Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mataifa ya magharibi yameshtushwa na uamuzi wa Uturuki kuziwachia benki zake 5 kutumia mfumo wa ulipaji kimtandao wa Mir ulioasisiwa na Urusi.Wakati huo huo Uturuki imeanza kununua gesi ya Urusi kwa kutumia sarafu ya Ruble ya Urusi.
Kutumika kwa mfumo wa kadi za Mir badala ya Visa na Mastercard kutawawezesha watalii wa Urusi kutembea na kulipia huduma nchini Uturuki bila shida yoyote.
Juzi raisi Erdogan alikutana kwa mazungumzo ya faragha na raisi Putin wa Urusi kwenye mji wa Sochi ikiwa ni wiki kadhaa tangu walipokutana kule nchini Iran. Nchi za NATO zinasema hatua hiyo ya Uturuki na mataifa mengine rafiki wa Urusi utavifanya vikwazo vya kiuchumi kwa Urusi kutokuwa na athari zilizokusudiwa.