SI KWELI Utumishi Yatangaza Mabadiliko Makubwa Ajira Portal: Kiapo (Affidavit) Kufutwa Rasmi?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetoa tangazo rasmi likiwataka waombaji wote wa ajira mpya serikalini kurekebisha taarifa zao kwenye mfumo wa Ajira Portal kufuatia maboresho makubwa yaliyofanyika.

Hatua hii inalenga kuhakikisha waombaji wote wanakidhi vigezo vilivyowekwa wakati wa mchakato wa maombi ya kazi pindi nafasi zinapotangazwa. Katika taarifa iliyotolewa jijini Dodoma na Katibu wa Sekretarieti hiyo, Bw. Juma Selemani Mkomi, imeelezwa kuwa mfumo huo kwa sasa hautambui tena kiapo cha kisheria (affidavit).

Kutokana na mabadiliko hayo, waombaji wanawajibika kuhakikisha kuwa vyeti vyao vya kuzaliwa, vya sekondari, vya taaluma, na kitambulisho cha NIDA vina majina matatu yanayolingana kikamilifu bila tofauti ya herufi hata moja ili kuwezesha mfumo kufanya utambuzi sahihi wa nyaraka zao.

Mchakato huu wa kuhuisha taarifa unapaswa kukamilika kabla au kufikia tarehe 23 Oktoba, 2026, ambayo ndiyo siku ya ukomo wa zoezi hili. Ili kukamilisha Marekebisho hayo, waombaji wanatakiwa kuingia kwenye mfumo wa Ajira Portal na kufuata mwongozo uliowekwa.
Affidavity.jpg
 
Tunachokijua
Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na tangazo linalodaiwa kuwa limetolewa na ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na utawala bora kueleza kuwa mfumo wa ajira (Ajira Portal) haupokei affidavity kwa wale wenye changamoto za majina hivyo wanapaswa kupiga simu kupitia namba zilizowekwa kwenye tangazo hilo kupata msaada.

Ufuatiliaji umebaini kuwa tangazo hilo ni la kubuni na halijatolewa na Menejimenti ya Utumishi wa umma na lina lengo la ulaghai kwa wananchi.

JamiiCheck imebaini kuwa tangazo hilo la kubuni ambalo limekuwa likitolewa kwa nyakati tofauti tofauti huku likiwa linabadilishwa tarehe na ujumbe kusalia kuwa ulele. Tangazo hilo limekuwepo katika vipindi tofauti ikiwemo mwaka 2025.

Tangazo hilo lina baadhi ya dosari ikiwemo za kiunadishi mathalani neno Ajira Portal limeandikwa Ajita Portal, sambamba na hilo tangazo hilo limetumia namba binafsi na si za mamlaka. Hata Hivyo tangazo hilo limekuwa likikanushwa mara kadhaa na mamlaka.
Hivi hakuruhusiwi kuwa na majina mawili tu?
 
Kusumbua tu watu kanakwamba hizo ajira wanawapa hawa Vijana, nchi ya hovyo sana hii
 
Kama majina yametofautiana inabidi mtu afanyeje?

Akafoji NIDA?

Huu nao ni ujinga wa aina yake.
 
Nyinyi watu wameomba hizo kazi mpk wameamua kuwa maafisa usafirishaji huku kitaaa. All in all wasumbufu nyie
 
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetoa tangazo rasmi likiwataka waombaji wote wa ajira mpya serikalini kurekebisha taarifa zao kwenye mfumo wa Ajira Portal kufuatia maboresho makubwa yaliyofanyika.

Hatua hii inalenga kuhakikisha waombaji wote wanakidhi vigezo vilivyowekwa wakati wa mchakato wa maombi ya kazi pindi nafasi zinapotangazwa. Katika taarifa iliyotolewa jijini Dodoma na Katibu wa Sekretarieti hiyo, Bw. Juma Selemani Mkomi, imeelezwa kuwa mfumo huo kwa sasa hautambui tena kiapo cha kisheria (affidavit).

Kutokana na mabadiliko hayo, waombaji wanawajibika kuhakikisha kuwa vyeti vyao vya kuzaliwa, vya sekondari, vya taaluma, na kitambulisho cha NIDA vina majina matatu yanayolingana kikamilifu bila tofauti ya herufi hata moja ili kuwezesha mfumo kufanya utambuzi sahihi wa nyaraka zao.

Mchakato huu wa kuhuisha taarifa unapaswa kukamilika kabla au kufikia tarehe 23 Oktoba, 2026, ambayo ndiyo siku ya ukomo wa zoezi hili. Ili kukamilisha Marekebisho hayo, waombaji wanatakiwa kuingia kwenye mfumo wa Ajira Portal na kufuata mwongozo uliowekwa.
View attachment 3675614
Juma Seleman Mkomi ni Katibu Mkuu OR-Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Katibu wa Sekretarieti ya ajira ni Bw. Hamis Abdallah Mkunga
Kwa mantiki hii nasadiki kuamini kuwa tangazo ni feki
Na kinacholengwa mtu akipiga hizo simu ndio mwanzo wa kutapeliwa
 
Mata

Matapeli hawa watakugonga soon🤣🤣
 
Juma Seleman Mkomi ni Katibu Mkuu OR-Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Katibu wa Sekretarieti ya ajira ni Bw. Hamis Abdallah Mkunga
Kwa mantiki hii nasadiki kuamini kuwa tangazo ni feki
Na kinacholengwa mtu akipiga hizo simu ndio mwanzo wa kutapeliwa
JamiiCheck
 
Tatizo wanalianzisha wao
Majina hawajui kuyaandika halafu watulaumu sisi
Kwanini wasiandike kama yalivyo?
Wanajua haya ila wanataka kurusha mpira kwetu
 
Back
Top Bottom