Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Nyie UVCCM kauli za wapinzani zinasumu kwenu?
Vipi kauli zenu nyie CCM na kauli zenu ya kwamba ni kauli za asali sana. Embu kuwe weledi hata kidogo basi
================
Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mtwara, katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika tarehe 25 Juni 2026, limepitisha maazimio mbalimbali yenye lengo la kuimarisha umoja, amani, maendeleo na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030.
Katika kikao hicho, Baraza limempongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa uongozi wake mahiri na kazi kubwa anayoendelea kuifanya nchini, hususan Mkoa wa Mtwara kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayowanufaisha wananchi.
Aidha, Baraza limeendelea kuviunga mkono na kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa juhudi zao za kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani, utulivu na usalama. Baraza limevitaka vyombo hivyo kuendelea kusimamia sheria na kuchukua hatua stahiki dhidi ya vitendo vyovyote vinavyoweza kuhatarisha amani na mshikamano wa Taifa.
Vilevile, Baraza limewahimiza wananchi kuendelea kuunga mkono utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2025–2030 na kuelewa kuwa masuala ya maboresho ya Katiba ni sehemu ya ajenda ya chama na serikali, hivyo yanapaswa kuendelea kushughulikiwa kwa mujibu wa taratibu na mipango iliyowekwa.
Baraza la UVCCM Mkoa wa Mtwara limewahimiza vijana na wananchi wote kuendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo, kudumisha umoja wa kitaifa na kuendeleza mshikamano kwa maslahi ya Taifa.