UTT Amis kuna shida gani? App yao haifanyi karibia wiki mbili sasa

Dynamics

Senior Member
Joined
Feb 2, 2024
Posts
159
Reaction score
194
Habari wadau,

Sielewi kwamba ni mimi mwenye ninayepitia hii hali au kuna wengine pia wanakumbana na hili.

Ni karibia wiki mbili sasa ninashindwa kuingia kwenye App yao.

Hii inanikwamisha kwa kiasi kikubwa kwani ninashindwa kutoa sehemu ya akiba yangu iweze kunisaidia kwenye masuala kadhaa yanayonikabili.

Wadau hebu tusaidiane hili mnalipatia vipi ufumbuzi?
 
Huwa inatokea hiyo, nadhani solution ni Kwenda ofisi zao, unawaonyesha tatizo halafu wataku register tena
 
Dalili hizo zinatosha kuwa macho muda wowote chochote kinaweza tokea
 
Kuna shida ya app uninstall kisha install na uweke upya password. Wamefuta password zote hivyo fuata hatua ya kubadili kwa ussd kwa kutumia menyu yao
 
Mbona kwangu ipo vizuri kabisa?

weka muda wa maongezi, kama hauna - 500 inatosha. Kupata password, piga *150*82#
 
Wamefanya maboresho kwenye app yao hakikisha ume update app pia alafu fwata maelekezo yanayo kuja kwenye screen wakati wa kulog in. Piga *150*82# kwa namba ile ile ulio jisajili nayo kwenye app hakikisha una salio la kawaida sio bundle. Then update ur password kisha malizia kwa kulog in kwenye app utakuwa ume maliza tatizo.
 
Hawafuati maelekezo wanayopewa wanakuja kutia watu taharuki uku mitandaoni watanzania sjui tupoje kwa kweli.
 
Hawafuati maelekezo wanayopewa wanakuja kutia watu taharuki uku mitandaoni watanzania sjui tupoje kwa kweli.
Upo sahihi Mkuu asilimia 100 kwasababu maelekezo yote yapo hapo kwenye simu kwanini hawasomi wafwatilie? Kz maelezo nilio toa sija yatoa hewani nilifwata maelekezo nilio pata wakati na log in na kila kitu kikaenda vizuri tu sasa wao walishindwa nini?
Tupunguze kulalamika vitu vingine nivya kujisaidia mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…