Utungaji wa Sheria nchini uzingatie Mtiririko Mzuri na Matumizi ya Lugha Rahisi

Utungaji wa Sheria nchini uzingatie Mtiririko Mzuri na Matumizi ya Lugha Rahisi

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Ili wananchi waweze kuelewa vizuri Sheria mbalimbali nchini pamoja na vifungu vyake, kunatakiwa kuwe na mtiririko mzuri katika uandishi wake pamoja na matumizi ya lugha rahisi.

Wananchi wanapaswa kuwa na uwezo wa kuelewa sheria bila kuhitaji msaada wa kisheria au ufafanuzi wa ziada. Hii itawezesha watu kufuata sheria na kuwa na ufahamu kamili wa haki na wajibu wao.

Mtiririko mzuri na matumizi ya lugha rahisi inasaidia:
~ Watu wote bila kujali viwango wyao elimu kuelewa sheria, haki pamoja na wajibu wao.

~ Kuongeza ushiriki wa raia katika michakato ya kisheria.

~ Kuepusha uwepo wa tafsiri potofu na upotoshaji wa sheria unaoweza kusababisha utata na mizozo katika utekelezaji wa sheria husika.

Kuongeza uwazi na uwajibikaji kwa serikali na vyombo vya sheria.

Mfano, katika Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi 2022, Sura ya 2 inayohusu kuanzishwa kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafasi imefuatiwa na Sura ya 3 inayohusu Usajili wa Wakusanyaji na Wachakata taarifa, wakati maelezo yanayohusu Vyanzo vya Fedha za Tume yameenda kuwa Sura ya 8, jambo linalofanya iwe rahisi kumpoteza msomaji kutokana na mtiririko huo.

Screenshot 2023-07-11 145320.png


Screenshot 2023-07-11 145347.png


Lakini pia kwenye sheria hii imetumia msamiati 'Lakiri' na 'Taasisi Nafsi', maneno ambayo bila kuwa mbobezi wa sheria au mtaalamu wa lugha huwezi kuelewa nini kimemaanishwa, tukianza kubangaiza wenyewe tunaweza kuja na na tafsiri elfu kidogo. Kutumia maneno rahisi badala yake, kunapunguza mkanganyiko katika uelewa wa sheria husika.

lakiri.png


Kutokana na hayo wadau walishauri Sura ya 8 inayohusu Vyanzo vya Fedha za Tume ndio iwe sura ya 3 ili kuleta mtiririko mzuri wenye maana.
 
Back
Top Bottom