Utumivu wa maneno kimakosa katika kiswahili

Utumivu wa maneno kimakosa katika kiswahili

Mkuu hapo ni kimakosa, walioandika nao ni watu.

Kwa hiyo mkuu na wewe unaona kabisa ni kweli kwamba 'Onyesha' ni 'Show'?

Hapanaaa!
'Onyesha' ni kumuadhibu mtu kutokana na kosa alilofanya, eitha kwa maneno ama vitendo.

Nisawa na mchezaji anapocheza rafu, anaonywa kwa kadi ya njano au nyekundu.
Sasa mkuu unapingana na linguist wa Kiswahili, maana almost matoleo yote ya dictionary tanzania na kenya yanasema hivyo.
Shida ni kwamba watu wengi huwa tunaandika maneno kama tulivyozoea kusikia yakitamkwa. Kwa mfani, kwasababu kumbe ni kwa sababu, baadae kumbe ni baadaye.
Pitia kamusi zote utagundua ni onyesha, onyesho, maonyesho
 
Onyesha = Onyo
Onesha = Ona

Niliwahi kuwasikia BAKITA wakiweka sawa jambo hili. TUKI najua wataweka sawa kwenye matoleo yao mapya
Kamusi zote za kiswahili sio TUKI tu, wanatumia onyesha mkuu na ndizo tunazitegemea kama reference. Sasa hebu tusubiri mpaka wakifanya hayo marekebisho
 
Kamusi zote za kiswahili sio TUKI tu, wanatumia onyesha mkuu na ndizo tunazitegemea kama reference. Sasa hebu tusubiri mpaka wakifanya hayo marekebisho
Hapo sawa. Maana nilimsikia nani sijui wa BAKITA akikiri kuwa makosa yalifanyika. Na kwa hivi sasa maneno yote yanaweza kutumika kwa maana moja...
 
Hapo sawa. Maana nilimsikia nani sijui wa BAKITA akikiri kuwa makosa yalifanyika. Na kwa hivi sasa maneno yote yanaweza kutumika kwa maana moja...
Inabidi waanze kuwa serious maana ndio wanategemewa kwa Kiswahili fasaha
 
Basi kuna mijamaa inasema neno sahihi ni Urozi, sio ulozi.

Nimechemka kubishana nayo. Acha nibakie na neno "Kuloga"
😂😂 Achana nayo! Siku moja nilienda dukani kuulizia 'Baking Powder' nikaambiwa haipo, nilivotazama vizuri nikaiona. Nikawaambia hiyo hapo, wao wakasema hiyo inaitwa 'Pekeni poda'. 😂😂
 
😂😂 Achana nayo! Siku moja nilienda dukani kuulizia 'Baking Powder' nikaambiwa haipo, nilivotazama vizuri nikaiona. Nikawaambia hiyo hapo, wao wakasema hiyo inaitwa 'Pekeni poda'. 😂😂
Mkuu hebu niambie huwa ni maalum au maalumu maana kwenye Tuki kwenye intro ya dictionary wametumia maalum mara 3 ukija chini sasa kwenye wakatumia maalumu halafu kuna maelezo tena ya maneno mbalimbali wanatumua maalum yani full kunichanganya
 
Wapwa, habari za muda huu?
Kuna neno 'Onyesha' naona linatumika vibaya na mara nyingi limekuwa likitumika mahali ambapo si mahali pake.

Kuna maneno mawili watu tumekuwa tukiyachanganya 'Onesha' na 'Onyesha'.

'Onesha' likisimama kwa maana ya kumfanya mtu atazame kitu au jambo fulani, wakati 'Onyesha' likisimama kwa maana ya kumkataza au kumzuia mtu ama kiumbe chochote kisifanye jambo fulani.

Sasa hapo nimeona kwa watu wengi wakitumia Onyesha badala ya Onesha.

Mfano hata kwenye mabango makubwa unakuta yameandikwa 'MAONYESHO YA SABASABA' , 'MAONYESHO YA NANENANE', na mengine mengi.
Sasa ile ni sehemu ya kuwaonya watu au ni sehemu ya kuwafanya watu waone bidhaa?
Maana mimi ninavyojua 'Maonyesho' ni mahali ambapo mtu anapewa maonyo na 'Maonesho' ni sehemu ambapo mtu anaoneshwa jambo fulani.
Sasa unakuta mtu kakoma kaonyeshwa mzigo sio wenyewe, usiku kaota akaonyeshwa jumba la kifahari.

Ahsanteni wapwa, tunaelimishana tu kidogo!
Shukran kwa elimu
 
Mkuu hebu niambie huwa ni maalum au maalumu maana kwenye Tuki kwenye intro ya dictionary wametumia maalum mara 3 ukija chini sasa kwenye wakatumia maalumu halafu kuna maelezo tena ya maneno mbalimbali wanatumua maalum yani full kunichanganya
Mimi kwa ninavyojua neno 'maalum' linaweza kuwa sawa kwa maana neno maalum ni neno la kiarabu ambalo linaweza kubeba maana tofauti tofauti ikimaanisha kwamba ni kitu kinachojulikana chenye matumizi yaliyotengwa. ila 'Maalumu' ni sauti tu njinsi mtu anaweza tamka neno. Ukiangalia kiswahili kimetohoa maneno mbalimbali kutoka Arabic language pia. Kwa hiyo naweza nikasema 'Maalum' ni sawa.
 
Kama wazungumzaji wanaelewana Wala Haina shida. Lengo kuu la lugh ni mawasiliano kwahiyo kama wanakosea na wanaelewana isikupe shida Sana.
 
Kama wazungumzaji wanaelewana Wala Haina shida. Lengo kuu la lugh ni mawasiliano kwahiyo kama wanakosea na wanaelewana isikupe shida Sana.
Shida ni kwa wanetu. Lugha tunayozungumza/waliyoizoea si ile wanayoikuta kwenye mtihani.
 
Haya wewe kwenye kichwa cha habari yako hakuna neno la Kiswahili la KIMAKOSA
 
[emoji23][emoji23] Achana nayo! Siku moja nilienda dukani kuulizia 'Baking Powder' nikaambiwa haipo, nilivotazama vizuri nikaiona. Nikawaambia hiyo hapo, wao wakasema hiyo inaitwa 'Pekeni poda'. [emoji23][emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] umenikumbusha kuna mdau mmoja alinikomalia eti 'extension cable' inaitwa 'station cable'
 
Haya wewe kwenye kichwa cha habari yako hakuna neno la Kiswahili la KIMAKOSA
Ndugu hiyo ni sentensi moja. Hilo neno lipo hapo kulingana na sentensi yenyewe inasemaje.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] umenikumbusha kuna mdau mmoja alinikomalia eti 'extension cable' inaitwa 'station cable'
Tena unakuta kakulazimisha kweli. Baasi ungemuuliza sehemu ya kukaa abiria ni wapi?😂
 
Kwenye kamusi neno onesha na onyesha yote yamewekwa kuwa yana maana moja, ni sawa na neno senyenge na seng'enge yote yana maana moja, kwa hiyo wewe haupo sahihi kwa sababu waliokabidhiwa jukumu la kutunga kamusi wamesema onesha na onyesha yote yana maana sawa.
 
Haya ndugu yangu, binafsi miaka ile nilikuwa nikiona mwalimu anaandika notes ubaoni na akakosea neno, baasi sikuwa nanakili hivo hivo bali nilikuwa nasahihisha.

Kwenye hii dunia uwe na akili ya kuelewa na kutambua, itakusaidia. Full stop!

Samahani kwa kauli nilotumia hapo mwisho, kwa vile hii haijapoint kwako mkuu. 🙏
 
Back
Top Bottom