UVCCM wamuonya Anthony Diallo

UVCCM wamuonya Anthony Diallo

a.k.a jasusi mbobezi... alimwambia kichaa wa mirembe niguse ninuke, kama hujapotea kwenye hizo corridor za ikulu. Nchi ina mambo hii!
Mzee wa niguse ninuke kawa kimya sijui kafanikisha mission gani huyu bwana
 
Katibu wa umoja wa vijana wa CCM Khenan Kihongosi amemuonya mwenyekiti wa ccm mkoa wa Mwanza bwana Diallo kuwa aache upotoshaji mara moja, kitendo cha kusema baadhi ya viongozi waliopita walitakiwa kuwa mirembe ni cha kipotoshaji kwani Diallo yupo kwenye vikao vyote vya maamuzi kwani ni mjumbe wa kamati kuu.
===

CCM imelaani kauli ya kubeza viongozi wastaafu iliyotolewa na mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mwanza, Antony Diallo katika mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha televisheni nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Julai 10, 2021 na katibu mkuu wa umoja wa vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi katika kikao cha majumuisho ya ziara ya kuimarisha chama inayofanywa na sekretarieti ya chama hicho ikiongozwa na katibu mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.

Kihongosi amesema kauli iliyotolewa na kiongozi huyo ni msimamo wake mwenyewe na si wa CCM na kwamba jumuiya ya vijana inalaani kauli zinazotolewa na kiongozi huyo kuwabeza viongozi walioitumikia nchi, akitaka wastaafu hao kuachwa wapumzike.

"Tangu leo asubuhi tumeona ujumbe ukisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikinukuu kauli iliyotolewa na mmoja na kiongozi ambaye anaingia kwenye vikao vya maamuzi lakini leo ameamua kutoa kauli hii ambayo imetuchukiza sana vijana kwani tulitegemea wawe wa kwanza kutuongoza, " amesema.

Kihongozi amesema kiongozi huyo wa CCM ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amenukuliwa akisema viongozi wengine wanaoteuliwa na CCM wanapaswa kuwa hospitali ya magonjwa ya akili ya Mirembe iliyopo mkoani Dodoma.

MWANANCHI
Tukkulize wewe dogo.. Aliyo yasema Dialo ni kweli au uongo? Je ni uongo alitembea na mabunduki mengi? Ni uongo aliharibu protocol za utawala? Ni uongo aliharubu uchumi?? Dialo sio size yako. Wewe ni dogo sana kwenye siasa za nchi hii. Kavue dagaa
 
alitak
alitaka asidaiwe kodi kisa yeye ni mwenyekiti wa CCM?
Na vipi yule aliyechukia baada ya kuulizwa zilipo 1.5 trillion? Akamchukia na CAG maisha yake yote hadi anatwaliwa😅😅😅😅😅😂😂😂😂
 
Tukkulize wewe dogo.. Aliyo yasema Dialo ni kweli au uongo? Je ni uongo alitembea na mabunduki mengi? Ni uongo aliharibu protocol za utawala? Ni uongo aliharubu uchumi?? Dialo sio size yako. Wewe ni dogo sana kwenye siasa za nchi hii. Kavue dagaa
Kwa hiyo world bank ni waongo kwamba Tanzania imeingia uchumi wa kati?
 
Alikuwa anakipigania chama sio yule mwehu.. Diallo tunamjua ni tajiri wa kisukuma. Sio choka mbaya kama wewe
Halafu najiuliza hawa UVCCM walikuwa wapi wakati kina hapi, musiba , na wengineo wana wasema vibaya wastaafu eti leo mungu wao kuambiwa ukweli wa tabia zake wana ibuka na vioja.
 
soma katikakati ya mistari...ni daktari anayeweza kuthibitisha fulani ni kichaa... kupitia report ya daktari ndio tunaweza kuthibitisha hilo....umeshawahi kuiona hiyo report ya daktari?.....
Si kila kitu unaweza kutumia ripoti za wataalamu. Mfano huwezi ukauluza sehemu au njia wale watu wanaookota takataka na kula jalalani kwa kuwa tu huna uthibitisho wa kidaktari. Vivyo hivyo jengo refu au daraja lina nyufa unasema unaishi humo au kupita kwa kuwa tu wahandusi hawajatoa cheti cha ubovu wa miundombinu husika.

Kuna vitu vya kuangalia na kutumia common sense uliyonayo vinginevyo ukishindwa na weww unakuwa katika kundi husika lisilojitambua.

Unatumia matendo,kauli na tabia kutambua utimamu wa mtu.

Kwa kusema hivyo sio kuwa naunga mkono hoja iliyopo mezani,no.Nilikuwa nakazia juu ya matumizi ya "common sense" katika maeneo mbalimbali.
 
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita yapo mengi ya kujivunia yaliyofanywa na Serikali ya CCM.

Ulikuwepo upendeleo maalumu wa kuinua uchumi wa Mwanza.

Sasa iweje mwenyekiti wa CCM Mwanza asione yote hayo na badala yake akaongelea mbinyo wa kodi?

Kisiasa hii inamaanisha mwenyekiti huyo aliwadanganya wanamwanza katika kuinadi ilani ya CCM mwaka 2020 hivyo inambidi awajibike.
 
Usidhani watu kukaa kimya baada ya kutishwa na yule kiongozi muovu hawajui uovu aliokuwa anaufanya. Nenda Afrika kusini uone kama weusi tuliokuwa tunawaunga mkono, kama wanamsifia Kaburu Pieter Botha aliyejenga Afrika kusini.

Kama maendeleo ni kigezo cha watu kuvumilia uovu, ni kwanini Nyerere alipoteza raslimali za taifa kuwasaida weusi wa Afrika kusini, wakati nchi yao ilikuwa inapata maendeleo makubwa kuliko hata sisi Tanzania?
 
Back
Top Bottom