UVCCM wamuonya Anthony Diallo

UVCCM wamuonya Anthony Diallo

Muulize mtoto wa mjini DC mpya Lijualikali au muulize Sumaye aliambiwa sumu haionjwi
Hivi ndivyo jinsi ya kuthibitisha tuhuma?Ungeulizwa na mahakama kuwa thibitisha tuhuma zako ungeiambia mahakama kuwa ikamuulize Lijuakali?Nikikuambia kuwa kichwani una funza badala ya ubongo nitakuwa nimekuonea?Vijana wa CCM mna tatizo gani katika kufikiri na katika kujenga hoja?Mna laana gani?
 
Hivi ndivyo jinsi ya kuthibitisha tuhuma?Ungeulizwa na mahakama kuwa thibitisha tuhuma zako ungeiambia mahakama kuwa ikamuulize Lijuakali?Nikikuambia kuwa kichwani una funza badala ya ubongo nitakuwa nimekuonea?Vijana wa CCM mna tatizo gani katika kufikiri na katika kujenga hoja?Mna laana gani?
Diallo ameomba radhi kwa upupu wake
 
Comrade Anthony Diallo amesema maneno mazito.

Ametimiza ahadi ya mwana TANU/CCM isemayo "Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko".

Ukweli uliochelewa ni bora kuliko uwongo uliowahi.
Ukweli umefika msikilizaji kasepa
 
Bila shaka anapaswa kujiuzulu
Kauli yake imewaponda mpaka waliompitisha mgombea, nao wanaonekana waliambukizwa ugonjwa walipokwenda kumtazama mgonjwa milembe, Diallo ajiandae kuunganishwa na Jasusi Bobezi aka Niguse Nismell
 
Amesema ameeleweka vibaya na Chadema
Chadema wameuziwa kesi bila kutaka, sikuwa najua kuwa Kenani Kihongosi ana kadi ya Chadema kisirisiri, mmmh!! Watu ni wasaliti balaa!🤣
 
Khenan, Diallo si saizi yako.
Watoto kama hao hawana heshima, malezi waliyopitia ndani ya CCM yamewaathiri kiakili na kisaikolojia. Unaweza kukuta kijana mwenyewe labda kazaliwa kwenye mikesha ya mwenge! CCM imewaharibu sana vijana wetu.

Usanii12.jpg
Usanii10.jpg

 
Na nyie nendeni startv mtuambie ukweli ni upi, tushachoka....
 
Katibu wa umoja wa vijana wa CCM Khenan Kihongosi amemuonya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza bwana Diallo kuwa aache upotoshaji mara moja, kitendo cha kusema baadhi ya viongozi waliopita walitakiwa kuwa Mirembe ni cha kipotoshaji kwani Diallo yupo kwenye vikao vyote vya maamuzi kwani ni mjumbe wa kamati kuu.
===

CCM imelaani kauli ya kubeza viongozi wastaafu iliyotolewa na mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mwanza, Antony Diallo katika mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha televisheni nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Julai 10, 2021 na katibu mkuu wa umoja wa vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi katika kikao cha majumuisho ya ziara ya kuimarisha chama inayofanywa na sekretarieti ya chama hicho ikiongozwa na katibu mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.

Kihongosi amesema kauli iliyotolewa na kiongozi huyo ni msimamo wake mwenyewe na si wa CCM na kwamba jumuiya ya vijana inalaani kauli zinazotolewa na kiongozi huyo kuwabeza viongozi walioitumikia nchi, akitaka wastaafu hao kuachwa wapumzike.

"Tangu leo asubuhi tumeona ujumbe ukisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikinukuu kauli iliyotolewa na mmoja na kiongozi ambaye anaingia kwenye vikao vya maamuzi lakini leo ameamua kutoa kauli hii ambayo imetuchukiza sana vijana kwani tulitegemea wawe wa kwanza kutuongoza, " amesema.

Kihongozi amesema kiongozi huyo wa CCM ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amenukuliwa akisema viongozi wengine wanaoteuliwa na CCM wanapaswa kuwa hospitali ya magonjwa ya akili ya Mirembe iliyopo mkoani Dodoma.
1626023877414.png

MWANANCHI
Dah!!!!

1626023877130.png
 
Kauli yake imewaponda mpaka waliompitisha mgombea, nao wanaonekana waliambukizwa ugonjwa walipokwenda kumtazama mgonjwa milembe, Diallo ajiandae kuunganishwa na Jasusi Bobezi aka Niguse Nismell
Ameshangaza sana
 
Back
Top Bottom