A
Anonymous
Guest
Nina kero kuhusu mchakato wa ajira kupitia Sekretarieti ya Ajira, nilifanya usaili wa mahojiano kwenye Kada ya Ualimu mwaka 2025 na 2026, nilifaulu, baada ya kufika ofisini kwao na kujiridhisha lakini sisi tuliofaulu hatupangiwi kazi ila kikitoka kibali kipya wanatangaza tuombe upya badala ya kutuajiri tuliofaulu kwanza.
Hii inatufikirisha namna ya mfumo huu ulivyo sababu tunatumia gharama nyingi kwenda kufanya usaili kwa kukopa fedha, hivyo tunaomba Utumishi irekebishe hizo sheria kuweka usawa.
Napendekeza kuwa wale wanaofaulu wawe wanaingia kwenye waiting list kwaajili ya nafasi zijazo, kikitolewa kibali kipya wa waajiri wale waliopo kwenye kanzidata na siyo kutuambia kutuma upya maombi ili kufanya usaili upya.
Pia soma ~ Sekretarieti ya Ajira: Tumeboresha Mfumo wa Ajira Portal, ambao hawakufaulu usaili wanapewa ujumbe