Uturuki: Mbunge avunja simu yake kwa nyundo akipinga sheria kandamizi

Uturuki: Mbunge avunja simu yake kwa nyundo akipinga sheria kandamizi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mbunge huyo, Burak Erbay, mwanachama wa chama cha upinzani cha Republican People's Party amefanya tukio hilo alipokuwa akizungumza bungeni akipinga mswada unaoungwa mkono na Serikali.

Chini ya sheria hii, mitandao ya kijamii na tovuti zitalazimika kutoa maelezo ya watumiaji wanaoshukiwa ‘kueneza habari za kupotosha’, na inaweza kusababisha mshtakiwa kufungwa jela kwa miaka mitatu.

Wakosoaji wanadai mswada huo ukipitishwa kuwa sheria, utakiuka uhuru wa vyombo vya habari na kusababisha udhibiti mkubwa.
---

Turkey MP smashes phone with hammer in parliament

A Turkish MP has smashed his mobile phone with a hammer, while speaking in parliament.

Burak Erbay, who is a member of the opposition Republican People's Party, was protesting against a proposed government-backed bill which aims to combat online "disinformation".

Under this legislation, social media networks and internet sites would have to release details of users suspected of "propagating misleading information", and could result in the accused being jailed for up three years in prison.

Critics say that the bill, if passed into law, would infringe press freedoms and lead to widespread censorship.



Source: BBC
 
Meanwhile in Tanzania.

Waziri anaomba Bunge liidhinishe sheria ya Tozo mpya, wabunge wanampigia makofi na kumshangilia kwa kuongeza chanzo cha mapato.

Waziri huyo huyo anarudi Bungeni kuomba Tozo zipunguzwe ili kuwapa ahueni wananchi, wabunge wanamshangilia zaidi kwamba Serikali inajali wananchi wake.
 
Back
Top Bottom