Elections 2015 UVCCM yamvaa LOWASSA, yakerwa na kauli zake za kutetea wabakaji, wamshangaa SUMAYE

Elections 2015 UVCCM yamvaa LOWASSA, yakerwa na kauli zake za kutetea wabakaji, wamshangaa SUMAYE

UVCCM hatutegemei mmuongelee vizuri Lowasa,na hiyo ni moja ya hoja zenu mlizolua mnazijadili ngurudoto za kumchafua Lowasa. Lowasa anakubalika nadni ya ccm na nnje ya ccm. Watanzania wanahitaji mabadiliko kupitia Lowasa. Hata mkimchafua kiasi gani lakini jembe letu ikulu lazima liingie.
 
UVCCM hatutegemei mmuongelee vizuri Lowasa,na hiyo ni moja ya hoja zenu mlizolua mnazijadili ngurudoto za kumchafua Lowasa. Lowasa anakubalika nadni ya ccm na nnje ya ccm. Watanzania wanahitaji mabadiliko kupitia Lowasa. Hata mkimchafua kiasi gani lakini jembe letu ikulu lazima liingie.
ndoto za mchana...
 
Upuuzi mwingine huu...angeongea kwa mtitiriko ndo mgemsaport! Inawauma nini/ Umati ule ulikuwa,wa kwenu? Mlifingua kampeni zenu tuliona....ya jana ilikuwa ya ukawa.
 
Baba zao wako wapi?mbona vijana wanakereka kuliko baba zao?wapumbavu wakiamua wanaamua bana
 
wakitoka kwenu mafisadi wakiwa kwenu wasafi, swali, je! Mnaweza kutuambia baadhi ya mafisadi ambao bado mko nao kabla hawajahama? Je, ni lini serikali ya ccm imewatangaza mafisadi? Kwa maana hyo ccm inaongoza serikali ya kifisadi hasa awamu hii ya mwisho akiwepo baba mwenye nyumba!
 
Sasa tumejua,fisadi wa Richmond ni Kikwete!
 
Mdogo wangu Mtela Mwampamba hivi ulipokuwa Chadema ulikuwa na Cheo gani? Kusema ukweli nakuonea huruma na roho inaniuma sana, yaani ulikuwa una bright future ya kisiasa lakini sasa hata ukiongea unachukuliwa kama mtu mwenye kutema pumba tu

yashike sana haya maneno yangu, JK akishatoka madarakani kama mwenyekiti wa CCM, wewe na yule dada mliyekimbilia CCM ndio utakuwa mwisho wa habari yenu,
kuna kitu mlikuwa hamkijui mwanzo, CCM ina wenyewe, ni ngumu sana kwa kijana usiye na jina na pia haumo ndani ya mfumo wao kuwa na maana ndani ya chama, umemuona Makonda alivyokuwa anamlamba miguu Rizimoko na matokeo yake umeyaona? ni tofauti sana na ilivyo Chadema ambayo inamnyanyua mtu kutoka kusikojulikana na kuwa jina kubwa kisiasa, Nyie mmetoka Chadema, kuna vijana kama Mwalim wamechipuka na ndio wanashine sasa

Muda bado upo na umri unakuruhusu, omba radhi na rudi kwenye Chama unachokipenda

hivi umemuona Hizza jana, CCM walishampoteza
 
Last edited by a moderator:
Jamani si kazindua Jana tu kampeni na sasa yupo iringa? akimaliza wiki mtakuwaje kama Jana tu mkakesha kuandaa tamko! Yatakayoongelewa Iringa kesho mje na tamko lingine!
 
Mdogo wangu Mtela Mwampamba hivi ulipokuwa Chadema ulikuwa na Cheo gani? Kusema ukweli nakuonea huruma na roho inaniuma sana, yaani ulikuwa una bright future ya kisiasa lakini sasa hata ukiongea unachukuliwa kama mtu mwenye kutema pumba tu

yashike sana haya maneno yangu, JK akishatoka madarakani kama mwenyekiti wa CCM, wewe na yule dada mliyekimbilia CCM ndio utakuwa mwisho wa habari yenu,
kuna kitu mlikuwa hamkijui mwanzo, CCM ina wenyewe, ni ngumu sana kwa kijana usiye na jina na pia haumo ndani ya mfumo wao kuwa na maana ndani ya chama, umemuona Makonda alivyokuwa anamlamba miguu Rizimoko na matokeo yake umeyaona? ni tofauti sana na ilivyo Chadema ambayo inamnyanyua mtu kutoka kusikojulikana na kuwa jina kubwa kisiasa, Nyie mmetoka Chadema, kuna vijana kama Mwalim wamechipuka na ndio wanashine sasa

Muda bado upo na umri unakuruhusu, omba radhi na rudi kwenye Chama unachokipenda

hivi umemuona Hizza jana, CCM walishampoteza

Akitahamaki washamsahau! kuna vyama ukiwa kiongozi watu wanakuona kichwa na wanataka kusikia kuhusu wewe na chama hicho ni cdm siyo ccm
 
Last edited by a moderator:
Usaliti ulioufanya kwa wana Mbozi hautakuja kukufanya uwe huru maisha yako yote. utabakia kutumika na kutumiwa.
 
shaka.jpg


TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA WA CCM ( UVCCM) MAKAO MAKUU DAR ES SAALAM KWA VYOMBO VYA HABARI JUMAPILI 30 AUGUST 2015.


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Agosti 29 kimezindua kampeni zake katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo viongozi kadhaa wa Chama hicho wakiwemo na waliokuwa Mawaziri waandamizi katika Setikali ya CCM, Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi, Edward Lowassa pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Lawrance Masha wakihutubia mkutano huo.

Ni jambo la kushangaza kumsikia mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa akihemewa na Kujikuta akishindwa kuikabili hadhira ya Watanzania wanaofikia milioni 45 kuwaelezea ana malengo gani ya urais, Chama chake kina dira na sera zipi za msingi, pia akizungumza bila kuonyesha mtiririko wa sera kusudiwa kama muongozo wa uendeshaji Serikali ukikosa kuainishwa kwenye kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.Kwa msingi huo, CHADEMA/UKAWA wameonesha jinsi gani wasivyo na maandalizi ya mkakati wa kitaalam na mipango endelevu kwa maendeleo ya kisekta katika dhamira ya kujenga uchumi imara utakaoimarisha huduma za jamii, kuheshimu misingi ya utawala bora wa sheria huku akionesha kukosa dira makini ikiwemo mipango ya muda mfupi na muda mrefu ya Serikali yao ikiwa itatokea muujizq wa wa kushinda na kujikuta wakitaja changamoto zinazozikabili nchi nyingi zinazoendelea.

Mgombea wa CHADEMA Lowassa ni dhahiri ameshindwa uchaguzi mkuu mapema, amebakia akilalama, kupiga soga na kujenga matumaini hewa kwa Watanzania huku akishindwa kujua ni changamoto zipi za msingi zinazowakabili wananchi katika maisha ya kila siku na hatimaye atoe majawabu mbadala ya utatuzi wa msingi unaoweza kuaminiwa na wananchi wanaoishi aidha mijini au vijijini.

Lowassa ameshindwa kabisa kukonga nyoyo na kugusa hisia za Watanzania katika mambo ya msingi kwa sababu ya kuandamwa kwake na pupa, kiherehere na kukurupuka toka Chama kimoja hadi kingine huku akiwa hana maandalizi yanayoweza kutoa majibu halisi yanayowakabili wafanyakazi, wakulima, wavuvi, wafugaji, walimu, madaktari, wauguzi pia wasanii na wanamichezo.

Lowassa na CHADEMA, wameshindwa kubainisha dhamira na maandalizi ya kuleta chachu ya maendeleo mbadala kwa sababu sehemu kubwa ya changamoto zilizokuwepo zimetatuliwa hatua kwa hatua kwa kipindi cha miaka kumi iliopita chini uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambapo sasa mashirika ya Kimataifa ya kusimamia uchumi na fedha ikiitaja Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kuelekea uchumi wa kati.

Sisi UVCCM, tulitegemea sana kuona labda ile shauku , mikiki , hamu na kiu alionayo Lowassa ya kutamani Urais kwa gharama yoyote huenda angekuwaa na mikakati. , sera au mipango mipya ya kushughulikia matatizo yaliyobaki ambayo aidha yamekawia kiutekekezaji kwa ukosefu wa fedha au utatuzi wa matatizo hayo miradi husika imeanzishwa na kutofikiwa suluhisho kwa wakati au baadhi ya viongozi waliopewa dhamana hizo kushindwa kutekeleza kwa muda na wakati muafaka.

Hotuba ya Lowassa kuhusu azma na dhamira yake katika kukuza uchumi, UVCCM tunaifananisha na orodha ya manunuzi (shop list) maana haioneshi viashiria , njia au vyanzo vya mapato ya kukuza uchumi kwa mwendo haraka wa kisera na kujikuta akipiga porojo akifanana na kasuku aliyekariri maneno aliyofundishwa akiyatumia bila kujuwa tija , faida, hasara na maana ya jambo analolikusudia.

Tumeshangaa kumuona akishindwa kuzungumzia masuala ya ufisadi na kutowataja wezi waliopora rasilimali za umma na maliasili za nchi, waliofuja uchumi, wala rushwa watu waliokosa kuwajibika na kutochukuliwa hatua za kisheria kwa masuala mazima ya kukiuka maadili ya uongozi ikiwemo sakata zito za mradi wa kufua umeme wa dharura kupitia kampuni hewa ya RICHMOND ambayo ilimsababishia Lowassa kulazimishwa na Bunge ajiuzulu Uwaziri Mkuu akiwa ni Waziri Mkuu aliyekaa muda mfupi zaidi kuliko yeyote katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

UVCCM tunachukua nafasi hii kuwaasa na kuwaomba sana Watanzania wenzetu kwamba mabadiliko au mageuzi ya kiuchumi na kisiasa hayahitaji pupa na papara kama iliyotokea kwa wananchi wa Taifa la Libya ambao sasa wako katika dimbwi la majuto.

Viongozi wa Upinzani akiwemo Lowassa na kundi la UKAWA hawana dhamira njema kwa nchi yetu na UVCCM tunawafanisha sawa na manahodha ambao muda mfupi ujao toka sasa watagombea sukani wakiwa katika kina kirefu cha bahari jambo ambalo ni hatarishi kwa maisha na mustakabali wa wasafri waliomo kwenye chombo chenye amani, utulivu, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa kinachoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lowassa ameonyesha dalili za kuwa kiongozi dikteta asiyeheshimu hata misingi ya utawala bora hasa pale aliporejea kwa mara ya pili akisisitiza msimamo wake wa kuwaachia huru Masheikh wanaokabiliwa na tuhuma za makosa ya ugaidi ambapo suala hilo sasa lipo mbele ya mahakama na hatutakiwi kuingilia mwenendo wa kesi kulingana na matakwa ya mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili ya dola.

Mbali na suala hilo, pia ameonekana kulizungumzia suala ambalo tayari mahakama ya juu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekwisha litolea hukumu kesi ya Mwanamuziki Nguza Viking na mwanawe Papii Kocha waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ubakaji kana kwamba Lowassa anaona vyombo vya sheria vimewaonea na kuwakandamiza.Ifahamike kati ya makosa ambayo yameainishwa katika sheria za Tanzania, kosa la ubakaji halina msamaha.Aidha, Lowassa na UKAWA wameonekana kuzungumzia sana dhana ya uzalendo wakati mfumo utokanao na itikadi ya Chama chao imejiegemea katika uliberali usiojali wala uzalendo zaidi ya kuthamini utajiri binafsi, kujilimbikizia mali zisizo na vyanzo na uvukaji wa mipaka isiyozingatia mila, desturi na utamaduni.


UVCCM tumeshangazwa sana na ujasiri uchwara ulionyeshwa na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye anapothubutu kuzungumzia ufisadi wakati yeye mwenyewe ni miongoni mwa viongozi wanaotuhumiwa kwa kashfa ya uanzishaji wa Televesheni ya Taifa {TVT} na ufufuaji wa fedha za umma , soko la Kibaigwa, tuhuma ya uporaji ardhi huko Tondoloni akitumia madaraka yake vibaya pia chini ya usimamizi wake akiwa mtendaji mkuu wa Serikali, halmamshauri nyingi za wilaya nchini ziliongoza kupata hati chafu kutokana na matumizi holela ya ruzuku toka serikali kuu kama ilivyofichuliwa na ofisi ya CAG kufuatia upotevu wa fedha za miradi ya maendeleo ya jamii.

Sumaye kinywa chake wakati mmoja kikitoa moto na baridi ndiye aliyekitaka Chama cha Mapinduzi kutompitisha Lowassa kuwa mgombea urais kwa madai ya kuhusika kwake na tuhuma za ufisadi huku akitishia kuhama CCM. Matamshi ya Sumaye yameushangaza ulimwengu na sasa anapopania kumsafisha Lowasa kwa kutumia maji taka akifikiri atasafika ili aaminiwe na watanzania werevu na wazalendo ajijue fika anatwanga maji kwenye kinu.
SHAKA HAMDU SHAKA (MNEC)KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TANZANIA

uvccm ni vikaragosi wafa njaa wenye kutumika kama ndom.
tangu lini mtu wa kutoka ccm akasema cha maana??

LOWASSA NI WA CHADEMA NYIE WA CCM.ANAWAHUSU NINI??


KANYENI NA BAO LENU LA MKONONI MTAFUNGANA WENYEWE MWAKA HUU HATUTAK UPUMBAVU
 
Huyu Shaka msema hovyo huko kwao Zanzibar nsiye katumwa na hawa wachovu kuwatolea tamko?!
 
UVCCM hatutegemei mmuongelee vizuri Lowasa,na hiyo ni moja ya hoja zenu mlizolua mnazijadili ngurudoto za kumchafua Lowasa. Lowasa anakubalika nadni ya ccm na nnje ya ccm. Watanzania wanahitaji mabadiliko kupitia Lowasa. Hata mkimchafua kiasi gani lakini jembe letu ikulu lazima liingie.

Hizo ni mbinu za kutapatapa kwa ccm na hazitasaidia chochote kuiokoa ccm,watanzania tumeshaamua kuipiga ccm chini
 
Back
Top Bottom