UTT AMIS naona kwenye account yangu ya UTT hela imeongezeka kidogo

Hongera sana ndugu yangu kwa hatua hiyo nzuri na bora ya kuwekeza UTT,

Bilionea Warren Buffet aliwahi kusema, "If you don't find a way to make money while your sleeping you will work till you die" , akimaanisha kwamba, "Usipotafuta njia ya kukufanya kuingiza fedha huku ukiwa umelalala, itakulazimu na itakubidi ufanye kazi mpaka siku UNAKUFA"

Binafsi nakupongeza sana kwa uamuzi huo bora, pia mimi mwenyewe nimejipanga kufikia mwakani 2023, December kuwekeza kiasi hicho-hicho cha 10Mil UTT.

Anything above everage ni tatizo kubwa kwa watanzania wengi, neno langu ni moja tu kwako, achana na watu wenye mipango na mawazo dhaifu, fuata vision yako na Mungu atakusaidia.

Thanks.
 

Asante kwa hongera kaka. Mm mbona hawa watu siwasikilizi kwa chochote. Vitu ambavyo wamefeli ni pamoja na kutojua malengo ya mm kuwekeza UTT, Hawajui UTT ni nn, Hawana maono ya mbele na kubwa kabisa wengi wanaoponda hawana capital ya angalau hata 3m mtu wa hiv atashauri nn juu ya mtu mwenye capital ya 10m. Lkn wanashindwa hata kushtuka na kukuuliza huyu mtu hii 10m ya kuiwekeza UTT amefanyaje fanyaje mpk kafikisha hicho kiasi na kwann aamue kuwekeza kule? Watu wa hivi wanakushauri nn.?
 
[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Nimewahi kufuatilia uwekezaji wa UTT,nikaelekezwa kwenye benki moja ambayo wanahusika,nikafika kwenye Ile benki,nikaelekezwa kwenye dawati la anaehusika,kumuuliza akawa hajui,ikabidi apige simu makao makuu,UTT, aliyepokea nae akashindwa kuelezea,ikabidi atuambie tusubiri kidogo aulizie,baadaye kidogo akapiga simu,alivyoelezea hata sikumuelewa. Nikaondoka nikiwa nimekata tamaa. Nikaachana na Hilo wazo. Conclusion niliyo ondoka nayo kichwani ni kwamba,kuna watu wapo kwenye nafasi/ vitengo,Ila hawana uelewa na kazi Yao.
 
Kabisa mkuu, Mimi kuna mfanyakazi mmoja wa CRDB rafiki yangu, aliniambia hisa za CRDB hakuna kitu, alinivunja moyo, ila nikaendelea kutafuta knowledge kutoka vyanzo tofautitofauti hadi nikafanikiwa kupata uelewa wa kutosha.

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Hii faida naitamani sana.... maana 6M yangu haizalishi kitu ....bora inipe 50 ya kwenda bagamoyo kila mwisho wa mwezi.... tusio na muda biashara zinatupozea pesa
 
Una akili sana
 
Ukiwa na viapnde 2.5m utakuwa na sh ngapi? Unapenda kubet😎
Na utakuwa umewekeza kiasi gani hadi kupata hiyo return? Utagundua utakuwa umewekeza pesa ndefu sana
 
Kwahiyo mfano hapo alipoweka milioni 100 ambayo nisawa na vipande 11,000+ it means 11,000 mara 1 so anapata elfu 11,000/- kwa kuweka milioni miamoja huu ni undezi wa aina gani?!
 
Kwahiyo mfano hapo alipoweka milioni 100 ambayo nisawa na vipande 11,000+ it means 11,000 mara 1 so anapata elfu 11,000/- kwa kuweka milioni miamoja huu ni undezi wa aina gani?!
Nakwambia huu ni uwekezaji wa kipumbavu kuwahi tokea.
Japo wanapata 12% kwa mfano wako atapata 12mil
Ambayo ni sawa na 1mil kila mwezi kwa mtaji wa Milioni 100

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Nakwambia huu ni uwekezaji wa kipumbavu kuwahi tokea.
Japo wanapata 12% kwa mfano wako atapata 12mil
Ambayo ni sawa na 1mil kila mwezi kwa mtaji wa Milioni 100

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Sasa huyu jamaa anafanya kazi mgodini huko... kila pesa akisema azungushe kwenye kamari zenu si atapoteza.... mtu biashara hajawahi fanya akurupuke kisa anapesa
 
Kwahiyo mfano hapo alipoweka milioni 100 ambayo nisawa na vipande 11,000+ it means 11,000 mara 1 so anapata elfu 11,000/- kwa kuweka milioni miamoja huu ni undezi wa aina gani?!

Hili kama jinga vile. Hujui vitu unajifafanulia mwenyewe hlf unajipatia hitimisho mwenyewe kwa kuponda. Km hujui vitu kaa kimya

Ukiwekeza 100M kwa kila mwezi utakua unapata gawio la zaidi ya laki 8.8 huku pesa yako uliyowekeza inakua kutokana na thamani ya vipande. Kwa haraka haraka ukiwekeza hiyo 100M kwa miezi 6 utakuta 101M plus umeshapata laki 8 na zako kwa hiyo miezi 6. Acheni ubisha wa kijinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…