Ndugu zangu habarini, nilikuja hapa siku za nyuma nikiwa na tatizo la kutosimamisha.
Namshukuru Mungu sana nimepona, nawaombea pia wale ambao wanasumbuliwa na tatizo kama hili Mwenyezi Mungu awape wepesi wapone.
Binafsi nimepitia uzoefu mkubwa sana kipindi hiki Cha mpito, ila nawashukru Wana JF wote walionyesha Nia ya kunisaidia na wengine walinisaidia kadri ya uwezo wao. Lakini wapo pia ambao walikuwa kimaslahi zaidi kupitia changamoto yangu.
Nimetumia dawa nyingi sana nashindwa kuelewa hata niseme nimepona kwa dawa ipi, ila yote kwa yote Mungu ashukuriwe mno.
Nilienda kwa baba mmoja yeye anadili na magonjwa ya wanaume kushindwa kusimamisha tu, ni tabibu Toka 1990's nilikuta vijana wengi wakipata Tiba hapo nyumbani kwake, ila yeye sio Mganga ni mtu aliyeachiwa dawa na baba yake.
Nilichogundua vijana wengi kwasasa wanasumbuliwa na tatizo hili, alinipa huduma ila Mimi sikutaka kukaa hapo kama wengine maana Mimi tatizo langu halikuwa clonic kiasi Cha kuishi pale. Nimetumia dawa nyingi nashindwa kujua hata nimepona kwa dawa ipi.
Ila namshukuru Mungu sana nimepona, Mungu aendelee kubariki hili jukwaa la JF.