Habari.
Mimi ni kijana wa kiume niliyebahatika kusoma uuguzi nchini Tanzania.
Nipende kuwapongeza wote waliobahatika kusoma uuguzi Tanzania maana moja ya kada inayoiendesha hospitali kwa asilimia kubwa sana na wanasaidia wagonjwa maana ndio wanaoshinda nao masaa 24.
Niseme ukweli mimi nitakuwa wa kwanza kuuacha uuguzi pindi nitakapoenda kujiendeleza elimu ya juu.
Nilisoma nikiwa na mapenzi ya dhati sana na moyo wangu ukiipenda hii kazi lakini niliyokutana nayo kazini ni Tofauti na hayo ndio yananifanya nikiri nitaiacha hii fani mapema sana.
1.Uuguzi Tanzania ni miongoni mwa kada za afya zinazodharaulika kupita kiasi na inaonekana kada ha watu wasio na akili hali ambayo ni tofauti kwa nchi za ulaya na uarabuni .
2.Upande wa maslahi uuguzi haiwezekani muuguzi wa degree Mwenye kusoma miaka minne sawa na mfamasia ,fizio yeye akalipwa TGHs C (around million 1 basics) wakati wenzake wakaanza na TGHs D(around million 1.3basics) na mpaka sasa inaonekana kawaida.
3.Upande wa Hopitali muuguzi anaongozea kudharauliwa sana na watu wa kada nyingine Hasa medical doctor kwa kumchukulia muuguzi kama mtu aliye muoa(mke wake)kiasi kwamba hospital nyingine hasa za mission wauguzi wamekuwa wakiwekeana zamu ya kuwapikia na kuwaandalia madaktari chakula.
4.Jamii inamuona muuguzi katili na mtu Mwenye majibu ya ovyo hali ambayo ni tofauti kwa wauguzi wa hivi karibuni wanaojaribu kupambana kwa hali na mali kubadilisha Hadhi ya uuguzi lakini bado hali inaonekana muuguzi ni katili ndo maana kila lawama za hospitali ni MUUGUZI.
5.Muuguzi Hajapewa nafasi ya maamuzi ya matibabu kwa mgonjwa hata kwenye emergency kiasi kwamba kutoa panadol tu mpaka amsubiri daktari hali ambayo ni tofauti kwa nchi za wenzetu hasa ulaya na muuguzi hajawekwa sehemu ya uongozi wala maamuzi ya hospital ilhali muuguzi wa degree Anasoma vitu vingi vinavyohusu mgonjwa na uongozi pia.
6.Chama cha Wauguzi TANNA na TNMC haviko katika minajili ya kumsaidia muuguzi zaidi ya kumkandamiza na kumnyanyasa ndo maana kila siku kazi yao kuongelea maadili lakini wanamwacha muuguzi huyu kwenye mazingira magumu kumsaidia kwenye masuala ya maslahi ,hela ya overtime ,na haki zake binafsi.
Wauguzi wa nchi za wenzetu kama Nchi za ulaya wameufanya ionekane kada bora na yenye malipo mazuri na zaidi kuwafanya wafanye kazi kwa ufanisi na kuspelize kabisa kama muuguzi wa watoto,usingizi,magonjwa tofauti na nchi ya Tanzania muuguzi amekuwa ni kilaka wa kufanya kazi popote pale .
Muuguzi wa ulaya analipwa hela nzuri kwa lisaa wengine hasa wa ICU wamezidi mishahara hata baadhi ya madaktari.
Kiukweli mambo ni mengi ila kama kada ya uuguzi Tanzania haitabadilika tutarajie kupunguza idadi kubwa ya vijana kusoma uuguzi hasa wanaume.
Wa kwanza nitakuwa Mimi.