UVCCM wamuonya Anthony Diallo

UVCCM wamuonya Anthony Diallo

Usidhani watu kukaa kimya baada ya kutishwa na yule kiongozi muovu hawajui uovu aliokuwa anaufanya. Nenda Afrika kusini uone kama weusi tuliokuwa tunawaunga mkono, kama wanamsifia Kaburu Pieter Botha aliyejenga Afrika kusini.

Kama maendeleo ni kigezo cha watu kuvumilia uovu, ni kwanini Nyerere alipoteza raslimali za taifa kuwasaida weusi wa Afrika kusini, wakati nchi yao ilikuwa inapata maendeleo makubwa kuliko hata sisi Tanzania?
Shida ya CCM ukisema ukweli wewe ni adui namba 1 wanataka kusifia full time
 
Avuliwe nafasi zote za uongozi ndani ya Chama.
Ni kweli kama angalikuwa CDM angalivuliwa nafasi zake zote za uongozi na kufukuzwa uanachama kama walivyofanywa akina Halima Mdee, kwa kosa la kukisaliti chama. CCM haiko hivyo, ni wastaarabu.
 
Avuliwe nafasi zote za uongozi ndani ya Chama.
Vichaa ccm ndio chimbo lao
Screenshot_20210711-094708_Twitter.jpeg
 
Ninaanza kuamini kuwa kuna vifo hufurahiwa na watu wengi.
 
Diallo ni mfukuza upepo ambaye maslahi yake yaliguswa na JPM....sasa anataka huruma dunia imsikie kama naye yupo..Hapa ndio namuumgaga mkono JPM kwa kunyooosha hizi pumbavu...
Ni pumbavuu kwel kwel..na zilinyoroshwaa haswaaa..shenzi kabisaaa..walishajimilikisha chama..na nchi kwa ujumlaa..sasa wanaanza kupayuka payukaa jinga kabisaa haoo
 
Hii inaonesha kuwa wamekubaliana
na jambo hili.
Haiwezekani aliyekuwa Mkuu wa Nchi aitwe Mwehu afu Viongozi Wakuu wa Chama wasitoe tamko lolote.
Ni dhahiri kuna genge liko nyuma ya Dialo.
 
Mimi nilifikiri angalau wangempongeza kwa kujaribu kujitoa kundi la wanafiki,ili angalau warejee kwenye misingi,hapa dawa ni Katiba mpya dawa ya waliojimilikisha nchi na vyote vilivyomo . Ili ujumbe ufefika na mimi nasimama nae.
Atafukuzwa kwenye chama
 
Katibu wa umoja wa vijana wa CCM Khenan Kihongosi amemuonya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza bwana Diallo kuwa aache upotoshaji mara moja, kitendo cha kusema baadhi ya viongozi waliopita walitakiwa kuwa Mirembe ni cha kipotoshaji kwani Diallo yupo kwenye vikao vyote vya maamuzi kwani ni mjumbe wa kamati kuu.
===

CCM imelaani kauli ya kubeza viongozi wastaafu iliyotolewa na mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mwanza, Antony Diallo katika mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha televisheni nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Julai 10, 2021 na katibu mkuu wa umoja wa vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi katika kikao cha majumuisho ya ziara ya kuimarisha chama inayofanywa na sekretarieti ya chama hicho ikiongozwa na katibu mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.

Kihongosi amesema kauli iliyotolewa na kiongozi huyo ni msimamo wake mwenyewe na si wa CCM na kwamba jumuiya ya vijana inalaani kauli zinazotolewa na kiongozi huyo kuwabeza viongozi walioitumikia nchi, akitaka wastaafu hao kuachwa wapumzike.

"Tangu leo asubuhi tumeona ujumbe ukisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikinukuu kauli iliyotolewa na mmoja na kiongozi ambaye anaingia kwenye vikao vya maamuzi lakini leo ameamua kutoa kauli hii ambayo imetuchukiza sana vijana kwani tulitegemea wawe wa kwanza kutuongoza, " amesema.

Kihongozi amesema kiongozi huyo wa CCM ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amenukuliwa akisema viongozi wengine wanaoteuliwa na CCM wanapaswa kuwa hospitali ya magonjwa ya akili ya Mirembe iliyopo mkoani Dodoma.

MWANANCHI
Kenan akumbuke kuwa Sabaya yuko nyuma ya nondo! Aweke maneno ya akiba
 
Back
Top Bottom