EllySkyWilly
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 2,204
- 2,085
Habari za Leo wa ungwana.
Natamani sana taifa langu liwe tajiri.
Kuna msemo unasema kwamba utajiri unapatikana ardhini. Huu msemo ni wa kweli kabisa.
Kwasababu ndani ya ardhi ndio kuna mali, kuna madini, kuna maji, kuna mafuta, kuna gesi, kuna makaa ya mawe kuna misitu, kuna miti, kuna wanyama na kila kitu na ardhi yenye rutuba.
Nawashangaa sana vijana wa kitanzania wanao ng'ang'ana na biashara za mitandao mara yutube mara kubeti. Hizo ni dalili za kukosa maarifa na uvivu wa kufikiri.
Hizo biashara tuwaachieni wazungu. Sisi bado ardhi yetu ni bikira kabisa ina kila kitu. Ni sisi tu kuamua. Wazungu wenzetu ardhi yao ilisha tumika na walishakomba kila kitu.
Sasa nirudi kwenye mada mimi kama kijana napenda sana taifa langu liwe tajiri. Tukitaka tuwe matajiri ni vyema taifa lijikite kutafuta rasilimali zenye thamani kubwa, tutafute madini ya aina mbalimbali yenye thamani, tutafute gesi kila mahali kwenye mito na maziwa yetu yote. Tutafute mafuta kwenye mito na maziwa yetu yote. Tukipata hizo rasilimali tuzitumie kwa ufanisi, kivipi tuziongezee thamani ili tukiuza end product tupate pesa nyingi zaidi ya ile tungeipata kwa kuuza malighafi.
Nije kwenye gesi asilia. Tukiitumia gesi kwa ufanisi tunaweza kuwa matajiri maramoja sana.
1. Gesi asilia tunaweza kuibadirisha kuwa mbolea za kutumia mashambani Pamoja na kemikali mbalimbali. Mbolea na kemikali tukiziuza ndio tutapata pesa nyingi zaidi.
2. Gesi asilia tunaweza kuibadili kuwa petroli ya kwenye magari. Bei ya petroli ni kubwa kuliko ya gesi. Na magari mengi yanatumia petroli kwa hivyo twaweza kupata soko kubwa na la haraka zaidi. Kwanini tusiwe matajiri.
3. Tukitafuta mafuta tukayapata tusiuze mafuta machafu, bali tuyasafishe ili tupate petroli, dizeli, mafuta mazito, vilainishi vya injini, mafuta ya taa, rami, mafuta ya ndege, na gesi ya LPG pamoja na kemikali mbalimbali.
Kutoka kwenye huo msafisho tunaweza kupata kemikali ambazo tunaweza kutengezea matairi ya magari na pikipiki, na matairi makubwa pamoja na mabomba ya plastic na nyloni.
Hivi vitu vyote tukiviuza ndivyo vyenye thamani zaidi kuliko mafuta, machafu.
4. Japo makaa ya mawe yanachafua sana mazingira lakini yanaweza kuwa malighafi moja kubwa ya kutengezea kemikali za aina nyingi mnoo zenye thamani kubwa sana. Kutokana na uwepo wa kampaundi nyingi sana ndani yake.
Hivyo tukifanya hivyo ni wazi ndani ya muda mfupi tutakuwa matajiri.