Huu mfuko unawafaa wale wanaoweka akiba bank kwenye saving acc ambapo unaendana na makato.
Mimi nipo kwenye mfuko wa liquid fund.
Nilikuwa na mpango wa kununua kitu fulan, nikawa nakusanya pesa kidogo kidogo kutimiza lengo langu. Mwanzoni nilikuwa naziweka kwenye Acc ya bank (Saving Acc).
Zikiwa kama 5M ndo nikazihamishia UTT, so zikiwa zinaongezeka kati ya shs 30,000-40,000 kila mwezi.
Kama kawaida kila nikipata kiasi fulan naongezea ili nifikishe 15M nitimize lengo langu.
Kwangu niliona ni bora nipate kidogo kuliko hiyo pesa ninayondunduliza ikae bank tu bila kuzaliana . Kila mwezi UTT unapata kama 1% ya pesa yako.
Uzuri wa liquid fund unaweza kutoa pesa yako muda wowote kati siku 3-5 za kazi.
Niliendelea kundunduliza hadi pesa ya malengo yangu ikafika nokaichomoa nikafanya yangu.
Kwa mtazamo wangu huu mfuko unatakiwa uweke ile fedha ambayo huna matumizi nayo kwa wakati huo.
Mfano ada za watoto za shule, akiba ya dharura n.k uzuri fedha yako una uhakika wa kuipata kwa haraka wakati unaitaka.
Nawasilisha