Utumiaji wa Kahawa

Utumiaji wa Kahawa

Mosiwakaya

Senior Member
Joined
Jul 22, 2014
Posts
185
Reaction score
35
Salaam wana jf Doctor.

Mimi ni mtumiaji (mnywaji) wa kahawa kwa sasa nina takribani miaka saba ya utumiaji wa kahawa.
Naombeni mnijuze kama kuna madhara yoyote ya kiafya naweza kuyapata kutokana na utumiaji wa kahawa.
 
Inategemea na 'tolerance level' yako kwa caffeine. Kwa miaka 7 ungeshadhurika ingekuwa huna uhimili mkubwa wa hiyo kafeini.

Madhara ya hiyo kitu ni pamoja na goitre, mwili kushupaa/nyauka, msongo wa mawazo usioisha, misuli kukakamaa, kushindwa kukazia fikra katika jambo lolote, shinikizo la damu, vidonda vya tumbo, kukosa usingizi hadi kuathiri utendaji mwingine wa mwili/akili, hasira za karibu, kwa mdada anaweza kuwa mkavu sana ukeni hata akitomaswa vp wakati ule, kwa mwanaume anaweza kushindwa kufika kwa muda muafaka (si lazma hii ikawa jambo jema), n.k.

Si kwamba mtu huyohuyo atapata yote. Inategemeana na kiungo gani kitaathirika zaidi na muundo wa kila mtu mwilini.

Kwa kuwaza tu kuwa inaweza kuwa na madhara, huenda imeanza kukudhuru japo akilini. Itumie kwa kiasi tu mkuu.
 
Huzalisha asid nyingi tumboni. Kuwa na gesi na mgurumo tumboni
 
kweli baadhi ya dalili hapo nshaziona kama ya kuchelewa kufika kwenye kilele cha kibo ila sio cku zote na ckubaini kama ni matokeo ya kahawa, ila kwasasa nina miezi kama sita hv toka stop matumizi ya kahawa japo kwa sasa shitua kiaina ubarikiwe mkuu kwa mchango wako Fundisi Muhapa
 
Last edited by a moderator:
Pa1 sana Mosiwakaya

Ila kuna kitu kinaitwa 'withdrawal symptoms'. Ukishazoea jambo usiache ghafla. Endelea tu kushtua kwa raha zako.

Mi kupunguza uraibu wa kahawa, ninatumia robo kijiko cha chai au pungufu (instant coffee) kwenye maji km robo kikombe kidogo cha chai.

That way napata fleva niipendayo (uchungu) na kafeini kidogo. Mwili umerudi kwenye fomu hadi raha. Na sinywi kahawa usiku kamwe.
 
Kuna kipindi nilikuwa natumia kopo la Africafe la gm 100 kwa mwezi niliacha ghafla ckuona mabadiliko ikabidi juzi ninue kadogo ka gm 50 ndo nashtua kidogo hv sasa Fundisi Muhapa
 
Hizi instant coffee (africafe, nescafe, tanica, etc) ndo zinasumbua. Tumia ground coffee. Halafu zina aroma safi sana. Instant itumie kwa nadra mkuu.

Ni ghali kiasi ila hutajuta.
 
Last edited by a moderator:
Usiache maana inaongeza uwezo wa kufikiri, kukumbuka na concertration hasa maofcn
 
Inapatikana wapi hiyo ground coffee mkuu Fundisi Muhapa

Kwenye supamaketi yoyote kubwa wanakuwa nazo. Kama utamudu though, chukua kwenye coffee shops ambako unaona wakikaanga na wakiisaga. Inachangamsha sana ukiamka na kikombe asubuhi kuianza siku.

The catch is km ni mtu wa ofsn, inabd pia uwe na vichujio vyake. Navyo vipo kila supamaketi inayouza ilosagwa. Otherwise mkuu km mawe yako kamata coffee maker ya ukwee (kenwood iko poa) utafurahia sana unywaji wako wa kahawa. Nazo zinapatikana supamaketi kubwa.
 
Niliizoea sana kupiga kikombe changu then naingia job akili imechangamka vzr kwelikweli kuiacha mazima itanichukua muda sana ngoja niitafte hiyo mkuu kwenye supermarket.
 
Kuna nini kibaya kwenye CHAI na KAHAWA?:

Kwenye chai na kahawa kuna kitu kinaitwa CAFFEINA/KAFEINA. Kafeina ni nini?:
1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la stimulants drugs. Utashangaa. Habari ndiyo hii, watu wengi wanatumia madawa ya kulevya kila siku pasipo wao kufahamu. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina. Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; cocacola, pepsi, sayona nyeusi, azam cola n.k, kafeina huongezwa pia katika red bull na malta. Kaffeina huongezwa pia katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini. Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya.

2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics). Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni sumu isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa sumu/kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio cha chai/kahawa au soda. Madhara yake ni nini?, moja kama unakunywa kinywaji na muda si mrefu unalazimika kwenda kukitoa inamaanisha kinywaji hicho hakikutumika vema na mwili, pili kumbuka ulikunywa kikombe 1 na umeenda kutoa 2 hivyo umekopwa maji mwilini mwako na ukumbuke kuwa MAJI NI UHAI.

3. Kafeina husababisha KANSA. Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH (potential hydrogen). Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini. Kafeina yenyewe ni asidi, hivyo ikiwa mtu anafanya chai au kahawa ndivyo vinywaji vyake vya kila siku basi mtu huyo lazima atakuja kupatwa na kansa katika siku za usoni kwakuwa seli za kansa huishi katika hali ya uasidi pekee na kafeina ndimo mazingira mazuri ya kuishi asidi.

Jarida moja la afya la Uingereza, ‘The British Medical Journal Lancet’, limeripoti uhusiano mkubwa uliopo baina ya utumiaji wa kahawa na kansa ya kibofu cha mkojo na kupungua kwa uzarishwaji wa mkojo.

4. Kaffeina huchangia upotevu wa madini na vitamin mhimu mwilini. Kafeina ambayo ni kikojoshi, huyalazimisha maji kukimbia nje ya mwili kwa haraka na kuziacha seli bila muda wa kutosha kuyatumia maji hayo, maji yanapokimbia kwa haraka nje ya mwili huyakimbiza pia madini mhimu nje ya miili yetu.

5. Kaffeina husababisha kisukari. Mwili una vyanzo 3 vya nguvu ambavyo ni Sukari, Mafuta, na Maji/Chumvi. Tumesema kaffeina ni kikojoshi, hivyo kaffeina hupelekea upotevu usio wa lazima wa maji mwilini, mwili unapokosa maji kama chanzo chake cha nguvu, moja kwa moja huhamia kuitegemea sukari kama chanzo chake cha nguvu na mwishowe kisukari lazima kitokee.

6. Uchovu sugu. Mateja wa chai ya rangi na kahawa mara nyingi wanapojisikia uchovu hukimbilia kikombe cha kahawa au chai. Kaffeina iliyomo katika chai au kahawa huenda kuiamsha na kuitumia nguvu iliyokuwa imehifadhiwa na mwili kwa ajili ya matendo ya dharura na kukuacha wewe ukiwa huna nguvu ya ziada kwa ajili ya kazi za dharura, matokeo yake ni mwili unakuwa upo katika hali ya msukosuko muda wote.

Utolewaji wa sukari iliyokuwa imehifadhiwa, kunapelekea mfadhaiko mkubwa kwenye mfumo wa dharura wa mwili. Unaposhitushwa kidogo tu, unakuwa na nguvu za haraka (Unahamaki) kushughurika na tatizo. Hali hii hatimaye inawezapelekea kukauka kwa tezi ya adreno kutakakosababisha damu chache yenye sukari (hypoglycemia), udhaifu, na kuumwa sana iwapo sukari haitachukuliwa mapema kupandisha juu damu sukari.

Kwa sababu ya biashara kuunda vyakula vyetu vyote maalumu na vinywaji vyenye radha mpya, radha nzuri na nguvu ya kutosha kwa kutumia kafeina toka katika mimea na mitishamba kama vile ginseng kuisisimua tezi ya adreno, kunasababisha Ini kutoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa mwilini kwa ajili ya matumizi ya dharura ya mwili.

Hakuna nguvu iliyomo kwenye kafeina au ginseng. Kuna majina mengine mengi ya visisimuwaji hivi kama vile, kokwa za guru, kokwa za cola na mfalme wa yote ni guarana. Mbegu za guarana zina kiasi cha kafeina mara tatu zaidi ya zile za kahawa, na hawatakiwi kuliorodhesha neno kafeina kwenye vifungashio (packages) au kontena.

Ungaunga wa guarana hutumika kutengenezea vidonge vya kupunguza uzito kwa sababu kafeina itazisambaratisha hisia za njaa, lakini hakuna mahala neno kafeina linaonekana kwenye vifungashio vya dawa hizi.

Kuna mimea, kokwa na kemikali nyingi ambazo zitaisisimua tezi ya adreno na kusababisha ini kuitoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa au hata kuitengeneza toka tishu za mwili wenyewe ‘(gluconeogenesis)’.

Imethibitika pia kuwa kafeina imekuwa ikiingilia na kuathiri unakilishaji wa kinasaba (DNA), namna ambavyo seli mpya hutengenezwa. Kafeina inaweza kusababisha upotevu toka mwilini wa vitamini nyingi za kundi B, kundi C, zinki, potasiamu na madini mengine. Kahawa huongeza hali ya uasidi kwenye utumbo mdogo.

Kafeina inaweza kusababisha msukosuko ndani ya mwili.

Kafeina siyo kwamba tu huimaliza nguvu iliyokuwa imehifadhiwa kwenye ubongo, bali pia huzuia mfumo vimeng’enya katika kutengeneza kumbukumbu kwenye ubongo.

Kituo cha sayansi kwa masirahi ya umma (Center for science in public interest) kimewashauri kinamama wajawazito kukaa mbali na kafeina kwa kuwa tafiti zimeonesha kwamba kiasi cha kafeina kilichomo kwenye vikombe 4 vya kahawa kwa siku kinaweza kusababisha matatizo wakati wa kujifungua kama yalivyoonwa katika majaribio kwa wanyama.

‘Madawa na wewe’, kwa mjibu wa Dr. Earl Mindell, mwandishi wa kitabu; ‘Earl Mindell’s New Vitamin Bible’ (zaidi ya nakala milioni 10), anasema katika ukurasa wa 414 wa kitabu hicho kuwa ‘kafeina ni dawa yenye nguvu kubwa, uwezekano ni kuwa, hauifurahii tu kahawa au cola yako ya kila siku, bali umekuwa mtegemezi/teja (addicted) kwavyo’.

Madhara ya chai ya rangi na kahawa mwilini ni mengi sana na tatizo moja litapelekea lingine na orodha inakuwa haiishi.

Namna ya kuepuka kaffeina kwenye kahawa na chai:

Badala ya kutumia majani hayo ya chai meusi, wewe chemsha maji yako ya chai kama kawaida na unaweza kutumia vifuatavyo kukamilisha chai yako; unaweza kutumia tangawizi na kumbuka pia tangawizi ni dawa ya magonjwa zaidi ya 72 kwahiyo unapoinywa chai ya tangawizi siyo tu unaepuka madhara ya kaffeina tu, bali pia unakuwa umekunywa dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini, unaweza pia kuweka mdalasini, unaweza pia kutumia mchaichai, unaweza pia kukamulia ndimu, pia unaweza kutumia mchanganyiko wa viungo vingi vya chai (spiced tea) ambavyo vinapatikana kwa wingi katika soko la kariakoo dsm na Zanzibar.

Kahawa iache mara moja.
 
Back
Top Bottom