Wana JF, kabla ya kusema, hili gazeti ni udaku, mwandishi siyo makini nk. ni vema kuhakikisha kuwa hizo figure zipo sahihi au la. Nimetafuta kila njia kuwasiliana na wahusika bila ya mafanikio. Sasa tunaweza kuendelea kuchunguza thamani ya misaada itolewayo na hawa wafadhili wetu. Hizi figure za ajabu ajabu na hasa penye misaada ya mashule iwe ni vitabu madawati nk. ni jambo la kawaida, sema wengi wetu hatujalikazia macho maana linakuja na kiini macho cha charity au wizi unaofanywa na halimashauri husika.
Kwa vile wanao pokea misaada wanaghubikwa na furaha ya kupokea mzigo, kesho mfadhili akija kuomba chochote, wao watakumbuka mamilion!! madawati!! nk. japo thamani iliyotajwa si sahihi. Hii ni kwa vile hawafahamu hata neno milliion ni ninii? Hii habari imezidi kunikumbusha yule adui UMASIKINI ambaye JKN aliona na mapema mojawapo ya maadui wakubwa.
Mafisadi wanajua fika njia nzuri ya kuendelea kututawala na kutugandamiza ni kutufanya masikini na mafukara maana haya yanawafanya waathirika wanyonge, waoga na hata kudhohofisha uwezo wa kufikiri. hapa imejidhihirisha, hivi Bw. CheUngele alishindwa kufanya mahesabu ya haraka haraka na kumwuliza huyu mfadhili kama figure anazotoa ni sahihi au la?