1. Si kweli kwamba uuguzi unadharaulika sana. Japokuwa kuna baadhi ya wajinga wana udharau.
2. hapo nakuunga mkono.
3. Hapa majibu ni kama namba moja.
Lakini pia wauguzi wenyewe mnasababisha kudharauliwa kwa sababu ya kutokujitambua. wengi majukumu yao hawayajui, wanasubiri kutumwa na kada nyingine, na hata wakipewa orders hawatekelezi kama standard zinavyotaka.
Matokeo yake ni kudharaulika na kutumwa kuchemsha chai.
Hivi wewe Muuguzi unaejitambua umesoma three years au four years unakubalije kwenda kumchemshia chai mtu mwingine Hayo yalikuwa zamani ila sio leo. badilikeni.
4. Majibu ya ovyo.
Hii ni kweli, na chanzo ni wauguzi wenyewe, hasa hawa mama zetu na dada zetu.
Tatizo ni maadili kutokuzingatiwa sana huko shuleni.
Zamani watu walikiwa wanapita tuu na kozi za muda mfupi anakuwa muuguzi tayari. Hii imechangia sana kuleta wapuuzi kwenye hiyo
kada.
5. Duniani kote muuguzi anafanya kazi kwa kuzingatia order ya daktari.(except kwa wale ambao nicertified practitioner huko majuu)
Hiyo ndiyo kazi kuu Ya muuguzi,
Hospitali kumegawanywa majukumu
kuna anae diagnose na kupriscribe
Mwingine ana dispense
Mwingine ana administer
Mwingine ana investigate.
na wote hao wanafanya kazi kwa kushirikiana kwa pamoja.
Katika emergency wauguzi wamekuwa wakifanya maamuzi mbalimbali.
mfano mgonjwa yuko kwenye cardiac arrest huwezi kusema unasubiri daktari akuambia ndio muanze CPR.
muhimu muuguzi hakikisha umeiva kwenye kila kitu kinachokuhusu hakuna atakae kusumbua wala kukudharau.
6. Kwanza kijana inabidi uelewe Tanna na TNMC ni nini.
Tanna ni chama cha wauguzi.
hii ndio inatakiwa kuwa sauti ya wauguzi.
TNMC ni baraza la wauguzi na wakunga wauuguzi.
Kitu kimoja elewa TNMC ipo kwa ajili ya KUILINDA JAMII DHIDI YA HUDUMA ZITOLEWAZO NA WAUGUZI NA WAKUNGA.
Tnmc haiko kwa ajili ya kumtetea muuguzi.
TNMC ni mkono wa serikali.
Ndio maana wajumbe wote wanateuliwa na waziri wa afya.
Mwisho, Uuguzi ni Kada nzuri na muhimu kwenye uhai wa sekta ya afya.