Utumishi siwaelewi kabisa

Mi juzi allihamisi kuna mshikaji wangu kaitwa idara ya maji kutoka kazi data interview kafanya mwaka na nusu ulopita pia tuna kama mwezi kaletwa mtu wa masoko ofisimi in the same way
 
Naomba niulize na huku kwetu kwenye idara ya afya hawa wanaoitwa kwenye ajira za mkataba benjamin mkapa foundation walifanya interview lini?....na wao pia watatuambia walikuwa kwenye data base.....mbaya zaidi wanaajiriwa waliomalizs 2019 mpaka 2020 sisi wa miaka ya nyuma tunaachwa....ILA HAINA SHIDA HAKUNA MAREFU YASIYOKUWA NA NCHA ...😧😧😧
 
Kama uko utumishi, naomba niwatukane kwamba wanafanya mambo ya kishenz! Hawana weledi na sasa tumeona dalili za kuchezea mfumo wa online application. wanaingiza watu wanaowataka na kuzuia wanaostahili kusailiwa.
 
Inaitwa kanzi data (database). Waliowekwa kwenye kanzi data ni vijana wa kitanzania waliofanya usahili wakafanya vizuri ila hawakuitwa kazini kwa sababu ya ufinyu wa nafasi.
 
Aiseee.. utumishi wapo fair sana kanzi data imenipa ajira Mimi na rafiki zangu wengi sana pasipo kumtegemea kabisa bila connection yeyote wengine wametolewa juzi majamaa 4 Tanesco na ofisi ya waziri mkuu, wengine TTCL
Hiyo ni mwaka huu tu na hata ajira yangu ni mwaka huu
Kikubwa ni kujiandaa vizuri na kuperform na kumtanguliza Mwenyezi Mungu mbele.
 
Hongereni sana mliofanikiwa kazi kupitia utumishi. Wengine tulishawahi kuomba utumishi na kuitwa kwenye interview karibia mara nne. Baada ya kuboresha mfumo wao maboresho na maboresho ikawa unaona tangazo na sifa zote unazo lkn kila ukituma inagoma. Imekuwa hivyo na kujaribu takriban mara 40 kwa miaka kadhaa hadi sasa tumeamua kuacha kabisa ku apply na kujichuja wenyewe kuwa kazi utumishi kuaaply basi tena labla kwenye ma NGO
 
huenda account yako ajira portal hujai update mahali fulani. endapo utaona tangazo unalo fit kwa vigezo nitafute then nitakuambia ni nini shida na tutaitatua pamoja hivyo system itakurihusu ku apply.
 
Waliyo kwenye system hua wanaa apply kwanza kabla hazijatangazwa...

Poleni sana...
 
Hiki ulichosema mpendwa sidhani kama ni sahihi, kuna watu nawafahamu hawafahamiani na yeyote utumishi wameajiriwa kwa kanzi data, kanzi data ni sahihi na kuna watu (wa kawaida kabisa wanaajiriwa)
 
Hiki ulichosema mpendwa sidhani kama ni sahihi, kuna watu nawafahamu hawafahamiani na yeyote utumishi wameajiriwa kwa kanzi data, kanzi data ni sahihi na kuna watu (wa kawaida kabisa wanaajiriwa)
Sasa mkuu KINACHONIUZI hawa utumishi Kila placement za ajira unakuta kada Fulani lazima waajiri watu.. Sasa kwann kama nafasi zinakuwepo hawatoi nafasi za kuomba ili na sisi tusiokuwa kwenye data base tuwepo pia...?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…