Utumishi ya Kapteni Mkuchika wa awamu ya tano hii imekuwa mbaya na kisiasa zaidi

Kuhusu kupandishwa na mishahara, tatizo ni maafida utumishi, hao ndiyo mchwa na wanastahili kufungwa au kufukuzwa kazi.

Wala huna haja ya kumtetea Jiwe ,Sheria ni zenu/ Majeshi ni yenu/Mahakama ni zenu mnashindwa nini kuwa wajibisha hao wanao kosea !!??
 

Wewe endelea kumsifia huyo mungu wako. Ila kiufupi tu watumishi wa umma tulio wengi kwa sasa tunazingua tu kwenye maeneo yetu ya kazi. Ukweli ni kwamba, hatuna tena morali ya kazi kama ilivyokuwa enzi za JK.

Na umwambie asipokubali kubadilika, basi tutazingua zaidi. Hakuna mgomo mtamu kama ule wa kugomea moyoni. Utamlazimisha punda kwenda mtoni, ila hutaweza kumlazimisha kunywa maji.
 
Tarehe 01/05/2020 mambo yatakuwa mazuri kwa Watumishi wa Umma wote na Wafanyakazi wa Umma wote.

Kwasasa nimelazimika kutofautisha kati ya Watumishi wa umma na Wafanyakazi wa umma.

WATUMISHI WA UMMA:
Ni wale wanaokula Good life Mawizarani hasa serikali Kuu.

WAFANYAKAZI WA UMMA:
Ndiyo kina sisi, Walimu, Health Personnels wanaokimbia wagonjwa wa Corona and Co. Mostly ni wale wa Local Government.
Hawa wanaajiriwa Maskini na Wanastaafu wakiwa Maskini kwasababu si Watumishi bali ni Wafanyakazi wa Umma.

KN
 
Miaka mitano hakuna nyongeza ya mishahara alafu uchumi keshautibua. Gharama za maisha na familia zimeongezeka.

Kisha unamkuta fundi rangi,nguo,selemara,kupaua anamsifia Jiwe kwa kubana watumishi! Kesho yake analalamika kazi hamna au amepata amelipwa kidogo ila njaa tu ndio imemfanya akubali,au kakimbiwa na nesi/daktari wakati anaumwa 'kohona'!

Hawajui kuwa baba mbabaishaji huzaa watoto wabaishaji!
 
Ndugu yangu yupo Wizarani lkn malalamiko ni yale yale tu. Wizara inayokula good time labda ni ile ya Fedha na Mipango tu - najua pia unajua PS wake ni nani?
 
Umetoa mfano mzuri sana ni kweli hapa Idukilo kuna Mfanyakazi anajenga ila ameishia kwenye renta mwaka wa pili sasa huu
 
Sasa wakiwa na jazba zenye msingi wa madai yao ya kisheria, inategemea wakuhudumie wakiwa na furaha kweli?

Wakati huo mtu amefura hasira za Kodi,bills,kofokewa fokewa na "politicians" wajinga wajinga,unatarajia nini?

Maana eti mpaka wenye viti wa serikali za mitaa/vijiji wanakuwa maboss wa manesi,walimu,matabibu,na waajiriwa wengineo! Hahahaaa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu wimbo wa nyongeza ya mshahara nimekuwa nikiusikia kila inapokaribia Mei Mosi, hakuna mwaka ambao sijausikia, hivi kwa mfano ndio serikali ikawa inaongeza mshahara kila mwaka kama watumishi wanavyotaka, si unaweza kuta mtu analipwa milioni mia mbili sasa??

Nashauri tu pale mnapoweza kutafuta chanzo kingine cha mapato na kuacha sasa fedha ziende kuimarisha sekta nyingine pia, sio kupandisha mishahara tu kila mwaka.
 
Du! Kumbe unajua kweli mfumo wa uongozi wa nchi hii. Yaani Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji anayetoka CCM hapa TZ ana nguvu kuliko hata Katibu Mkuu wa Wizara. Usione akina Kitila Mkumbo wanataka ubunge - sio mchezo babake!
 
Kaka inawezakana we unafanyia kazi Benki Kuu au Wizara ya Fedha ndiyo maana unatapika tu hovyohovyo!
 
Kaka inawezakana we unafanyia kazi Benki Kuu au Wizara ya Fedha ndiyo maana unatapika tu hovyohovyo!
Hapana mkuu mimi ni mkulima ambaye kodi yangu ndio hiyo wafanyakazi wanayotaka kujipendelea nayo kila mwaka, ni muda muafaka sasa mkajifunza kutengeneza vyanzo vingine vya mapato na sio kutunyonya sisi wanyonge. Kuna mambo mengine muhimu pia ya kufanya sio mishahara yenu tu. eboo.
 
Mie pia sio mfanyakazi na kilichonishinda ni manyanyaso wanayoyapata. Ninanunua mazao unayolima wewe then nauza ninapata mahela. Ila ukweli hayo mahela hayaji vizuri siku hizi kwa sababu walaji wengi ni wafanyakazi wa Umma ambao ni kweli kwa sasa baadhi wanadhalilika isipokuwa wachache waliowekwa sehemu zenye neema! Kwa maana hiyo wana haki ya kualalamika ili wasikike!
 
Kama akili hawana acha wanyanyaswe tu maana hakuna namna nyingine
 
Mbwakoko wewe [emoji34][emoji34][emoji34][emoji34]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…