KERO Utumishi na TAMISEMI, huu ni mkakati maalum kuzuia maombi ya uhamisho kwa watumishi wa umma?

KERO Utumishi na TAMISEMI, huu ni mkakati maalum kuzuia maombi ya uhamisho kwa watumishi wa umma?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Walimu ni daraja la mwisho katika utumishi wa umma.
Hiyo ni kulingana na akili zako zilizojaa kamasi. Kwavile wewe sio mwalimu hujui lolote kuhusu walimu kwahiyo tuliza bichwa lako huko. Narudia tena kusema kuwa hujui lolote kuhusu walimu na ndio maana unajidanganya sana ili kujifariji na maisha magumu yanayokupiga huko.
Kwa taarifa yako walimu wanalipwa kama kada zingine nyingi sana za serikali na kwavile weww sio mwalimu huwezi kufahamu hilo. Hayo makasiriko yako nahisi ni kwasababu ya kukosa hela kwahiyo katafute hela ili uache kuishi kwa makasiriko. Wewe kama upo kundi la mwisho, usifikiri kila mtu yupo kama wewe. Watu wenye hela huwa hawana hayo makasriko uliyonayo, kwahiyo katafute hela.
 
Wakuu natumai mu wazima

Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa kidigitali wa uhamisho kwa watumishi wa umma, lengo likiwa kupunguza urasimu na paperwork katika kufanikisha suala la uhamisho kwa watumishi.

Pamoja na lengo hilo zuri mfumo huu tangu uanze umekua ni kero na kizungumkuti cha hali ya juu kwa watumishi wanaoomba uhamisho mbalimbali kupitia mfumo huu.

Watumishi wanaoomba uhamisho wa kubadilishana ili mfumo uweze kukubali maombi yao lazima wote wawe wa kada moja na daraja moja kiutumishi tofauti na hapo mfumo hauwezi kubali maombi yao, kwamfano tabibu daraja la 2 hawezi badilishana kituo cha kazi na tabibu daraja la 1, hili suala ni kikwazo sana kwa watumishi wa idara moja na kada moja kupata nafasi hii ambapo kabla ya mfumo huu hili suala liliwezekana.

Licha ya changamoto nyingi za kimfumo ikiwepo server kuwa down kila mara, kutokupata incoming request, kusema ukweli utumishi muweke wazi kama mfumo umewashinda basi turudi kwenye analogia kuliko haya mateso mnayowapatia watumishi wa umma.
 
Serikali ya samia haipendezi kuona watumishi mnahama kaeni huko huko mtekeleze ilani,mama kizimkazi anaupiga mwingi sana
 
Hiyo ni kulingana na akili zako zilizojaa kamasi. Kwavile wewe sio mwalimu hujui lolote kuhusu walimu kwahiyo tuliza bichwa lako huko. Narudia tena kusema kuwa hujui lolote kuhusu walimu na ndio maana unajidanganya sana ili kujifariji na maisha magumu yanayokupiga huko.
Kwa taarifa yako walimu wanalipwa kama kada zingine nyingi sana za serikali na kwavile weww sio mwalimu huwezi kufahamu hilo. Hayo makasiriko yako nahisi ni kwasababu ya kukosa hela kwahiyo katafute hela ili uache kuishi kwa makasiriko. Wewe kama upo kundi la mwisho, usifikiri kila mtu yupo kama wewe. Watu wenye hela huwa hawana hayo makasriko uliyonayo, kwahiyo katafute hela.

Umuhimu wa walimu unaonekana kipindi cha kusimamia uchaguzi na kwenye sensa,baada ya hapo wanakua kama toilet pepa.
 
Hii mifumo ni miradi ya ulaji wa fedha za Umma tuu. Hailetwi kwaajili ya kutatua changamoto au kuongeza Ufanisi. Walileta mfumo wa Madenimis haukuwa na chochote. Kuna kipindi Utumishi walileta mfumo wa Watumishi Portal 2017 kwa ajili ya Uhamisho, haukufanya chochote
 
Tangu kuanzishwa na kufunguliwa kwa mfumo wa watumishi portal ess.utumishi.go.tz na kuunza kutumika rasmi mnamo tarehe mosi ya mwezi september.

Ukiwa na lengo la kupokea na kushughulikia maombi ya uhamisho kwa watumishi wa umma,ambapo lengo ni kupunguza urasimu na kuondoa paper work na kurahisisha uchakataji wa maombi hayo.

Watumishi wa umma walihamasika na wengi wamejisajiri katika mfumo huu ambao pia unawapa nafasi za kupata taarifa mbalimbali ikiwamo upatikanaji wa salary slips pamoja na kuomba mikopo online ukiachilia mbali maombi ya uhamisho,hakika mfumo huu umekua na msaada.

Hoja yangu ni hii hivyo ningeomba wahusika watupatie majibu.

Mfumo tangu kunzishwa kwake umekua na matatizo lukuki hasa upande wa uhamisho kwa watumishi,kuna wakati mfumo una load muda mrefu bila mafanikio yoyote.

Mfumo kupoteza taarifa za watumishi waliomba maombi ya kubadilishana baina yao (incoming exchange request),hivyo kushindwa kuendelea na maombi kati ya watumishi wanaohitaji uhamisho wa kubadilishana.

Wasimamizi wa watumishi kushindwa kuchakata maombi (request approval)hasa ngazi za halmashauri wakiwa na sababu kwamba wao hawajui kutumia mfumo na hawana mafunzo juu ya utumiaji wa mfumo huo.

Pia ili kupata msaada kupitia changamoto za kimfumo mawasiliano yaliyotolewa na ofisi ya utumishi namba zao hazipatikani ama nyingine kuita siku nzima bila mafanikio,barua pepe nayo hazijibiwi.
View attachment 2795531


View attachment 2795532
Je hii ni mbinu mpya ya ofisi ya utumishi na tamisemi kuzuia maombi ya uhamisho kwa watumishi wanao teseka kupata uhamisho ambao ni haki yao kwa mujibu wa sheria na taratibu za kiutumishi.

Maombi kwa njia ya barua yamepigwa marufuku,maombi kwa njia ya mtandao nayo vikwazo ni vingi,je ni nini hatma ya watumishi hawa.

Mawaziri wa wizara husika sikieni kilio chetu.
Inaumiza mno yaani Mimi ombi langu limefika mkoani naambiwa nikachukue nianze upyaa kwenye mfumo Hali ya kuwa walipokea na kukaa nalo kwa muda wotee huo ,,wanasahau nilitumia gharama za kwenda na kurudi halamashauri,,mkoani acha tu
 
Nadhani tangu mfumo wa ESS uanze kutumika rasmi tar 01/09/2023, hakuna mtu ambaye amefanikiwa kuhama, kama wapo basi ni idadi ndogo sana.

Mtumishi kuhama ni haki yake,na kiukweli mfumo ni mzuri lkn madam wanaoukontroll ni binadamu,ubaya wake ndo unapoanzia hapo,kibaya zaidi zaidi na watumishi walewale wolokuwa wananufaika na kitu kidogo ili mtu ahame.

OMBI:
Wizara zinazohusika na utoaji vibali vya uhamisho,watoe tathmini mapaka sasa watumishi wangapi wamehama kupitia mfumo wa ESS walojinasibu kuwa itakuwa inachukua mda mfupi mtumishi kuhama

Nawasilisha
 
60% ya watumishi wa Umma hawana ufanisi katika kazi zao
Unasababishwa na serikali kutosikiliza matatizo ya wafanyakazi,mtu anaomba aheme hilo eneo kaboreka nalo au haelewani na viongozi hapo,serikali haitaki kuruhusu,ufanisi utatoka wapi?
 
Tangu niweke ombi la kuhamia kwenye mfumo mwezi wa kwanza mpaka sasa bado DHRO hameshindwa kuliidhinisha eti!.
 
Back
Top Bottom