Sauda
JF-Expert Member
- Jun 26, 2018
- 860
- 1,106
Na wewe ni wale wale, huna lolote.Kaka mkubwa umeshawahi kutambua umuhimu wa dini ?
Je ushawahi kujiuliza kielimu ni yapi malengo ya dini ?
Kaka unaposema wazungu wanawacheka,huu ni ujinga uliopea kabisa,inaonekana kwako wewe wazungu ndio kipimo cha ustaarabu na kuelimika,hali ya kuwa ukweli wa mambo ni kinyume ?
Na unaposema wazungu wana kucheka una maanisha wazungu gani na wanakucheka kwanini ?
Je unafikiri kila mwafrika ana yafanya hayo unayohisi kwayo wazungu wanawacheka ?
Hapa nakupa malengo ya dini japokuwa swali hili nimekuuliza hapo juu,na ninajua usingeweza kulijibu.
Malengo ya dini :
1. Dini imekuja kuilinda akili ya mtu
Hili ni miongoni mwa malengo ya dini,kuja kwake ni kuilinda akili ya binadamu isifisidike,yaani isiingiwe na uchafu na kuyakemea yote yapelekayo akili kuharibika,kama vile matumizi ya pombe,madawa ya kulevya na mfano wake.
2. Dini imekuja kulinda mali za mtu
Hili pia ni lengo la dini. Kuwepo kwa dini watu watajua kuchunga amana za watu,kuepuka dhuluma,kutafuta machumo ya halali,kuacha kula mali za mayatima na mfano wake.
3. Dini imekuja kulinda vizazi vys watu.
Hapa ndio maana unakuta dini inakemea sana uzinzi na mfano wake.
4. Dini imekuja kulinda na kichunga heshima ya mtu
Hapa dini imekuja kutufunza jinsi ya kuishi na wenzi wako,wapendwa wako na maadui zako na mfano wake.
5. Dini imekuja kututoa kutoka katika hali duni kiutendaji kwenda katika hali ya juu kiutendaji
Dini imekuja kurekebisha zile ada na desturi za kihayawani,ushirikina na ujings mwengine.
Narudi..........
Kwani mtu kutambua kuwa "UKILALA NA MKE WA MTU SI VIZURI" mpaka awe nfuasi wa Dini fulani?
Mtu kukupatia msaada fulani mpaka awe wa dini fulani?
Mbona ni vitu vya kawaida kabisa hivyo jamani, hata haihitajiki dini kuyatambua/kuyatenda.
Pengine nikuulize, "Bila dini, watu wangeona kuua wenzao ni kitendo chema?
Kiranga