BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
UVCCM WAMEMTISHA DKT. ANTHONY DIALLO NA AMEKUBALI KUTISHIKA!
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa Dkt. Anthony Diallo alizungumza na kutoa maoni yake na ulimwengu umemsikia. Alipokuwa akiongea alionekana kuwa timamu. Alionekana alikuwa na agenda na alionekana alijiiandaa vema kuwasilisha agenda zake kwa umma. Inaonekana hakuna aliyemshawishi kufanya mahojiano yale na Nyanda. Kinyume chake, huenda yeye ndiye aliyeshawishi kufanya mahojiano yale kwa kuwa alikuwa na agenda au kama hakushawishi, basi alikuwa ameridhia bila shinikizo ombi la kufanya mahojiano. Aliongea kwa ufasaha hoja zake na akajibu maswali kwa ufasaha kwa kuwa hakukuwa na shinikizo. Moja ya aliyoyaongea ni pamoja na kusema kuwa huko nyuma waliruhusu mtu mwenye rekodi ya kutibiwa Milembe kuongoza nchi!
Baada ya mahojiano yale, alikaripiwa na kufokewa vilivyo na Kiongozi wa UVCCM. Karipio limemwingia vilivyo na hivyo ameamua kuita Vyombo vya Habari ili kutoa ufafanuzi juu ya alichokuwa amekiongea. Katika ufafanuzi wake ameshindwa kujenga hoja ya kufuta hoja ya mwanzo. Badala yake anasema alikosea alitumia 'Past Tense' badala ya 'Future'! Kwamba hakumaanisha wakati uliopita kuwa waliruhusu mtu mwenye rekodi ya kutibiwa Milembe kuongoza nchi, bali alimaanisha kuwa wakati ujao inaweza kutokea!
Jina la Diallo lina kianzio cha Dkt yaani Daktari. Hatujui kama ni Daktari wa Tiba au Daktari wa Falsafa au Daktari wa Heshima! Kwa vyo vyote vile, mtu mwenye elimu ya aina hiyo hawezi kuchanganya 'Past Tense' na 'Future'! Yaani Dkt. Diallo achanganye 'madesa' kiasi cha kuita wakati ujao uwe wakati uliopita?! Shida iliyopo ni hofu! UVCCM wamemtisha Dkt. Diallo naye akajaa hofu. Matokeo yake akaita Vyombo vya Habari na kuanza kuongea hoja ambazo hakuwa nazo na wala hakujipanga! Dalili za ukosefu wa uhuru wa kutoa maoni ndani ya CCM ndio zinafunuliwa wazi sasa. Hatujui Dkt. Diallo anaogopa kupoteza cheo au heshima ndani ya CCM au anaogopa kufukuzwa!
Hofu ikiingia katika jamii ye yote ile, watu wanakosa ujasiri. Watu wanakuwa sio wakweli kwa nafsi zao. Watu wanalazimika kuongea yale ambayo nafsi zao hazikuwa tayari kuyaongea. Hatari ya kuongoza watu wenye hofu ni kubwa. Lakini hatari ya kuongoza viongozi wenye hofu ni kubwa zaidi. Kama watu wazima kama Dkt. Diallo watafikia hatua ya kutiwa hofu na vijana na kisha kulazimika kusema tofauti na walivyokuwa wamejandaa ni hatari kwa ustawi wa jamii. Hili la Dkt. Diallo na UVCCM sio msiba tu kwa CCM, bali ni msiba kwa Taifa zima. Tunatafakari nini cha kumshauri Dkt. Diallo, lakini itoshe kusema yaliyotokea ni jaribio la kutaka kuzima uhuru wake wa kutoa maoni na yeye mwenyewe amelazimika kuzimika! Hakuna jamii iliyowahi kubadilishwa na wanaozuia maoni na hakuna jamii iliyowahi kubadilishwa na waoga!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula