BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Songwe Ndg Fatuma Hussein amewatoa hofu vijana kutokana na serikali kusitisha utoaji wa mikopo ya 10% iliyokuwa ikitolewa katika ngazi za Halmashauri.
Fatuma ameleza kuwa kama UVCCM wanaamini kuwa serikali itakuja na mpango bora zaidi wa utoaji wa mikopo hivyo hivyo kuvitaka vikundi ambavyo vilikwisha undwa kuendelea kujiandaa na pindi dirisha la mikopo litakapozinduliwa wawe wa kwanza kunufaika na fedha hizo.
Aidha katika hatua nyingine Fatuma ameiomba serikali kuharikisha ujenzi wa soko la Tunduma ambalo lipo katika hatua za mwisho kwani wananchi wengi wanasubiri kwa hamu soko hilo, kwani litakuwa ndio mkombozi wa vijana wengi kujiajiri
Mwenyekiti Fatuma ameyasema hayo katika Ziara ya kamati ya utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Songwe ambapo Leo tarehe 18 Aprili wapo wilayani Momba.