Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,720
- 6,957
Aina hii ya mavazi huvaliwa Ulaya na Amerika ya kaskazini kipindi hichi cha mwaka kwa sababu ya baridi kali na barafu inayodondoka huko. Kichekesho ni pale unapomwona mtu mzima na akili zake amevaa mavazi haya hapa Dar huku joto likiwa kali kiasi kwamba wewe uliyevaa T-shirt tu unatamani kuivua utembee kifua wazi.
Huu ni ulimbukeni wa kiwango cha kupitiliza, hata Wazungu waliobuni aina hii ya mavazi wakiona mtu amevaa mavazi haya huku kwetu na joto lote hili la Dar huwa wanacheka sana, wanatudharau sana na kutuona bado sana sisi ni watumwa wa fikra.
Kuna watu watatetea ulimbukeni huu kwa kisingizio cha sikukuu ya X-mass ambayo nayo ni upagani tu wala haina maana yoyote katika dini ya KWELI ya KIKRISTO. Na wengine watasema ni namna ya kuvutia biashara; lakini bado haileti maana hata kidogo. Nasema haileti maana sababu hakuna uhalisia wowote ule wa kuvaa nguo kama hizi sana sana anayevaa anageuka kuwa kituko kwa wale wanaoelewa maana ya mavazi haya.
Kwa akili hizi sisi Waafrika tutabakia kuwa watumwa wa Wazungu mpaka siku ile BWANA YESU atakaporudi tena kwa mara ya pili. Kwa akili hizi ndio maana Wazungu wanatuibia madini yetu mpaka na mchanga pia wanachukua na kusafirisha kwenda kwao tena tukiwasindikiza sisi wenyewe mpaka uwanja wa ndege na bandarini huku tukiwalinda na silaha nzito, na wao kutuachia mahandaki matupu.
Ningekuwa mimi ni Rais wa nchi hii ningepiga marufuku kabisa aina hii ya ulimbukeni kama alivyofanya Rais wa Korea ya Kaskazini Kim Jong-un; amesema hataki kabisa kuona raia wake wanasheherekea X-mass ama wanajihusisha na tamaduni zozote zinazoambatana na sherehe hizi za kipagani zilizoanzishwa na Wazungu wa Rumi.