De Opera
JF-Expert Member
- May 23, 2013
- 780
- 1,664
Wapwa, habari za muda huu?
Kuna neno 'Onyesha' naona linatumika vibaya na mara nyingi limekuwa likitumika mahali ambapo si mahali pake.
Kuna maneno mawili watu tumekuwa tukiyachanganya 'Onesha' na 'Onyesha'.
'Onesha' likisimama kwa maana ya kumfanya mtu atazame kitu au jambo fulani, wakati 'Onyesha' likisimama kwa maana ya kumkataza au kumzuia mtu ama kiumbe chochote kisifanye jambo fulani.
Sasa hapo nimeona kwa watu wengi wakitumia Onyesha badala ya Onesha.
Mfano hata kwenye mabango makubwa unakuta yameandikwa 'MAONYESHO YA SABASABA' , 'MAONYESHO YA NANENANE', na mengine mengi.
Sasa ile ni sehemu ya kuwaonya watu au ni sehemu ya kuwafanya watu waone bidhaa?
Maana mimi ninavyojua 'Maonyesho' ni mahali ambapo mtu anapewa maonyo na 'Maonesho' ni sehemu ambapo mtu anaoneshwa jambo fulani.
Sasa unakuta mtu kakoma kaonyeshwa mzigo sio wenyewe, usiku kaota akaonyeshwa jumba la kifahari.
Ahsanteni wapwa, tunaelimishana tu kidogo!