Kama nilivyomwelewa Mwanzisha Thread, analalamika kuwa hali imekuwa si kawaida. Tunafahamu kuwa erection hutokea nyakati fulani mtu akiwa amelala, lakini inapofikia kiwango cha mtu kusumbuka hiyo si kawaida ila ni tatizo.
Ingawa mada hii imefanyiwa mzaha, ninapenda kuwataarifu kuwa erection ambayo si ya kawaida inaitwa ''Priapism''. Hii inaweza sababishwa na mambo kadhaa ambayo yanaathiri mzunguko wa damu katika uume. Priapism inapodumu kwa masaa 4 mfululizo huishia na Impotance [Uhanisi]. Kama hakutakuwepo na hatua madhubuti basi uhanisi utakapotokea hauwezi kurekebishwa[Irreversible]. Uhanisi wa aina hii si upungufu wa nguvu za kiume ambao unaweza kusaidiwa na dawa kama viagra bali ni ukomo wa tendo la ndoa kwa mhusika.
Sielewi ni kwa kiasi gani mto mada ana ukweli, huenda ameamua kuchangamsha forum, lakini kwa dhati kabisa nakueleza kama kuna ukweli basi hiyo ahadi ya mtu kuzuia magoli inaweza isitimie si siku ya kurudi nyumbani tu lakini forever, ni muhimu uonane na Daktari.
Ahsante