Uturuki yaonywa kuingilia uchaguzi wa Ufaransa

Uturuki yaonywa kuingilia uchaguzi wa Ufaransa

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametahadharisha juu ya Uturuki kuingilia kati katika uchaguzi wa rais nchini Ufaransa mwaka ujao.

Emmanuel Macron: 'For me, the key is multilateralism that produces results'  | Financial Times


Ameituhumu serikali ya mjini Ankara kwamba inaeneza uwongo kupitia vyombo vyake vya habari. Akihojiwa na kituo cha televisheni nchini Ufaransa cha France 5, Rais Macron alisema amegundua rais Recep Tayyip Erdogan anataka kuimarisha uhusiano ulioharibika kutokana na mivutano kuhusu mgogoro nchini Libya, Syria na Nagorno Karabakh pamoja na tuhuma zilizotolewa na Uturuki kwamba Ufaransa ina chuki dhidi ya waislamu.

Macron amesisitiza kwamba Ulaya haitoipa kisogo Uturuki lakini pia amesema kuimarisha uhusiano na nchi hiyo litakuwa jambo gumu ikiwa serikali ya mjini Ankara haitobadili mienendo yake.

Rais huyo wa Ufaransa amesema amezungumza na mfalme wa Qatar Tamim bin Hamad al Thani ambaye ni mshirika wa karibu wa Erdogan, juu ya wasiwasi wake.
 
Aah wao wanaingilia mambo ya watu ...wao wakiingiliwa wanalialia
 
Back
Top Bottom