Artificial intelligence
JF-Expert Member
- Jan 28, 2021
- 1,265
- 2,252
Kichwa cha mada chahusika hapo juu. Usaili wa mahojiano wa nafasi tajwa hapo uliofanyika leo tarehe 08/09/2022 umegubikwa na vitendo vya udanganyifu. Maswali yote sita ya nafasi tajwa juu hapo yamevujishwa na baadhi ya maofisa wa sekretarieti ya utumishi wa umma kwa kushirikiana na viongozi kadhaa wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali yaani GCLA.
Maswali hayo yamevuja kupitia kwa msailiwa aitwaye Mercy ambaye alikuwa na maswali hayo huku akitaja baadhi ya maswali hayo na majibu yake kabla ya sahili zote mbili, TCRA Inaweza kuchunguza mawasiliano ya mtahiniwa huyo ya hivi karibuni ili kuthibitisha hili.
Ikumbukwe vitendo vya uvujishaji mitihani kwa wasailiwa kabla ya usaili havirusiwi chini ya sheria ya Utumishi ya sekretarieti ya ajira, na yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo anastahili kuadhibiwa kisheria.
Vitendo hivyo uchangia pakubwa kuajiri incompetent personnel's katika taasisi mbali mbali na uminya haki na usawa kwa wasailiwa wote wa kada husika.
Hivyo basi napendekeza Serikali kufuatilia usaili wa mahojiano wa GCLA uliofanyika leo tarehe 08/09/2022 kupitia utumishi na endapo itajiridhisha na uwepo wa vitendo hivyo vya udanganyifu, ifute usaili huo na nafasi hizo zitangazwe upya na mchakato urudiwe chini ya usimamizi na uangalizi wa Serikali.
GCLA ni taasisi nyeti ya Serikali, hivyo inatakiwa kuajiri kwa kufuata misingi ya haki na usawa.
nape nauye