MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Katika hali isiyokua ya kawaida inadaiwa kua kuna vuguvugu la ndani kwa ndani katika umoja huo linalohusishwa mikakati ya kuomba uungwaji mkono kutoka ngazi za juu ili kuitisha kikao cha wajumbe wa umoja huo kuelezea hisia zao ambazo wamekua wamezikalia nyoyoni kutokana utendaji usioridhisha wa mwenyeki wao Hamidu Shaka.
Kuna fununu ambazo zinadakwa na baadhi ya makada wa chama hicho tulionao karibu wakidai kua ni kweli hawaridhishwi na utendaji wa mwenyekiti wa umoja wao na wanaona ni kama mzigo ndani ya jumuiya yao, wameenda mbali zaidi kwa kudai hakuna hamasa kabisa za kukuza itikadi za chama kama ilivyokua enzi za kina Shigela na Nchimbi.
"Tuna mwenyekiti jina tu mwoga mwoga asiyetaka kuelekezwa jambo, mimi nitakua tayari moda wowote kuongozana na wenzangu kwenda kwa katibu mkuu wa chama kumwelezea ukweli wa mambo" hii ilikua ni kauli ya kada mmoja na mjumbe wa umoja huo ambaye nae anaonekana wazi kabisa. kutoridhishwa na mwenyekiti wao ndugu Shaka.
Kikubwa kinachoonekana kuwakera vijana wa umoja huo ni ukimya na woga wake kuendelea kuwalea baadhi ya watu wanaofuja maji za umoja wao bila hata kuwakemea au kuwachukulia hatua zozote, Wamesema kua kitendo kumchukulia hatua kada wa chama hicho ndugu Sixtus Mapunda na wenzake ilikua ni kama tone la maji ndani ya bahari lakini pamoja hivyo wanalalamikia kuwaona watu hao wakiendelea kuranda mtaani huku wakiwa na kadi za chama.
Kuna miguno msingi sana ndani ya taasisi ya umoja huo wa chama tawala ambayo inaonekana umaarufu wake ukipungua siku hadi siku tofauti na siku za nyuma kwa sababu ambazo wengi wanadai chanzo ni mwenyekiti wao ndugu Shaka Hamidu.