Utunzaji na Uhifadhi Endelevu wa Mazingira na Maliasili Tanzania

Utunzaji na Uhifadhi Endelevu wa Mazingira na Maliasili Tanzania

Aisee Mkuu. Kwakweli Nakushkuru sana.
Hakika tunahitaji wanaharakati watakaoweza kusimama mstari wa mbele kutetea mazingira.

Thank you, I'm real inspired.
Pleasure is mine mkuu.
Ndio inabidi kuwa na akili za ki harakati zaidi lakini pia kuwa tayari kwa yatokanayo.
Mimi niko kwenye sekta nina ushuhuda wa jinsi gani suala la hifadhi ya mazingira linapigwa vita hasa na wana siasa kuliko hata wawekezaji Tanzania.

Unapojaribu kufanya intervention kwenye mradi wowote wenye athari za mazingira kabla hujafanya chochote utapokea simu kutoka ngazi usiyoitarajia ikikuamrisha kuachana na suala hilo mara moja!

Bahati mbaya unajikuta una hata wa kuku backup in case wana kwenda beyond ya normal resistance.
Kama kuna really people with conscious na mazingira tuungane tuone tutaokoa kiasi gani.
 
Pleasure is mine mkuu.
Ndio inabidi kuwa na akili za ki harakati zaidi lakini pia kuwa tayari kwa yatokanayo.
Mimi niko kwenye sekta nina ushuhuda wa jinsi gani suala la hifadhi ya mazingira linapigwa vita hasa na wana siasa kuliko hata wawekezaji Tanzania.

Unapojaribu kufanya intervention kwenye mradi wowote wenye athari za mazingira kabla hujafanya chochote utapokea simu kutoka ngazi usiyoitarajia ikikuamrisha kuachana na suala hilo mara moja!

Bahati mbaya unajikuta una hata wa kuku backup in case wana kwenda beyond ya normal resistance.
Kama kuna really people with conscious na mazingira tuungane tuone tutaokoa kiasi gani.

Mkuu Hapo Sasa Umegusa Point muhimu sana. Tuunde Taasisi ya Watetezi wa Mazingira.

Mimi Nikionaga Baadhi ya Wanaharakati wa haki za bidamu, watoto, wanawake n.k.. Huwa nawaza vipi kama tunakuwa na watetezi kama hawa hawa wa mazingira. Watu ambao watatetea mazingira bila woga.
Mimi niko tayari mkuu.

Kwa wengine tuendelee kuonesha interests then baadae tuangalie nini cha kufanya.

Commitment ni Muhimu Sana.
 
Ndugu Conservator nakupongeza kwa kufikiria kumshika mkono yatima mazingira angalau naye apate mtetezi japokuwa sina uhakika kama atapata kweli!

Nianze kwa kusema suala LA mazingira ni mtambuka lakini u mtambuka huu umebakia kwenye maandishi tu si kwa vitendo.

Ukiweka utetezi wa mazingira katika vitendo ni mgumu kutokana na kwamba hifadhi ya mazingira ni kikwazo katika uchumi, ndio maana hata trump kajitoa kwenye Paris accord ili kulinda uchumi wa viwanda.

Lakini si trump tu hata Tanzania tuna rais asiyejari mazingira, kama tulivomsikia hivi karibuni kwa nyakati mbali mbali akisema "mwekezaji atakayeona ardhi inamfaa kujenga kiwanda ajenge tu halafua aone nani atamnyima kibali" hii ina maana kwamba tathimini ya athari za mazingira haitafanywa mahala kiwanda kinapojengwa Ila kibali kitolewe kwa amri ya rais tena kiwanda kikiwa tayari kinafanya kazi.

Lakini pia tumemsikia akisema mradi wa umeme wa rufiji falls lazima uendelee pamoja na kwamba unapingwa na wataalamu wa mazingira, ukiacha hayo kuna hotel nyingi A kitalii zinazojengwa mbugani na kupelekea athari za mazingira na ecology.

Suala kubwa ni mgongano wa maslahi ya kiuchumi na maslahi ya hifadhi ya mazingira.
Pili ni kwakuwa athari za mazingira social impact ni kwa mtu wa hali ya chini zaidi kuliko wa hali ya juu hivyo watunga sera na watoa maamuzi hawaguswi kwa kiasi kikubwa na athari hizi.

Kutokana na hivyo basi, hata kama kila sekta iwe ya Mali asili, iwe kilimo na uvuvi, iwe ni nishati na madini nk, na pia sheria kuu ya mazingira ya mwaka 2004 haziwezi kufanya kazi bila kuwepo utashi wa watunga sera na watoa maamuzi.

Mwisho kabisa, huwa nafikiria kuwa njia rahisi ya kulinda mazingira yetu ni kuwa mwana harakati maana kwa kufanya hivi utalazimisha hoja kuingia masikioni kwa wasiopenda kusikia.
Umechanganua vizuri Mkuu, big up sana kwa hili.

Pia nikupongeze kwa rai uliyoitoa mwishoni "Njia rahisi ya kulinda mazingira yetu ni kuwa mwana harakati maana kwa kufanya hivi utalazimisha hoja kuingia masikioni kwa wasiopenda kusikia".

Naomba nikuulize suala fulani, Je unadhani kuwa mwanaharakati pekee kutotosha kuweka mkazo na hamasa katika utunzaji wa Mama Mazingira?.

Nitolee mfano wa Mwanamama Maathai niliyem-mention hapo juu kwa harakati zake zilizobeba jina la "Green Belt Movement".Huyu Mama alikutana na changamoto nyingi sana zikiwepo za kusumbuana sana na Serikali ya Kenya ya wakati ule (Danie Arap Moi, R.I.P), kutishiwa maisha, udogo wa ufahamu kwa hadhira juu ya utunzaji wa mazingira na mengine mengi ya namna hii.

Je, kwa ufupi wa maelezo hapa juu hudhani kuwa tuanze na hizi changamoto kwanza kuliko kumtafuta mwanaharakati?.
 
Watu hawana uzalendo kwenye uhifadhi kwa sababu hawaoni direct benefits za kutunza mazingira na wanyama pori. Serikali na wadau wengine kwa muda mrefu hawakushirikisha jamii kwenye kupanga matumizi endelevu ya ardhi.
Heshima Mkuu!

Unasema "Watu hawana uzalendo kwenye uhifadhi kwa sababu hawaoni direct benefits za kutunza mazingira na wanyama pori"?.

Ni kweli kuwa hatuoni direct benefits kama unazodhani au muendelezo na Ushamba wetu wa muendelezo wa falsafa ya kila mtu na lwake?.

Nadhani faida ya Mazingira na wanyama pori inafahamika wazi sema tu Ulimbukeni wetu na Ujuaji ndiyo unaotufanya tusitunze mazingira.
 
Wakuu.

Nimejikuta nasoma upya uzi huu as if sio mimi noliendika.

Nafkiri nikazie tena yafuatayo;

JF tuhutaji Jukwaa Mahususi la Mazingira na Maliasili (Environment and Natural Resources Forum)

It seems wengi bado tuna mtizamo wa kusema ulinzi au uhifadhi wa mazingira na maliasiri zetu ni jukumu la serikali au taasisi zisizo za kiserikali au mashirika ya kimataifa.

Naona kama bado hatujafikia hatua ya kuona we are really connected to nature in such a way that we can't survive without it..Yet we treat all environmental services as free public/common goods that no one shall be held responsible based on the portion he or she destroyed..

Bado tunaona kama utetezi (advocacy) wa mazingira na natural resources ni jukumu la wanaharakati zaidi..

Nafikiri Tukiwa na JF Mazingira tutakuwa na direct access ya kujadili maswala kadha wa kadha kama;-
- Utoroshwaji wa madini/mchanga au makinikia katika maeneo mbalimbali
-Ukataji ovyo wa miti katika maeneo muhimu kama maeneo oevu (wetlands), vyanzo vya maji n.k
-Utolewaji wa vibali/ lesseni vya kuvuna misitu kwa upendeleo
-Fursa za wananchi kufaidika na uhifadhi wa pamoja wa misitu na wanyapori kupitia program kama Joint Forest Management (JFM), Community Based Forest Management (CBFM) na Community Based Wildlife Management (kupitia WMAs) n.k
-Kujadili changamoto zinazokumba hifadhi za wanyapori kama Ujangili, Utalii Usiofuata Taratibu, Kugongwa na Magari, ukame n.k
-Migogoro ya wananchi na askri wa hifadhi kama walipo chini ya TAWA/TANAPA au TFS n.k
-Uvamizi wa Hifadhi
-Utalii kwa ujumla
-Uchafuzi wa Bahari na maeneo ya fukwe
-Uvuvi Haramu

Na Mengine mengi..

This thread was meant to lay foundations or to add on existing ones..
 
Kwanza kabisa napenda kuwaelezea kidogo hawa jamaa. Friends of Usambara ni taasisi iliopo katika milima ya Usambara Magharibi. Taasisi hii imeanza kufanya shughuli za utalii tamaduni kwa malengo ya kutunza mazingira na utamaduni mwishoni mwa miaka ya tisini hadi hivi sasa.

Katika kipindi chote hiki tumeweza kuona manufaa makubwa ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya watalii katika milima hii kulikopelekea ukuwaji wa uchumi pamoja na vijana wengi kupata ajira.

Katika miaka ya hivi karibuni hadi leo hii tumeweza kuona walivyojikita katika kutunza mazingira wakiwa na lengo la kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya milima ikiwemo vilele vya milima, mashamba ya raia na pia kwenye misitu ya asili iliongua kutokana na sababu mbalimbali. Mpaka sasa wanasema wameshapanda miche zaidi ya milioni saba.

Kilichonivutia zaidi ni pamoja na ajira walioitoa kwa vijana zaidi ya 400 wanaofanya kazi katika shughuli nzima ya kutunza mazingira.

Nimepata kutembelea moja ya vitalu vyao vilivyoko Lushoto mjini na kujionea.

Hizi ni baadhi ya picha.
IMG_20180816_131249.jpg
IMG_20180816_131254.jpg
IMG_20180816_131237.jpg
IMG_20180816_131243.jpg
IMG_20180816_131258.jpg
IMG_20180816_114837.jpg
 
Nili kuwepo huko juzi kati nlikaa milima ya usambara Pana Hali ya hewa tulivu na miti murwaa
Kuanzia pale lutindi hospital pamezungukwa na mapori na miti mikubwa kuna ukijani sana huko...

Ova
 
Home sweet home. Safi Sana hongera kwa utunzaji mzuri wa safu za milima ya usambara.
 
”Badala yake Halmashauri zimekuwa zikiripoti na kutoa taarifa ya upandaji wa miti kadhaa lakini unapozunguka kwenye Halmashauri kutaka kujua hiyo miti.. haipo!” Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Sio siri huyu mama huwa namu-admire sana. ni mchapa kazi sana na ana busara sana
 

Attachments

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene ameziagiza Mamlaka zote za Serikali Nchini kuanzia Mamlaka za Mikoa mpaka mamlaka za Vijiji kuweka utaratibu wa kutumia ardhi kwa ajili ya kuhifadhi misitu ili kuweza kutunza mazingira.

Ameyasema hayo jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 5 wa Kisayansi juu ya utunzaji endelevu wa Mazingira ambapo alikua Mgeni Rasmi.

Amesema kuwa Elimu izidi kutolewa kwa Wananchi ili kuweza kupata uelewa zaidi juu ya maeneo ya uhifadhi wa misitu ambayo yametengwa..

Aliyataja maeneo hayo kuwa ni Serengeti-Ngorongoro, Ziwa Manyara, East Usambara, Jozani Chwaka-Zanzibar na Gombe-Masito-Ugalla.

Alisema kuwa maeneo hayo yametengwa kuwa maeneo ya hifadhi kwa sababu ya ikolojia na bayonuai iliyopo katika maeneo hayo. Kwa sasa maeneno hayo yanapata changamoto kwa kuvamiwa na shughuli za Binadamu hivyo kusababisha uharibifu katika maeneo hayo ya hifadhi.

Alisema kuwa ni vema kila Mtanzania kujua umuhimu wa mazingira na hivyo kuweza kulinda na kuhifadhi maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya hifadhi, na pale yalipoharibiwa basi parejelezwe kwani kwa kufanya hivyo ni kutunza mazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. George amefungua Mkutano huo wa 5 wa Kisayansi juu ya utunzaji endelevu wa Mazingira ambao umeandaliwa na Baraza la Usimamizi wa hifadhi ya Mazingira (NEMC) na umefanyika katika kumbi za Mikutano za AICC jijini Arusha.
 
Dunia ni sehemu nzuri ya kuishi inakadiliwa imekuwepo kwa takribani miaka 4.543 billioni, dunia ni nyumbani kwetu sisi na viumbe hai.

Kupitia dunia tunayo mazingira yenye utofauti na aina mbalimbali, mazingira haya yamekuwa yenye umuhimu kwetu na viumbe hai wengine.

Licha ya kuwa tunatambua umuhimu wa mazingira yetu, pengine unaweza shangazwa na dondoo hizi;-

|- Kila siku takribani miti 27,000 inakatwa duniani kwa ajili ya kutengeneza karatasi laini za chooni maarufu kama toilet paper

|- Kama tukitumia tena (Recycle) karatasi zinazotumika kuchapa gazeti la New York Times pekee kila siku, tunaweza okoa miti zaidi ya 75,000

|- Kila unapotupa chupa au vifungashio vya plastiki baharini unaua viumbe wa baharini milioni moja kwa mwaka.

|- Chupa ya kioo (Glass bottle) unayotumia inachukua zaidi ya miaka 4,000 kuoza na kupukitika

|- Kwa wastani inakatwa zaidi ya miti 1,000 kwa kila dakika, maana yake kila ndani ya saa moja tunakata miti zaidi ya 60,000. Ukitafuta Google The World Counts, utajionea maajabu ya idadi ya miti inayokatwa. Mpaka tarehe 15 March 2020 saa 12:43 jioni miti 5,729,738.49 ilikuwa imekatwa.

3m.png


Kila mtu anatumia (Consume) vitu kadhaa iwe chakula, vinywaji, kuendesha vyombo vya moto na viburudisho tofauti na kati yetu kunawapenzi wakubwa wa chocolate. Je umewahi fikiria kuhusu madhara ya hivi vitu tunavyotumia hasa katika mazingira yetu?

|- Biashara ya mavazi ni kichocheo cha pili cha uchafuzi wa mazingira tunayoishi baada ya mafuta. Viwanda vya pamba vinatumia dawa za kuulia wadudu (Pesticides) kuliko zao lolote na zaidi ya lita za maji 20,000 zinatumika kutengeneza tisheti moja na 'pair' moja ya suruali ya pamba. Fikiria hapo nyumbani una tisheti na jinzi ngapi zenye 'material' ya pamba.

|- Magari ni chanzo kikuu cha uchafuzi wa hewa hasa katika miji na majiji, kuanzia mwaka 2010 mpaka 2035 'kwa kadri' zaidi ya magari bilioni mbili yatakuwa yamezalishwa (Manufactured). Meli moja ya mizigo inasababisha uchafuzi wa hewa zaidi ya magari milioni 50, hapo hatujataja ndege.

|- Inachukua zaidi ya lita 24,000 za maji kutengeneza kilo moja ya chocolate na lita 21,000 za maji kutengeneza kilo moja ya kahawa. Kila tunachokunywa au kula kina madhara yake kwa kutugusa ama laah! (Directly or Indirectly). Nusu ya chakula kinapotea kila siku duniani kama taka, mpaka kufikia mwaka 2050 dunia itakumbwa na uhaba mkubwa wa chakula kama mifumo ya matumizi ya vyakula isipo boreshwa. Nunua au pika chakula kinachokidhi haja yako, badala ya kukitupa kumbuka watu wanakufa au kulala pasipo kula.

3mbq.png


Unatambua tangu dunia kuumbwa kiasi cha maji ni kilekile ila idadi ya watu ndiyo inazidi kuongezeka. Dunia imeundwa na asilimia 75 ya maji na bahari imechukua kiasi kikubwa.

Kama tusipotunza mazingira sasa kuna hatari ya kiwango cha maji kuzidi kupungua hali itakayopelekea dunia kukumbwa na ukame na kutoweka kwa baadhi ya viumbe.

Kumbuka mpaka sasa tayari dunia imekwisha poteza aina mbalimbali za viumbe hai na mimea, takribani aina 600 ya mimea na 300 ya wanyama, ndege na wadudu. Tuliwapoteza Baiji, Dodo, Great auk, Stellar Sea Cow, Thylacine, Quagga na wengine.

Utupaji taka hovyo umekuwa tamaduni sasa, unaruka vocha unakanyaga diaper huku ukitingwa na chupa/vifungashio vya plastiki. Ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa ni kama mafunzo ya stadi za kazi sasa.

3mbb2.png


| Suluhisho ya haya yote ni nini?

Ni kuwajibika katika kutunza na kuendeleza vyanzo vya maji, kupanda miti, kutumia taka kutengeneza bidhaa na kusitisha bunifu zilizoshindwa kujisimamia katika utunzaji wa mazingira (Plastiki).

Dunia hivi sasa inashuhudia jitihada na kujitoa kwa mashirika, taasisi na kampuni mbalimbali katika kutunza mazingira. Tutaweza kuona Parley for Oceans wakitumia plastiki katika utengenezaji wa mavazi kwa ushrikiano na adidas, BALR, Puma na timu mbalimbali za michezo pia tunaweza kuona Heartfeldt Foundation ikijitoa katika katika kuchangia vifaa wezeshi katika kupambana na uchafuzi wa mazingira.

Ni jukumu letu sote hivi sasa kutumia muda wa mapumziko katika upandaji miti, kusafisha mazingira na kubuni mbinu mpya ya kuondokana na uharamia wa kuiharibu dunia. #KeshoTutachelewa kama tusipochukua hatua madhubuti.

#WakatiNiSasa #IshiKijanja #ExperienceTheChange
 
Back
Top Bottom