Utumishi na malimbikizo ya mishahara

aamohamed

New Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
2
Reaction score
0
kwa uchache nawajua wenzangu wanne ambao wako katika hali kama yangu. ila haya ni maelezo yangu binafsi.

katika kipindi kilichokuwa kinarushwa na ITV na TBC taifa leo mida ya saa 12 jioni kuna mkurugenzi mmoja wa wizara hiyo kitengo cha (....sikumbuki ila kinahusiana na mambo ya kumbukumbu za watumishi kwa njia ya mtandao) anadai eti mtumishi wa umma akipandishwa cheo mwezi huu basi mwezi ujao anapata mshahara wake stahili. pia anadai eti kwa wale wanaodai malimbikizo ndani ya muda mchache tu (hakutaja how long) wanalipwa malimbikizo hayo.

mimi sielewi ni kwa nini baadhi ya watu wanapenda kupotosha ukweli. binafsi nilipandishwa cheo about a year after! na mpaka leo malimbikizo yangu sijalipwa. au wanazumgumzia watumishi gani wa umma?kwani sekta ya elimu sio watumishi wa umma? maana walimu siku zote tumekuwa nyuma katika kupata haki zetu...

kwa maoni yangu kama hujaweza kutekeleza kitu, ni heri ukae kimya. na kama umeamua kusema, basi sema kweli...
 
Tuliwaambia kuchagua magamba ni janga....Pole sana ndugu yangu endelea kusubiri na kuvumilia utalipwa siku uchumi ukiimarika.
 

Ni kweli mdau hata mimi yule mama alinikera kwani ule ni uongo mchafu tena hana aibu hata chembe watu wanadai malimbikizo hadi miaka 3 au ana maana mtumishi hulipwa kabla ya kufa labda muda mfupi kwa akili yake ni miaka kumi
 

poleni sana ndg.zangu chini ya wizara ya elimu, nilipaka kushuhudia N/W wa elimu Mulugo akihojiwa na wakufunz wa Korogwe T.C madai kama hayo lkn hakuweza kujibu khs kinachofanyika utumishi juu ya malimbikizo hayo,zaidi akaonyesha udhaifu kwa kusema eti MoEVT wakishapeleka madai utumishi ndio safari yao inaishia hapo,yaani hawawezi kufuatilia huko utumishi,sawa sawa na kusema utumishi watakulipa watakavyo jisikia hakuna wa kuwakumbusha. Pia akadai kuwa kama madai yenu ni ya ndan ya miaka 2 ya karibuni wala hawaangaiki na madai yako kwa sasa eti kikwete kawaambia walipe madeni ya zaman kwanza yakiisha ndio waanze na madai ya kuanzia 2011. Ukweli ni kwamba UTUMISHI wamekalia madeni ya watumishi wengi sana na wanadai kuwa hulipa pale tu serikali inapotoa pesa za kuwalipa(means hawana pesa iliyo tayari kwa madeni). Kupitisha madai kupitia utumishi ni tatizo lingine,bora warudisha system ya kupita moja kwa moja Hazina.
 
pole, kwa kutamanishwa malipo lkn haina kulalamika sana kwan hii ndo Tz ujanjaujanja umezidi mpaka umekua wehu mi mwenyewe nadai hela ya nauli za kuripot kituon ni muda mrefu umepita with no success. Kumbuka walimu ndo tunawahesabia kura magamba we need changes 2015
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…