UVCCM wamuonya Anthony Diallo

Mwenyekiti wa CCM mkoa huwa halipwi mshahara na chama,Sasa unamuonya mtu ambaye humlipi Wala halipwi? CCM ni aibu kutokumlipa mshahara mwenyekiti wa CCM mkoa . Fikirieni hii hoja.
 
Sasa uyu nae anashindana na senior wake kwenye chama, hivi ndani ya ccm vijana hua hawafundishwi adabu, ?

Uvccm eleweni hamkijui chama chenu, KUANZIA hx na nakadhalika

That,s ndani ya chama chenu mpo makundi manne

1.ccm kindakindaki
2. Ccm limbukeni
3. Ccm Maslahi
4. Ccm halisi
 
Wengi walipigia kelele kuhusu utawala wa awamu ya 5 kuendesha nchi kiimla bila kufuata sheria na katiba huku wana CCM Mpya wa mtaa wa Lumumba wakiimba mapambio na kusifu uovu huo.

Sasa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa naye kaamua kuvunja ukimya na kusema ukweli

 
Katibu UVCCM ni Mwajiriwa.anateuliwa
M/Kiti. Mkoa anachaguliwa
Wote ni wajumbe wa vikao kitaifa
Kiprotocal UVCCM wanaweza kumuonya Mkiti wa Mkoa?
 
Ifike mahali tuheshimu mawazo au maono ya mtu hoja hupingwa kwa hoja Kama kasema kweli itabaki kua kweli lakini Kama kapotosha pinga kwa hoja iliyonyooka unaposema viongozi waliopita inaonesha unamtaja unayemjua ni yupi
 
10 Julai 2021
Tunduma, Songwe
Tanzania

UVCCM waongea kwa uchungu mkubwa kufuatia kauli ya Mwenyekiti wa CCM wa mkoa


UVCCM watoa kauli ya kulaani vikali kauli hiyo ya Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza.

UVCCM yamuomba Katibu Mkuu wa CCM kuongea na Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Mwanza Dr. Anthony Diallo.

. Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Ndugu Kenani Laban Kihongosi amesema umoja huo unaikemea na kuilaani vikali kauli Iliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii akisema kuwa kipindi cha nyuma kuna viongozi walichaguliwa kuongoza wakati wana rekodi ya kuwa vichaa na walitakiwa kuwa 'Milembe' badala yake wakapewa kuongoza nchi.

Ndugu Kihongosi amesema kuwa UVCCM imesikitishwa na kauli hiyo ya uongo ambayo pia si ya kiungwana inayolenga kutweza na kudhalilisha viongozi waliowahi kuongoza nchi sambamba na kukosa maadili ya uongozi kwa mujibu wa taratibu za chama.

"Tumesikia maneno ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza tunaamini chama chetu, kiko makini katika kusimamia maadili ya viongozi wake, UVCCM tunaamini Chama kitatafakari na kuona namna nzuri ya kushuhulikia jambo hilo kwa mujibu wa kanuni za uongozi na maadili." Alisema Kenani Kihongosi

Amefahamisha UVCCM inaamini kuwa viongozi wa chama wanatakiwa waongozwe na busara na hekima pindi wanapozungumza kuliko kuongea mambo ambayo yanaleta ukakasi na kudhalilisha Chama na Serikali jambo ambalo linakwenda kinyume na maelekezo ya kanuni za maadili na uongozi.

"UVCCM tunaikemea na kuilaani vikali kauli hiyo, Viongozi wetu waliopita waachwe wapumzike na waheshimiwe baada ya kutekeleza majukumu yao, yeye kama aliona hivyo alibakia kwenye chama kufanya nini? Akitokea kiongozi wa namna hii anakiuka maadili ya chama chetu sisi UVCCM tutanyoosha mstari kulinda kanuni na maadili ya chama chetu," Alisisitiza Kihongosi.
 
Huyu akumtaja mtu ,Uvccm hao wamenyanua mdomo , nchi hii haiwezi endeshwa KWA sifa ,cheo , au u mwanachama wa ccm kisha mko madarakani ,Kama vile Mungu akatenda nchi KWA SSH, RAIS, na Mwanamama bado laja lingine ambapo hatutategemea, ASEMA BWANA ,tujifunze elewa madaraka ni mpito tu na hatuwezi pata wote,

Ila mliobahatika jua wapo binadam wenzenu wapo nyuma na na wanatekeleza shughuli zote kadri mungu alivyowaumba Kama binadam tofauti ni kipato , na maisha tuishio
UVCCM waongea kwa uchungu mkubwa kufuatia kauli ya Mwenyekiti wa CCM wa mkoa

 
Sio walipaswa kuwa milembe
Bali kumbukumbu zao ziko huko 🤣🤣🤣🤣
 
 
Sindano imegusa mfupa!

Mtasema yote mwaka huu! Kumbe Magufuli alikuwa na file Mirembe!🤣🤣🤣
 
Diallo ni mfukuza upepo ambaye maslahi yake yaliguswa na JPM....sasa anataka huruma dunia imsikie kama naye yupo..Hapa ndio namuumgaga mkono JPM kwa kunyooosha hizi pumbavu...
 
Huyu Katibu Mkuu aliwatandika bakora wafanyabiashara Arusha.

Huo ulikuwa msimamo wa chama !.

Huyu Katibu Mkuu alihimiza adhabu ya kifo kwa Mh Zitto Kabwe huo ulikuwa msimamo wa chama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…