DOKEZO UTUMISHI, Kuvuja kwa mitihani ya oral interviews Chemist II(Forensic science & toxicology Posts), Mwajiri Maabara ya Mkemia Mkuu (GCLA)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kichwa cha mada chahusika hapo juu. Usaili wa mahojiano wa nafasi tajwa hapo uliofanyika leo tarehe 08/09/2022 umegubikwa na vitendo vya udanganyifu. Maswali yote sita ya nafasi tajwa juu hapo yamevujishwa na baadhi ya maofisa wa sekretarieti ya utumishi wa umma kwa kushirikiana na viongozi kadhaa wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali yaani GCLA.

Maswali hayo yamevuja kupitia kwa msailiwa aitwaye Mercy ambaye alikuwa na maswali hayo huku akitaja baadhi ya maswali hayo na majibu yake kabla ya sahili zote mbili, TCRA Inaweza kuchunguza mawasiliano ya mtahiniwa huyo ya hivi karibuni ili kuthibitisha hili.

Ikumbukwe vitendo vya uvujishaji mitihani kwa wasailiwa kabla ya usaili havirusiwi chini ya sheria ya Utumishi ya sekretarieti ya ajira, na yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo anastahili kuadhibiwa kisheria.

Vitendo hivyo uchangia pakubwa kuajiri incompetent personnel's katika taasisi mbali mbali na uminya haki na usawa kwa wasailiwa wote wa kada husika.

Hivyo basi napendekeza Serikali kufuatilia usaili wa mahojiano wa GCLA uliofanyika leo tarehe 08/09/2022 kupitia utumishi na endapo itajiridhisha na uwepo wa vitendo hivyo vya udanganyifu, ifute usaili huo na nafasi hizo zitangazwe upya na mchakato urudiwe chini ya usimamizi na uangalizi wa Serikali.

GCLA ni taasisi nyeti ya Serikali, hivyo inatakiwa kuajiri kwa kufuata misingi ya haki na usawa.
nape nauye
Hili jambo halikubaliki, Serikali ifutilie haraka sana haiwezekani tuangaike kuwapa elimu watoto wetu, alafu watu wachache watuharibie. Mambo kama haya hayakubaliki kamwe, viongozi waandamizi na wenye mamlaka mpo humu, fuatilieni hili jambo watu wote wapate haki sawa. Hamna haja ya kubebwa kama mtu alisoma na kuhitimu kwa uwezo wake.
 
Mercy mpuuzi sana ukishapewa NONDO kausha
Hizi kazi sio wote mtapata akikosa uliempa NONDO lazima aku snitch

Hii dunia kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake
 
Kichwa cha mada chahusika hapo juu. Usaili wa mahojiano wa nafasi tajwa hapo uliofanyika leo tarehe 08/09/2022 umegubikwa na vitendo vya udanganyifu. Maswali yote sita ya nafasi tajwa juu hapo yamevujishwa na baadhi ya maofisa wa sekretarieti ya utumishi wa umma kwa kushirikiana na viongozi kadhaa wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali yaani GCLA.

Maswali hayo yamevuja kupitia kwa msailiwa aitwaye Mercy ambaye alikuwa na maswali hayo huku akitaja baadhi ya maswali hayo na majibu yake kabla ya sahili zote mbili, TCRA Inaweza kuchunguza mawasiliano ya mtahiniwa huyo ya hivi karibuni ili kuthibitisha hili.

Ikumbukwe vitendo vya uvujishaji mitihani kwa wasailiwa kabla ya usaili havirusiwi chini ya sheria ya Utumishi ya sekretarieti ya ajira, na yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo anastahili kuadhibiwa kisheria.

Vitendo hivyo uchangia pakubwa kuajiri incompetent personnel's katika taasisi mbali mbali na uminya haki na usawa kwa wasailiwa wote wa kada husika.

Hivyo basi napendekeza Serikali kufuatilia usaili wa mahojiano wa GCLA uliofanyika leo tarehe 08/09/2022 kupitia utumishi na endapo itajiridhisha na uwepo wa vitendo hivyo vya udanganyifu, ifute usaili huo na nafasi hizo zitangazwe upya na mchakato urudiwe chini ya usimamizi na uangalizi wa Serikali.

GCLA ni taasisi nyeti ya Serikali, hivyo inatakiwa kuajiri kwa kufuata misingi ya haki na usawa.
nape nauye
Mkuu naona unmsagia kunguni Mercy
 
Mitihani inavuja kwasababu watoto wa vigogo wanapewa maswali na majibu yake hapo ndo shida inaanzia hapo.
 
mimi nilifanya mwaka juzi yani tunaingia kwenye paper robo tatu ya tuofanya nao wanamihitani,niliumia kinyama na walikamata baadhi ya watu wakiwa na mitihani ila hamna hatua yoyote iliyochukuliwa zaidi walichukua ufaulu wa juu zaidi
 
Back
Top Bottom