Utunzaji wa nywele za asili

Ahsante sana my dear
 
ukuaji wa nywele ni nature na mtu,mi nywele zangu zinarefuka nch4 na nusu kwa mwaka,miaka mi3 nafikia urefu wa ruler nzima,sahv nina miezi 7 tangu nizi roll ziwe dread,hiyo picha nlopiga beach ilikuwa mwaka huu mwezi wa3,hio nyingne mwezi wa 10,hio ya mwezi wa 3 nywele zilikuwa hazijapitiliza kuzidi sikio,hio nyingne imepitiliza bado miezi mi5 nifunge mwaka,ntarudi tena kupost zikifikisha mwaka
 

Attachments

  • 39402056_10214910204422172_7674641447353581568_n.jpg
    47.2 KB · Views: 72
  • 43198609_10215256005746989_6473971945208545280_o.jpg
    64.4 KB · Views: 64
Kwan hata ukijifunga mfuko wa plastiki ukakaa nao lisaa Limoja au zaidi haujaboresha au stima ndio Bora zaidi
 
Kwan hata ukijifunga mfuko wa plastiki ukakaa nao lisaa Limoja au zaidi haujaboresha au stima ndio Bora zaidi
Mm natumia kofia ya plastic. Inakaa vzr tu, ingawa ya madam sijatumia
Huwa natumia ndiz olive oili na asali
Bt zote ni nzuri tu
 
Kama kichwa kinavyosema. Wale wapenda nywele natural kama Mimi hebu tupeane maujanja ya jinsi ya kutunza nywele zetu Kwa kutumia vitu vya asili.

Hapa nazungumzia jinsi ya kutengeneza shampoo Kwa kutumia vitu asili toa na faida yake na imekusaidiaje?

Kutengeneza shampoo ya asili

Mafuta unayotumia

Tupe na ratiba nzima ya nywele yako unavyoishughulikia.

Nakaribisha tujifunze pamoja.
 
Niko hapa, leo ni ijumaa ni siku ya kuzipa chakula cha wiki kesho naosha kisha natengeneza style ntakayokaa nayo wiki nzima hadi ijumaa inayofata.
 
Huwa sina formula ila nilishaacha kutumia shampoo, naosha nywele na sabuni ya kipande haswa jamaa.

Chakula nnachokilisha nywele zangu Kila ijumaa ni tui la nazi bila kulichanganya na maji. Siku nyingine ndizi mbivu na mtindi, siku nyingine parachichi na mtindi na olive oil, siku nyingine juice ya carrot na maji ya mchele, au maji ya mchele uliolowekwa kwa siku 5 au juisi ya kitunguu maji peke yake na siku nyingine nachanganya kitunguu maji na tangawizi nachuja juisi yake.

Vyote hivi sichanganyi na maji na nikipaka usiku nalala nimefunga nywele na kofia ya plastic asubuhi naziosha na kuzipaka hair butter na hair cream (Haya mafuta ya dukani) kisha naweka protective style mwenyewe ya wiki nzima.

Nshasahau kadhia za wasusi zaidi ya mwaka sasa na nywele zangu zinarefuka kila leo.

Pamoja na kurefuka wengi tuu wameshaniambia, Kasie una asili ya kisomali au kimanga wewe, hizi nywele zote ni zako mbona zina waves kama za kisomali wakati wewe ni mmatumbi wa kinyamwezi..... Basi Mie nacheka tuu hehehehee.

Kasie Manywele.
 
Hongera Sana najifunza kutoka kwako. Naamini nywele ya kiafrica hata kama ni kipilipili inakua vizuri kabisa.
 
[emoji7][emoji7][emoji7]
Unazidi kunifanya nijione sikukosea kuchagua Health hair.
 
Samahani tui la Nazi nalipataje bila kuchuja na maji.....nimependa Maelezo yako
 
Team natural,

Nimemix Coconut oil, Olive oil na Jamaican black Castro oil, sina shampoo maalum chochote nitakachoogea ndio naosha nywele pia.

Utanipata kwenye rough dread au TWA hair....
mafuta ya TWA natumia Cantu na rough dread natumia Jamaican Mango and Lime.
 
Hongera kwa kulisha chakula bora nywele zako.
 
Mimi nimejifunza vingi Sana kuhusu natural hair na bado naendelea kujifunza. Vichache nitashea na nyinyi hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…