mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,588
- 11,668
Hii nchi kuna sehemu tulimkosea sana Mungu au Mungu anatuonyesha mwanga lakini watanzania tumelala? Ni njema kwa Mungu ni lazima tuelewe, CCM wamechoka JAMANI.
Nitaeleza mambo mawili,moja hii la ndege na la mwisho wastaafu wa TZR na URAFIKI.
Inawezekanaje tusimalize hili jambo na kujipanga kwa majanga yatakayojitokeza? Mvua hazijanyesha na zinaweza kuwa kubwa kupitiliza,je tumejipangaje kusaidia watu kwenye mafuriko? Tumekuwa na mbwembwe kila janga likitokea kwa miaka sasa na hili la ndege tumepata ufafanuzi mzuri tu kutoka kwa rubani ,huku tuna watu 19 wamepotea.
Tujikumbushe lile Janga la Morongora la Moto, yani Mjini lakini idadi ya magari ya zimamoto machache? Je unaweza kutafakari kuna idadi ya magari ya zimamoto mangapi katika wilaya zetu? Nikisema Watanzania tuna shida sehemu nitakuwa na makosa?
Nitatoa mifano katika wilaya za mkoa wa dodoma ambazo hazina zima mota wilaya zima,moja Mpwapwa ,mbili Kongwa ,tatu Bahi etc
Narudi kenywe Mada kuu, Hivi ni kweli hakuna hata mtu mmoja aliyetakiwa kuwajibika na uzembe uliyotokea Bukoba?
Alafu Serikali wanakomaa na public attention Kwa Majaliwa ambae hata waliookolewa wanadai hawajamuona akiokoa zaidi ya mhudumu wa Ndege (Air hostess)
Hii nchi kuna watu wanatia hasira sana. Yani kuna ujinga unaratibiwa na RC mpaka unasema hatuna viongozi nchi hii? Mambo ya aibu haya.
Tazama na hii ndio utajua hakuna viongozi nchi hii.
La Mwisho ni wazee wetu wa TZR na URAFIKI wana miaka 20 + hawana mafao kila siku wanapigwa tarehe, Je vijana wetu wakipa uongozi watakumbuka Taifa kweli? kama style ndio hii.
CCM ni Janga katika nchi yetu. Vipaumbele vya CCM katika nchi yetu.