Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Sengerema wameaswa kutojihusisha na wagombea wa "mfukoni" wanaojipitisha majimboni na kata kutafuta nafasi za uongozi kabla ya wakati rasmi wa mchakato wa chama.
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mwanza, Ibrahim Kandumila, alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha Baraza la UVCCM Wilaya ya Sengerema. Amesema baadhi ya vijana wamekuwa mawakala wa wagombea hao, jambo linalokwenda kinyume na maadili ya chama.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Tukibaini kijana yeyote anajihusisha na tabia hiyo, hatutasita kuchukua hatua," alisema Kandumila, akiwataka vijana kuwa waaminifu katika kulinda viongozi waliopo madarakani badala ya kushiriki kampeni zisizo rasmi.