Utumikishwaji haupaswi kuendelea kuvumiliwa popote duniani

Utumikishwaji haupaswi kuendelea kuvumiliwa popote duniani

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
UTUMIKISHWAJI DUNIANI 1.jpg


Utumikishwaji ni suala zito ambalo linaathiri nchi zilioendelea na zinazoendelea. Katika nchi zilizoendele utumikishwaji hutokea katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kilimo na ujenzi. Ajira za lazima ni tatizo la kawaida katika nchi zinazoendelea, huku wanawake, watoto, na wazee wakinyonywa katika uchumi usio rasmi.

Kwa mujibu wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) utumikishwaji unaweza kuelezwa kama kazi inayofanywa bila hiari na kwa vitishio vya adhabu. Kuna viashiria kadhaa ambavyo vinaweza kutumika kuamua kama kazi fulani ni ya kulazimishwa, na mambo hayo ni kama vile: wafanyakazi kunyimwa uhuru wa kutembea, kunyimwa mishahara au hati za utambulisho, unyanyasaji wa kimwili au kingono, vitisho, utumwa wa madeni n.k.

Wanawake na wasichana ndio walio hatarini zaidi, lakini pia na wahamiaji ambao wamenaswa katika utumwa wa madeni na kulazimishwa kufanya kazi za shambani ambapo malipo ni kidogo au bila malipo kabisa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Makadirio ya Utumwa wa Kisasa Duniani mwaka 2022, kuna watu milioni 27.6 walio katika kazi za kutumikishwa. Idadi hii kamili inatafsiriwa kuwa ni kama watu 3.5 kwa kila watu elfu moja duniani wanatumikishwa. Idadi ya makadirio ni kuwa wanawake na wasichana wanaotumikishwa duniani ni milioni 11.8. Zaidi ya milioni 3.3 ya wote walio katika kazi za kutumikishwa ni watoto.

Ripoti hiyo ambayo inatolewa kwa ushirikiano wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) na taasisi ya Walk Free, pia inaeleza kuwa utumikishwaji umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni. Ulinganisho rahisi na makadirio ya kimataifa ya 2016 yanaonesha ongezeko la milioni 2.7 katika idadi ya watu wanaotumikishwa kati ya 2016 na 2021, ikiwa ni ongezeko kutoka watu 3 hadi 4 kwa kila watu elfu moja duniani.

Takribani watu milioni 6.3 duniani wako katika hali ya kutumikishwa kwenye biashara ya ngono, ambapo jinsia inaelezwa kuwa ni sababu kuu. Karibu watu wanne kati ya watano walionaswa katika hali hii ni wasichana au wanawake.

HALI YA UTUMIKISHWAJI DUNIANI.jpg

Ikiwa suala hili limeendelea kukua siku baada ya siku, wadau wanaopinga utumikishwaji duniani wamekuwa wakipendekeza namna kadhaa za kupambana na janga hili. Miongoni mwa mambo yanayopendekezwa ni pamoja na nchi kuhakikisha kuwa kabla bidhaa hazijaingizwa kwenye mipaka yake kwa ajili ya usambazaji, makampuni yanapaswa kuthibitisha kuwa bidhaa hizo hazitengenezwi katika mazingira ya utumikishaji au unyonyaji.

Lakini pia, uboreshaji wa itifaki za uhamiaji (hususan mchakato wa mahojiano) ambapo wale wanaosafirishwa kwa magendo wanaweza kutambuliwa kama waathiriwa na kupata huduma stahiki.

Utumikishaji ni aina mbaya sana ya unyonyaji, na haifai kuvumiliwa. Yeyote anayeshiriki moja kwa moja au kuwezesha utumikishaji awajibishwe, na serikali inapaswa kuhakikisha kwamba kazi za utumikishaji hazifanyiki popote nchini.
 
Mimi mwenyewe natumikishwa mkuu. Kufanya kazi kuanzia saa moja hadi saa 12 siku sita kwa wiki na kuamka saa kumi na mbili daily.

Sipendi kabisa adhabu yake, nisipotii nafukuzwa. Ukiangalia kwa umakini hakuna mtu hatumikishwi na utumwa upo tangu enzi za Musa na hautaisha kamwe na hali inazidi kuwa mbaya hasa huku vijijini.
 
Back
Top Bottom