Uvamizi wa ardhi nchini ni tatizo kubwa

Uvamizi wa ardhi nchini ni tatizo kubwa

Kamukhm

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2015
Posts
2,801
Reaction score
4,212
Kuna dhana inayojulikana kama Guerrilla Urbanization, miji kukua hovyo bila kufuata utaratibu ambayo pia inakuja na element uvamizi wa ardhi kwa kiasi kikubwa. Kwa kipindi kirefu mchezo huu umekuwa ukiitafuna Pwani & Dar es Salaam. Na kama hatutatafuta muarobaini itakuwa ni the new norm

Shida ya kuendelea kuifumbia macho tabia hii, kwa manufaa ya muda mfupi ya watu wachache kutapelekea Mfumo wetu wa kusimamia ardhi kulega na kupoteza sifa na Imani kwa mtu mmoja mmoja na kwa taasisi na mataifa mengine. Na Mfumo usipoaminika athari zake ni kubwa kwa kipindi cha muda mfupi na mrefu.

Athari zake ni pamoja na:-
• Kuwa na utamaduni wa kuoperate nje ya Mfumo unaopelekea kuwa na miji isiyoweza kusimamiwa. Kutokana na nature yake ya kukua hovyo nje ya utaratibu

• Miji isiyoweza kusimiwa ni miji dumavu, ambayo haiwezi kuwa mashine ya kukuza Hali ya kipato kw mwananchi mmoja mmoja kutokana na kushindwa kukusanya mapato Ili kuwezesha uendeshaji na kuwa na ukuaji usiokuwa na mipango hivyo mahitaji yake ni ngumu kuwa forecasted.

• Kukosa security of land uses, ambayo ingesaidia masoko (establishment's catchment) kulindwa..Ili kuisaidia biashara kukua na kukomaa hivyo kutoa ajira na vyanzo vya masoko ya huduma na bidhaa/malighafi.

• Na mwisho ni migogoro na hatimaye uvunjifu wa amani. Kama hii itaendelea Iko siku ulinzi pekee wa ardhi utakuwa no kufyatuliana risasi na kukatana mapanga.. na hii itakuwa aibu kwa nchi yenye ardhi kubwa kama Tanzania.

Sasa yote haya yanaendelea kuonekana kila kukicha, na idadi ya wavamizi hasa kwa mkoa wa Dar es salaam na Pwani is staggering.. basically hii imekuwa biashara kabisa with lawyers, funders and all sorts of enablers.. and I fear we are not taking it seriously enough...

Kwanza lazima serikali iache kujihusisha na mediation, Hawa watu wanaovamia ardhi zilizopimwa na kumilikishwa kwa mujibu wa sheria ni waarifu, tena wa jinai kabisa.. wanapaswa sio tu waondolewe kwenye maeneo waliyovamia ila washitakiwe na wafungwe.

Wengi wanaweza wasikubaliane na Mimi, Ila ukweli unabakia kuwa kama tunataka kuwa na nchi inayojinasibu kuwa inautawala Bora wa sheria lazima Sheria zake za ardhi ziheshimiwe. Sio labda ni Lazima.

Sheria za mipango miji, sheria za uhifadhi, sheria za usimamizi na Umiliki wa ardhi lazima ziheshimiwe. Kitendo cha mtu kwenda na kuvamia eneo lililogawiwa kwa mtu mwingine kisheria hakipaswi kuchekewa hata kidogo.

Nani atakuja awekeze kwenye nchi ambayo serikali inashirikiana na wahalifu kucompromise kwenye maswala ya uvamizi wa milki inayotolewa na serikali yenyewe? Ardhi inapangwa na inaombwa kwa kutengemea matumizi, unapokuta wavamizi na na kama serikali unahalalisha na Tayari unakuta mtu amekwisha weka uwekezaji wa awali akitarajia kuendelea kufanya upanuzi taratibu kwa kuwa eneo analo unaharibu mipango ya baadae ya uwekezaji huu.

Ukisha kufanya hivyo kwa wawekezaji wawili, kinachotokea ni Loss of trust.. na kwa wachache (ambao hawana namna) wanaokuja watakuwa wanaomba ardhi in excess ambao inaongeza tu gharama za Umiliki kupitia utwaaji na kodi ambayo. for sure will have implications kwenye bei ya bidhaa au huduma au hata mishahara ya wafanyakazi kupunguzwa kufidia.

Watu wanalipa hizi land rent kwasababu ya government guarantee kwamba haki zao za kuitumia ardhi na mipaka yake zitalindwa na kuheshimiwa. Sio kwa sababu wanaipenda serikali, it's give and take.

Hebu tuwe serious, kama Taifa. This need to End. Na sisi wananchi this is absurd and utterly stupid and very selfish. Tuache.
 
Back
Top Bottom