wa Tanzania Nchini Sweden (2017-2021) na Katibu Mkuu wa zamani wa CHADEMA Dkt. Willibrod Slaa, akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika hoteli ya Mesuma, Makumbusho, Dar es Salaam alitoa kauli inayodaiwa kudhalilisha waandishi wa habari pamoja na taaluma nzima ya habari.
Kauli hiyo inasema;
"Siku mlipoandika hotuba yangu, Dk. Slaa akubali uwekezaji, mlikubali amri za mabwana zenu, nyie wote mlitakiwa kufutwa kuwa waandishi. Sasa endeleeni hivyo, sisi tutawachochea Watanzania tuwaambie kabisa Tanzania hakuna magazeti msipoteze hela zenu kununua magazeti bandia".
JamiiForums iliweka pia sasisho lenye kichwa cha habari "Balozi Dkt. Slaa awakosoa waandishi kwa kuandika habari tofauti na alichokisema" lililofafanua hoja hii ya Dkt. Slaa.
Pamoja na Dkt. Slaa, wazungumzaji wengine waliokuwepo kwenye mkutano huo ni Askofu Emmaus Mwamakula, Wanasheria Peter Madeleka na Boniface Mwabukusi pamoja na mwanaharakati Mdude Ngagali.
Lengo kuu la Mkutano huo ilikuwa ni kujadili kuhusu Uwekezaji wa kampuni ya DP World kwenye Bandari ya Dar es Salaam na kauli hii ya waandishi aliitoa wakati akikemea tabia yao ya kuripoti kinyume na kauli alizosema wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Juni 13, 2023 ambapo vyombo vingi vya habari vilimnukuu kwa kusema ameunga mkono suala hilo.
UTPC wametoa barua hiyo?
Ukurasa rasmi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwenye mtandao wa Twitter ulikanusha taarifa hii Julai 12, 2023, saa 4:25 usiku kwa kuchapisha barua hiyo ikiwa na neno "FAKE"
Taasisi nyingi na watu wengine maarufu hutumia njia hii kukanusha baadhi ya taarifa zisizo sahihi.
Aidha, JamiiForums imebaini kuwa UTPC hawakuchapisha taarifa yoyote kwenye ukurasa wao huo tangu Julai 7, 2023, saa 8:14 mchana, siku ya saba saba.
Hivyo, watu wanapaswa kuipuuza taarifa hii kwa kuwa haijatolewa na UTPC.