Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Wadau.
Hapo juzi Serikali kupitia Manispaa ya Temeke imetangaza kuuza viwanja vilivyopimwa maeneo ya Gezaulole na kuwataka wanaohitaji kulipia form Tshs 30,000/- pamoja na picha 3.
Habari "za ndani" ambazo nimezipata ni kua zoezi hili ni batili na limejaa utapeli kama ilivyokua viwanja vya Tabata Kinyerezi ambapo mpaka leo hakuna anaejua lilivyoishia.
Utapeli huu unatokana na ukweli kwamba Wakati serikali inakusudia kuuza viwanja karibia 5,000, Pia imewahidi wakazi wa maeneo hayo kua wasiwe na wasiwasi kwani nao watapatiwa viwanja hivyo.
Utapeli unakuja pale ambapo wakazi hao nao ni zaidi ya 5000 hivyo kuna tetesi kua hivi vya mwanzo watapewa kwanza wao VYOTE.
Utata mwingine ni kwamba wakazi hao ambao leo walikua na mkutano na Manispaa, waliahidiwa kuuziwa viwanja hivyo kwa bei ya Tshs 1,000/- kwa 1sqm kupitua makubaliano maalumu waliosainishana na mabispaa tofauti na bei iliyotangazwa na ya Tshs 3,000/- hivyo wamedai kusalitiwa jambo ambalo hawatakubali, bali kwenda mahakamani kusimamisha zoezi hilo la ugawaji wa viwanja!!
Katika hatua nyingine, wakazi hao wa Gezaulole wamelalamikia kitendo cha Manispaa kulazimisha kupima mashamba yao ambayo yako mbali na mji na kuliacha shamba la Rais Mstaafu Bwana Benjamin William Mkapa.
Walidai kua Mkapa ana shamba Zuri tu kwa Viwanja na liko eneo zuri na karibu zaidi na Mijini kuliko wao hivyo anashangaa kwanin serikali inashupalia mashamba yao,tena kwa malipo kiduchu!!
Source;