Ndachuwa
JF-Expert Member
- Mar 8, 2006
- 6,269
- 4,579
Kwa muda sasa nimebahatika kuhudhuria baadhi ya sherehe za "send off" na kushangazwa sana na uvaaji wa yule anayeagwa.
Waalikwa wote kwa maana ya wake kwa waume huwa wamevaa nadhifu kwa maana ya kufunika sehemu zote za miili yao. Lakini kituko ni yule anayeagwa ambaye siku hiyo huwa nusu uchi yaani ngua inaanzia kwenye chembe cha moyo shuka chini.
Nisichoelewa wote tumealikwa ili tukamuage tayari kwa maisha mapya ya kuwa na mwanaume mmoja, badala ya yeye kuonyesha staha ya jinsi atakavyokuwa kwa mumewe siku hiyo yeye hugeuka kituko fulani kwani kwa tamaduni za kiafrika huo uvaaji haukubaliki mbele ya wazazi wake.
Sasa kama ameshafanya maamuzi ya kuwa na mwanaume mmoja, hiyo vaa yale inatuma ujumbe gani kwa wanaume wa aina ya fataki walioko kwenye hiyo sherehe? au anataka kuwaambia nini wale vijana ambao pengine nao walikuwa kwenye mbio za kumtaka wakazidiwa?