Uuzaji pombe hovyo sasa ni hatari kwa jamii. Vibanda vingi mtaani/stendi kila sehemu wanauza pombe

Uuzaji pombe hovyo sasa ni hatari kwa jamii. Vibanda vingi mtaani/stendi kila sehemu wanauza pombe

white wizard

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2011
Posts
8,566
Reaction score
13,770
Kwa hali iliyofikia huku mtaani sasa serikali inatakiwa kuingilia kati. Kwani sasa vibanda vingi mtaani/stendi kila sehemu wanauza pombe hasa hizo kali, jamii ya konyagi, kwa sasa utakuta kibanda kinauza machungwa, pipi, soda, unga, mkaa hapo hapo wanauza pombe kali

Kwani mamlaka husika hasa halimashauri, ambao wanatoa leseni wako wapi? Sioni hata umuhimu wa kupiga marufuku vile viroba kwani hata sasa pombe ya 500, inapimwa. Jamani Serikali jaribuni kuliangalia hili suala, pombe ziuzwe sehemu husika tu.
 
Sio kila kitu kuiita serikali iingilie kati, kama wanywaji hawawezi kujicontrol basi serikali haitaweza kufanya lolote maana shida inaanzia kwenye akili za wanywaji.
 
Cha ajabu watu wenye leseni wamepewa masharti kwamba wauze Pombe kuanzia SAA 10...ila Pombe inauzwa kwa wasio na leseni ya kuuza Pombe yaani viduka vya mtaani vinauza Bia na Pombe zote Kali...hao Machinga ndo usiseme wanaweka bia kwenye madeli na mabarafu ili ziwe za baridi na wanauza kuanzia SAA 11 asubuhi na wengine wanakesha...mfano halo Mbezi tu.

Kifupi hakuna serikali bhana...kuna wapenda sifa Fulani tu...wanafanya mambo kwa kick tu...yaani mtu analipa kitambulisho 20k anauza na Pombe...mwenye leseni ya duka la vyakula..anauza Pombe...Mwenye leseni ya kuuza Pombe..masharti magumu anawekewa mpaka kupelekea wengi kufunga biashara...

Serikali inahujumu uchumi wetu kwa kupenda sifa..kama hawawezi kudhibiti uuzwaji pombe kiholela waziache bar na groceries ziendelee na utaratibu wake...maana tangu zianze kufunguliwa SAA kumi sijaona mabadiliko yeyote Zaidi ya hali ngumu kwa wanaolipia leseni za biashara...Ifike kipindi tuwaambia ukweli wapenda sifa hawa...wanatuharibia nchi...wengine hatupendi siasa ila kuna mambo tunayaona tunashangaa Sana asee
 
Sio kila kitu kuiita serikali iingilie kati, kama wanywaji hawawezi kujicontrol basi serikali haitaweza kufanya lolote maana shida inaanzia kwenye akili za wanywaji.
Kwa hiyo hizo sheria ndogo ndogo ambazo zinatungwa na halimashauri /manisipaa huwa ni za nini? Kwani miaka ya nyuma yote pombe ilikuwa inajulikana inapatikana sehemu gani, na wanakuwa na leseni, mbona hawakuachiwa wanywaji waamue? Sehemu nyingi kwa sasa kwenye sehemu rasmi za kuuzia pombe kuna muda maalum wa kuuza pombe, kwanini wasiwaachie wanywaji tu, wajiamulie,ukisema uendeshe nchi kwa kuwaacha watu ndio waji control kwenye mambo, utaaweza kuongoza kweli?! Ndio maana kuna by laws, uzoaji taka tu kuna sheria zinazosimamia sembuse kwenye pombe?
 
Hapo mkuu umenena vizuri!! Ki ukweli wenye bar/grocery nawaonea huruma sana kwani leseni ina masharti kibao, kufungua ndio hiyo jioni, ulipe pango, tra, leseni, halafu kuna mtu ana kibanda tu, hasumbuliwi yeye toka asubuhi hadi asubuhi anauza tu, na wala hasumbuliwi kisa ana kitambulisho cha 20,000 na wengine hawana hata hicho kitambulisho. Kisa mambo ya siasa, mbona zamani haya kuwepo?

Ni awami hii tu, sheria hazina umuhimu bali ni matakwa ya kiongozi!! Siku moja nilimsikia trafic mmoja anazungumzia kuhusu hao wafanya biashara wa pembeni mwa barabara akasema kisheria, ni marufuku, ila kwakiwa wameambiwa wawaache hawana jinsi, japo ni hatari sana!!!
 
wape biashara nyingine ya kufanya pia usisahau kuwapa na mitaji mikubwa.
 
Hapo mkuu umenena vizuri!! Ki ukweli wenye bar/grocery nawaonea huruma sana kwani leseni ina masharti kibao, kufungua ndio hiyo jioni, ulipe pango, tra, leseni, halafu kuna mtu ana kibanda tu, hasumbuliwi yeye toka asubuhi hadi asubuhi anauza tu, na wala hasumbuliwi kisa ana kitambulisho cha 20,000 na wengine hawana hata hicho kitambulisho. Kisa mambo ya siasa, mbona zamani haya kuwepo? Ni awami hii tu, sheria hazina umuhimu bali ni matakwa ya kiongozi!! Siku moja nilimsikia trafic mmoja anazungumzia kuhusu hao wafanya biashara wa pembeni mwa barabara akasema kisheria, ni marufuku, ila kwakiwa wameambiwa wawaache hawana jinsi, japo ni hatari sana!!!
Inasikitisha sana ndugu...siasa zinatupeleka pabaya sana
 
wape biashara nyingine ya kufanya pia usisahau kuwapa na mitaji mikubwa.
Inshu sio biashara nyingine, au mtaji mkubwa, ila ni suala la utaratibu tu!! Popote kule uuzaji pombe una utaratibu wake, ndio maana hata leseni zake zinakuwa na masharti mengi,. Mfano biashara ya chuma chakavu kwa sasa zina masharti magumu, baada ya kuwa watu walikuwa wananunua hata mabomu bila kujua, wee pombe hadi,pembezoni mwa barabara?!!!
 
Back
Top Bottom