DodomaTZ
Senior Member
- May 20, 2022
- 197
- 233
UTT AMIS imeunga mkono juhudi za Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika kuadhimisha miaka 27 tangu kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kupitia Kongamano la Kumbukizi lililofanyika Mazimbu, Morogoro.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano kwa umma wa UTT AMIS, Martha Mashiku kongamano hilo ni sehemu ya juhudi za kuenzi na kurithisha kwa vizazi vya sasa na vijavyo misingi na falsafa zilizoasisiwa na Mwalimu Nyerere, ikiwemo falsafa ya kujitegemea.
Mashiku anasema katika kuendeleza misingi hiyo, UTT AMIS inachangia kuwawezesha Watanzania kujenga uwezo wa kifedha kupitia uwekezaji, ili waweze kufikia malengo yao ya kiuchumi na kuimarisha uhuru wao wa kifedha.
Anafafanua kwamba UTT AMIS (Unit Trust of Tanzania Asset Management and Investor Services PLC) ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 2005 kupitia mfumo wa awali wa Unit Trust of Tanzania (UTT) chini ya Wizara ya Fedha ya Tanzania lakini imeungana na watanzania wote kuadhimisha miaka 27 ya taasisi hiyo.
Anaeleza kwamba ingawa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hakuanzisha moja kwa moja UTT AMIS (kwa kuwa alifariki dunia Oktoba 14, 1999 na UTT ilianzishwa mwaka 2005), taasisi hiyo inajengwa na kuendeleza misingi mikuu aliyoasisi.
Mashiku anaiweka bayana misingi iliyoachwa na Mwalimu Nyerere ni pamoja na falsafa ya Kujitegemea ambayo alisisitiza kuwa maendeleo ya mtanzania yanatakiwa kutoka ndani ya nguvu na rasilimali zake wenyewe, jambo ambalo UTT AMIS inalitekeleza kwa kuwawezesha Watanzania wa hali zote kuweka akiba na kuwekeza kwa pamoja ili kujinasua kiuchumi.
Kushiriki katika Umiliki wa Uchumi, kupitia mifuko ya uwekezaji ya pamoja (Collective Investment Schemes kama vile Mfuko wa Umoja, Watoto Fund, Jikimu, Liquid Fund, na Bond Fund), wananchi wa kawaida wanapata fursa ya kumiliki hisa na hatifungani za makampuni makubwa ya taifa, jambo linalolingana na maono ya kugawa au kusambaza utajiri na rasilimali kwa umma badala ya kuachwa mikononi mwa wachache.
Ukombozi wa kifedha, UTT AMIS inaendelea kuuenzi urithi wake kwa kukuza utamaduni wa kuweka akiba na uwekezaji ili Watanzania wajenge uhuru wa kweli wa kifedha, unaotokana na falsafa ya uzalendo na usawa wa kiuchumi.
Ikiwa imepita miaka 27 tangu kifo cha Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere bado viongozi wa Tanzania wanaendelea kuyaishi mawazo, falsafa na busara zake kuiongoza nchi.
Miongoni mwa maono hayo ni nchi kutumia teknolojia kukuza uchumi na kuzalisha bidhaa zake kwa kutumia viwanda vya ndani ili kujiimarisha na kujitosheleza kwa bidhaa za ndani badala ya kutegemea za nje.
Katika kupambana na maadui wakubwa watatu; ujinga, umaskini na maradhi baada ya Azimio la Arusha mwaka 1967, Nyerere alianzisha viwanda ili kutumia teknolojia kuongeza thamani ya mazao ya ndani vikiwemo viwanda vya nguo vya Urafiki, Sungura na Mwanza Textile (Mwatex).
Katika uhai wake, Mwalimu Nyerere alikuwa na sifa ya utu, mpenda maendeleo, hakupenda kuona watu wakinyanyaswa, wakionewa au kupuuzwa kwa sababu za unyonge wao.
Mwalimu Nyerere alichukia rushwa, ufisadi, wizi na aina zote, kujenga misingi imara ya kulifanya Taifa lijitegemea, kutumia rasilimali zilizopo ili kujiletea maendeleo ya kweli.
Pia Mwalimu Nyerere alipenda kuona taasisi zilizoanzishwa na serikali zikiwakomboa Watanzania katika nyanja mbalimbali ili waweze kukuza mitaji, kipato chao na kulipa kodi stahiki. Miongoni mwa taasisi iliyobeba maono ya Mwalimu Nyerere na kuyafanyia kazi kwa vitendo ni UTT AMIS.
Taasisi hiyo ipo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango iliyopewa dhamana ya usimamizi wa mali kupitia Mifuko ya Uwekezaji wa pamoja.
Utajiri siyo fedha ambazo mtu anakusanya bali ni fedha zinazowekwa na kufanya kazi. Tamaduni zetu zimeifanya jamii kubwa kuhifadhi fedha ndani katika vyungu, magodoro, vibubu.
Uwekaji akiba na uwekezaji ni dhana mbili tofauti. Uwekaji akiba ni mzuri lakini bila kuziwekeza ni bure.
Ili uwe muwekaji akiba mzuri, unapaswa kuwa na nidhamu ya kujizoesha muda mrefu.
Awali UTT AMIS ilipewa dhamana ya usimamizi wa mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Wekeza Maisha, Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi. Hivi sasa taasisi hiyo imeongeza mfuko mwingine wa Hati Fungani.
Nchini Tanzania unaweza kuwekeza fedha zako katika masoko ya fedha, mitaji. Hatua hiyo inahusisha akaunti za muda maalum na zisizo za muda maalum katika benki za biashara.
Pia hati fungani za Serikali za muda mfupi, mrefu, kampuni na hisa zilizoorodhosgwa katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) ambazo zina nafasi kubwa ya kurejesha gawio zuri.
Uwekezaji unaofanywa na taasisi hiyo kupitia mifuko ambayo wanaisimamia ni fursa mbadala inayowezasha watu, vikundi, taasisi, kampuni kuwekeza pesa zao kwa Meneja wa UTT.
Meneja huzichukua fedha hizo, kuziwekeza kwenye masoko ya fedha, mitaji kulingana na waraka wa makubaliano.
Faida inayopatikana hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa uwekezaji uliofanyika kwenye mfuko husika.
Mfuko wa Umoja, ulioanzishwa Mei 16, 2005 ukilenga kutimiza mahitaji tofauti ya wawekezaji. Awali bei ya kipande ilikuwa sh. 70, kwa sasa sh. 590.2060.
Sifa zilizopo katika mfuko huo ni vipande kuuzwa kwa thamani halisi (hakuna gharama za kujiunga). kiwango cha chini cha kujiunga ni vipande 10 tu.
Malipo ya mauzo hutozwa asilimia moja ya thamani halisi, pia ni rahisi kujiunga, kutoka ambapo manunuzi na mauzo hufanyika kila siku ya kazi.
Mfuko wa Watoto una lengo la kuwasaidia watoto katika maendeleo yao nchini. Awali bei ya kipande ilikuwa sh. 100, mfuko ulianzishwa Oktoba 1, 2008.
Sifa za mfuko huo ni uwekezaji kwa ajili ya mtoto mwenye umri chini ya miaka 18. Kiwango cha chini cha uwekezaji sh. 10,000, unaruhusiwa kuwekeza kidogo kidogo kwa sh. 5,000.
Sifa nyingine ni vipande kuuzwa kwa thamani halisi (hakuna gharama za kujiunga), mfuko hutoa mipango ya aina mbili, kwanza malipo ya ada, pili mpango wa kukuza mtaji.
Malipo ya ada na mauzo ya vipande yanaruhusiwa pale mtoto anapofikisha miaka 12. Mfuko huo ni miongoni mwa mifuko inayotatua changamoto za kielimu hasa katika ulipaji ada kwa wanafunzi, kutoa mtaji baada ya ukomo wa shule kufikia.
Pia mfuko una mipango miwili mikubwa, mpango wa ada za shule na mtaji kwa mwanao. Ili mzazi aweze kuchangia kupitia mfuko huo, anapaswa kuweka sh. 10,000 kima cha chini na hakuna ukomo kwenye kiwango cha juu.
Mfuko ulianzishwa mwaka 2008. Kiwango cha chini cha kipande kilianzia sh. 100, hivi sasa sh. 346.3151.
Mfuko wa Jikimu una lengo la kukidhi mahitaji ya wawekezaji wanaohitaji uhakika wa mapato ya mara kwa mara, ulianzishwa Novemba 3, 2008 ukiwa na sifa za mipango ya uwekezaji, kiwango cha uwekezaji, mpango wa gawio robo mwaka.
Kiwango cha chini cha uwekezaji sh. milioni 2, mpango wa gawio wa mwaka (kiwango cha chini cha uwekezaji sh. milioni moja), tatu mpango wa mwaka wa kukua (sh. 5,000).Vipande vinauzwa kwa thamani halisi (hakuna gharama za kujiunga).
Mfuko wa Ukwasi unaotoa nafasi ya uwekezaji mbadala kwa wawekezaji wakubwa au taasisi ambao wangependa kuwekeza fedha zao za ziada kwa kipindi kifupi ama cha kati huku wakikuza mtaji wao.
Ulianzishwa Aprili 30, 2013, bei ya kipande ikiwa sh. 100.00, hivi sasa imepanda sh. 126.3239.
Sifa za mfuko huo ni rahisi mwekezaji kupata fedha zake za mauzo ya vipande ndani ya siku tatu za kazi baada ya maombi ya kuuza vipande kupokelewa Makao Makuu ya UTT AMIS.
Mfuko huo hauna ada ya kujitoa wala kujiunga, una unafuu wa gharama za uwekezaji, unafaa kwa wawekezaji mmoja mmoja au taasisi, kiwago cha chini cha kuwekeza sh. 5,000,000.00.
Kuongeza uwekezaji wako sh. 1,000,000.00, pia unaruhusu uhamishaji vipande kutoka kwa mwekezaji mmoja kwenda mwingine, kuruhuusu uhamishaji vipande kwenda kwenye mifuko mingine, kuviuza kwa thamani halisi.
Mfuko wa Wekeza Maisha unamwezesha mwekezaji kupata faida pacha (mapato mazuri pamoja na mafao ya bima).
Mfuko huo ulianzishwa Mei 16, 2007, wawekezaji kati ya miaka 18 na 55 ndio wanaoruhusiwa kujiunga. Unatoa mipango ya aina mbili, kuchangia uwekezaji awamu ya kwanza, mkupuo mmoja.
Vipande vinauzwa kwa thamani halisi, hakuna gharama za kujiunga. Kujiunga ni sh. 8,340.00 tu kwa mwezi. Bei ya kipande kwa sasa sh. 416.4499.