jozee jose
Member
- Sep 22, 2022
- 52
- 120
Ni raha sana pale unapoanza kazi kwa mara ya kwanza paaa salary hiyoo inaingia kwenye bank acount na kusoma 350k, 400k mara 570k au 700k na nk.
Mwanzo mwa maisha ya kazi ni raha na utajihisi kuwa una ubia au undugu mzuri na Serikali, pia utadumisha uadilifu mwingi na unyenyekevu kazini.
Sasa basi, kwa kuwa watu wengi hatuna elimu ya pesa(financial literacy) mara nyingi matumizi mabovu huanzia mishahara mitano ya kwanzaaaa bila kujua huko ndio unatengeneza foundation ya maisha yako hasa ya kiuchumi.
Katika kipindi hiki ndipo mtu anataka anunue sofa la 900k, simu ya iphone au sumsung ya 800k hadi 1m, DStv explorer ya 350k, pressure cooker, rice cooker, jiko la gesi lenye plate nne, feni tatu moja chumbani nyingine sebuleni na nyingine spare.
Haitoshi bajeti ya unywaji na kuhonga wanaweke ambayo kwa wiki hadi 50k hadi 100k. Hapo nimetaja 40% tu ya matumizi na mengine sijataja ambayo ni ya umuhimu sana au ya kawaida.
Sasa kwa mfumo wa maisha ya namna hii kwa nini maisha yasiwe magumu? Maana vipato haviendani na matumizi kabisa.
Je mtu kama huyu akisukia taarifa za Mei mosi zinasema kuhusu ongezeko la mshahara atazifurahia? Maana bila shaka atakuwa ameingia katika dimbwi la madeni hivyo akidhani ongezeko la mishahara litafidia madeni yake.
Mdau unasemaje!