UVCCM, CCM tuanzishe maandamano nchi nzima kuunga mkono mapendekezo ya mabadiliko ya katiba!!!

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2008
Posts
4,768
Reaction score
2,361
Wazee wa busara walisema , mtu akidanganya mara kwa mara bila uongo huo kukanushwa hadharani, wale wasioujua ukweli watadhani uongo huo ni ukweli.

Katika mchakato wa Katiba Mpya, wapinzani , hususan CHADEMA na CUF wameshikilia bango Rais kutoweka sahihi kwenye muswada mkakati wa mabadiliko ya katiba.

Wapinzani wanajisahau kuwa wana makelele mengi, lakini kuna watanzania waliowengi sana ambao hawaungi mkono vurugu zao.
Bungeni, wao wachache(kama watu 40 hivi) wakasusia majadiliano ya wengi(karibia wabunge280) kuhusu mkakati huo wa mabadiliko ya katiba.

Wazungu wanasema ni vyema ku-call a spade a spae, uVCCM na CCM inabidi wajipange na waanzishe maandamano ya kuunga mkono wabunge wao nchi nzima.

Ni vema wapinzani wakajua kuti walilolikalia!!
 
Msisahau kumkosoa Ndugai kwa kufikiri wabunge ni misukule
 
255306_253545028099538_105015986_n.jpg
 
Thubutu kama utaweza kuwapata watu wa kutosha, xaxana utaishia kuona wanaccm waliosombwa na Maroli toka Mashenzini.
Katiba mpya si ya CCM, acha upofu wako. Na usidhani CCM itakuwa madarakani milele, katiba ni mali ya wananchi kwa nini CCM kupitisha mswaada unaoonekana kuleta walakini. Post yako wala haina mashiko; Si wapinzani tu walioukataa mswaada huo bali ni watanzania wote ambao si wanachama wa CCM. Mimi sina Chama chochote lakini napiga kitendo cha CCM kutaka kuibaka katiba.
 
kwani wewe unadhani katiba ni ya chadema kama unavyofiri na akili yako.
 
Kikao kinaendelea pale Protea - Tungoje TAMKO rasmi.

ila mimi nitachanganya na za kwangu..
 
U better think 50 yeras to come wajukuu zako watakuwa na shepu gani. With ur greedY u will end up being mateja for having cheap moneys from taxpayers jasho. WAKEUP UR STATUS QIO WONT HELPYOU LONG UR TURNING TO BE WATU WA AJABU DUNIANI WASIOJUA UTU WAO.
 
Enyi kundi dogo la matapeli, fanyeni tu hayo maandamano harafu mlifundishe kundi kubwa la watu wema namna ya kuandamana nchi nzima kisha mtajifunza kuwa wanyenyekevu na watu wema
 
Wazee wa busara walisema , mtu akidanganya mara kwa mara bila uongo huo kukanushwa hadharani, wale wasioujua ukweli watadhani uongo huo ni ukweli.

Katika mchakato wa Katiba Mpya, wapinzani , hususan CHADEMA na CUF wameshikilia bango Rais kutoweka sahihi kwenye muswada mkakati wa mabadiliko ya katiba.

Wapinzani wanajisahau kuwa wana makelele mengi, lakini kuna watanzania waliowengi sana ambao hawaungi mkono vurugu zao.
Bungeni, wao wachache(kama watu 40 hivi) wakasusia majadiliano ya wengi(karibia wabunge280) kuhusu mkakati huo wa mabadiliko ya katiba.

Wazungu wanasema ni vyema ku-call a spade a spae, uVCCM na CCM inabidi wajipange na waanzishe maandamano ya kuunga mkono wabunge wao nchi nzima.

Ni vema wapinzani wakajua kuti walilolikalia!![/QUOTE

]

kipofu
 
kwani wewe unadhani katiba ni ya chadema kama unavyofiri na akili yako.
Nimeandika kwamba katiba ni mali ya watanzania wote hata wasiokuwa na vyama kama mimi hapa, na wala si mali ya vyama vya siasa kama unavyojidanganya eti ufanye maandamano. Kwani maandamano ya nini wakati Ndugai na maCCM wengine wameshajichanganya. Subiri uone moto utakaowaka muda si mrefu. Mioyo na akiri za watu zimeshajiandaa kisikolojia liwalo na liwe lakini Mswaada haukubaliki...Bunge wameshamaliza kazi yao kwa sasa maamuzi yamebaki wa rais JK na sisi Wananchi ambao ndo wenye mali( katiba); Sisi hatuna cha kula ila tunabadilisha maamuzi mambaya ya bunge kwa Nguvu ya Umma ( Maandamano).
 
Niliona katika Kipima joto cha Itv kuhusu rasimu hiyo iliyipitishwa na bunge kama ina manufaa kwa Tanzania na Watanzania, ni watu watano tu kati ya 139 waliosema ndio ina manufaa. Wengine waliobaki 134 walisema hapana. Kama mtu hawezi kuona kwamba hicho ni kiashiria tosha, ana lake jambo.
 
Nyerere mwaka 1992 aliacha maoni ya watanzania 80%,akachukua 20%wote tukamwona ana busara na matunda yake leo hii tunayashuhudia.
kwa akili ndogo za waliobaki ccm hata hilo hawalioni wao wingi ni hoja.
nawashauri maandamano yaanzie arusha au zanzibar.
 
Kinachwafanya wananchi kuunga mkono upinzani ni kwamba mambo ya msingi na yakidemokrasia mnayakataa ubabe mwingi na udictator hii sio katiba ya ccm ni watanzania wote jaribuni kuweka maslahi ya taifa mbele najua mnadamu ya kijani lakini penye ukweli ccm mjisahihishe usidanganye umma kuwa watnzania wnachukia chadema na cuf hali ni tofauti huku mitaani
 
Katika hesabu zako usisahau kuwa mbunge mmoja wa upinzani ukitoa mrema, shibuda, cheyo wa udp ni sawa na wabunge wa CCM 50.Na kama akili yao sawa na lusinde zidisha idadi yao mara 2.
 
Thubutu kama utaweza kuwapata watu wa kutosha, xaxana utaishia kuona wanaccm waliosombwa na Maroli toka Mashenzini.
Katiba mpya si ya CCM, acha upofu wako. Na usidhani CCM itakuwa madarakani milele, katiba ni mali ya wananchi kwa nini CCM kupitisha mswaada unaoonekana kuleta walakini. Post yako wala haina mashiko; Si wapinzani tu walioukataa mswaada huo bali ni watanzania wote ambao si wanachama wa CCM. Mimi sina Chama chochote lakini napiga kitendo cha CCM kutaka kuibaka katiba.
Kwa nini mnakuwa na woga?
Si mmetyataka!
Na itakuwa nani zaidi, na hata wakiletwa na malori kwani si wapiga kura hao ?
Watu wenye mawazo ya kifashisti mtapatikana mwaka huu!
Lazima mbichi na mbivu zijulikane, mimi niambiwe yanaanzia wapi tu nilichukue tawi langu lote.
 
ccm wanadai ni serikali.walikuwa wanapinga maandamano sasa watakubali kwanza ili waanze au wanafanyaje?hata mikutano ya hadhara walitoa mapendekezo ya kwamba baada ya uchaguzi hakuna siasa sasa wapo kwenye mikutano mbali mbali na kwa bahati mbaya sana kinana amejisahau anafikiri yeye ni kiongozi wa serikali na sasa ana kagua miradi ya maendeleo.

Wazee wa busara
walisema , mtu akidanganya mara kwa mara bila uongo huo kukanushwa
hadharani, wale wasioujua ukweli watadhani uongo huo ni ukweli.

Katika mchakato wa Katiba Mpya, wapinzani , hususan CHADEMA na CUF
wameshikilia bango Rais kutoweka sahihi kwenye muswada mkakati wa
mabadiliko ya katiba.

Wapinzani wanajisahau kuwa wana makelele mengi, lakini kuna watanzania
waliowengi sana ambao hawaungi mkono vurugu zao.
Bungeni, wao wachache(kama watu 40 hivi) wakasusia majadiliano ya
wengi(karibia wabunge280) kuhusu mkakati huo wa mabadiliko ya katiba.

Wazungu wanasema ni vyema ku-call a spade a spae, uVCCM na CCM inabidi
wajipange na waanzishe maandamano ya kuunga mkono wabunge wao nchi
nzima.

Ni vema wapinzani wakajua kuti walilolikalia!!
 
Wazee wa busara walisema , mtu akidanganya mara kwa mara bila uongo huo kukanushwa hadharani, wale wasioujua ukweli watadhani uongo huo ni ukweli.

Katika mchakato wa Katiba Mpya, wapinzani , hususan CHADEMA na CUF wameshikilia bango Rais kutoweka sahihi kwenye muswada mkakati wa mabadiliko ya katiba.

Wapinzani wanajisahau kuwa wana makelele mengi, lakini kuna watanzania waliowengi sana ambao hawaungi mkono vurugu zao.
Bungeni, wao wachache(kama watu 40 hivi) wakasusia majadiliano ya wengi(karibia wabunge280) kuhusu mkakati huo wa mabadiliko ya katiba.

Wazungu wanasema ni vyema ku-call a spade a spae, uVCCM na CCM inabidi wajipange na waanzishe maandamano ya kuunga mkono wabunge wao nchi nzima.

Ni vema wapinzani wakajua kuti walilolikalia!!
watakapoandamana wasisahau kuvaa nguo zao za kijani na njano ili tuwajue ni kina nani wanawaunga mkono wanaotunyonya
 
CDM wamezidi ngebe, namfagilia sana Kinana kwa kundeleza mapigo.
Lakini sasa tunataka maandamano ambayo yataondoa wasi wasi kuwa CCM bado ni nambari wani.
Wana CCM tuyataka hayo maandamano kuzima hii ngebe ya wachache kutaka kuleta vurugu.
 
Back
Top Bottom